Nina maanisha kwamba kwa vile EATV inaangaliwa na vijana wengi na watu wa rika mbalimbali ingekuwa kioo kwa jamii kuwaeleza ukweli watu wa rika tofauti umuhimu wa kuchagua viongozi bora na si bora viongozi.
Ingeweza kuwekeza katika kuielimisha jamii kwa kuwaita watu mbalimbali wenye mawazo chanya kuhusu Taifa letu na si pro vyama ambao wataenda kuelezea uzuri wa vyama vya na ubaya wa vyama vya upinzani.
Ni TV ambayo ingeweza kuwaibua vijana wenye ,maono ambao wangeweza kuwa viongozi wazuri baadaye mfano kuna akina betlehem,The Big show,Mchambuzi na wengine kama hawa ambao wako tayari kutetea utaifa wao.
Hata JF kuna wengi tu ambao wangeweza kuitwa kuielezea jamii yetu nini tunatakiwa kufanya,umuhimu wa vijana kujiandikisha kwa ajili ya kupiga kura na umuhimu wa jamii bila kujali umesoma au haujasoma umuhimu wa kupiga kura ili kuchagua viongozi bora.
Siyo sahihi kwa watanzania kukaa baa au sehemu yoyote kusubiri matokea ya uchaguzi wakati haujaenda kupiga kura ukiulizwa unasema ah nimeona ujinga kwenda kwani mwisho wa siku wataiba kura,sidhani kama watu wengi wakienda kupiga kura ile impact ya kuongeza kura za wizi itakuwa kubwa.
Hilo ndilo wazo langu kaka sina jingine zaidi ya hilo.Labda ulitengeneze vizuri zaidi kuliweka vyema ili lieleweke maana kiswahili ni chetu lakini kuna wakati kinazingua pia.