Unaonaje wewe? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unaonaje wewe?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Asulo, Aug 26, 2012.

 1. Asulo

  Asulo JF-Expert Member

  #1
  Aug 26, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 733
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wakuu habari za weekend...

  Mr Bony ni rafiki yangu,ambaye tumefahamiana kwa muda mrefu sasa,anafanya kazi chini ya wizara ya Elimu na..natumai mnaielewa hiyo wizara.

  Miaka ipatayo 6 iliyopita Bony kabla hajaoa alikuwa na mahusiano na binti m1 aliyempenda sana.

  Kwa bahati mbaya au nzuri,yule binti alishika mimba bila kuwa wamepanga,Kwa kuwa Bony alimpenda kwa dhati yule binti,aliamua kumuoa ili waanzishe familia..maana binti alikuwa nyumbani tu bila kazi yoyote.

  Kwa kuwa binti(Tina) alikuwa amesoma hadi kidato cha 4,mara alipojifungua Bony aliamua kumpeleka chuo cha ualimu ili waje kusaidizana maisha na mkewe Bi Tina.

  Kwa kipindi chote wakati Tina akiwa chuoni Bony alikuwa akimlea mtoto wao ambaye alikuwa bado ni mdogo.

  Hatimaye Tina alifanikiwa kumaliza masomo yake kupangiwa kituo cha kazi..Japo kituo alichopangiwa Tina hakikuwa karibu na nyumbani,alikuwa akienda na kurudi kila siku kitu ambacho kilikuwa kinawaingiza ktk gharama kubwa,Lakini baadae Bony alijitahidi kumwamisha mke wake na akafanikiwa kumsogeza karibu.

  Baadae walifanikiwa kupata mtoto wa pili.

  Bony yeye ni mwl wa Upili ila Tina ni mwl wa msingi.

  Kama unavyojua kwa wizara hiyo hailipi mishahara mizuri kwa watumishi wake,hivyo Bony alimwambia mke wake kuwa atakopa fedha bank ili waanze ujenzi wa nyumba yao ,maana walikuwa wakiishi ktk nyumba ya serikali aliyopewa Bony na shule.

  Walifanikiwa kupata ela na kununua kiwanja na kuanza ujenzi.

  Lakini kwa bahati mbaya Tina akaanza kuwa na tabia mbaya ambazo hakuwa nazo hapo awali..Kwa makusudi na yeye akaenda kuchukua mkopo bank bila mumewe kujua,hadi siku moja Bony ktk kufanya usafi ndo akakumbana na slip salary ya mkewe na kubaini hilo.

  Alipomuuliza mkewe kuhusu hilo,Tina alida kuwa mama yake alikuwa na shida ya ela ndo maana akaenda kukopa hizo 4milion..Bony akamuuliza sasa mbona hukunishirikisha hali unajua mi nimeshakopa kwa ajili ya ujenzi? Mkewe hakuwa na jibu..jamaa akaipotezea baada ya kusikia mkwewe ndo alikuwa na shida.

  Wakati wa ujenzi wa nyumba yao mke mara nyingi alikuwa akipenda kujifanya kwenda kusimamia ujenzi,kumbe alikuwa na mambo ya siri ya kipuuzi na m1 wa mafundi wao.. Watu wengi mtaani wakajua kuhusu hilo ila ilikuwa si rahisi kwenda kumwambia Bony kwa kuhofu kuonekana mmbeya,Lakini baadae Bony alikuja kuhisi kitu kati ya fundi na mkewe, ndipo siku moja alipomfata rafiki yake mwingine kumweleza kuwa anahisi tabia ta mkewe imebadilika, Ndipo huyo bwana akamweleza kile kinachoendelea kati ya mkewe na fundi wake..(Fundi akawa fundi wa vyote)

  Bony alimbana mkewe kuhusu shutuma hizo,na mkewe alikiri kutoa uroda kwa fundi,hivyo aliomba msamaha kuwa hatarudia tena. Bony alimsamehe mkewe na kuendelea na maisha yao. Tangu mwezi huu umeanza mke ameanzisha tabia tena za ajabu..Kila leo anaondoka nyumbani kwa safari zisizo na maana,kisingizio ni harusi leo atasema ya John,baada ya wiki atasema Dick na wengine ambao hata mumewe hawajui..mbaya zaidi kila akienda analala huko huko. Wiki 2 zilizopita usiku mida ya saa5, wakiwa wamejipumzisha Tina alipigiwa simu na kidume kingine,Ila hakuipokea,alupoulizwa na mumewe alidai kuwa ni bwana wa rafiki yake,Bony alikasirika sana na kutaka sababu za kwa nini apigiwe yeye usiku ule Kama si bwana wake? Mke alikuja juu na kumwambia amua utaloamua.

  Lakini Bony hakufanya kitu na asbh alikuja kuniomba ushauri.

  Juzi mkewe kamuaga kuwa kuna vitu anafatilia Mwnz maana anaishi Shy, alipotaka kujua ni nini mkewe alimjibu utajua hayo mabo yakishakamilika..Mbaya zaidi alipoondoka tu alizima simu hadi aliporudi nyumbani kwake siku iliyofuata.

  Mumewe alipomuuliza kuhusu alichofuata huko na kuhusu kuzima simu..alidai kuwa simu ndiyo kikwazo cha yeye kutofanikiwa..Bony akahoji sasa mbona uliichukua Kama ni kikwazo na ulipofika huko ndo ukazima, inamaana ulinizimia mimi au? Mkewe hakuwa na jibu zaidi ya kuondoka kwa hasira...

  Bony anaomba msaada wako wa ushauri..Amfukuze mkewe Tina au? Na vp kuhusu watoto? Na ile nyumba yao wanayojenga je? Kumbuka ni mkewe wa ndoa.
   
 2. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #2
  Aug 26, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Man's mind, once stretched by a new idea, never regains its original dimensions.
   
 3. Asulo

  Asulo JF-Expert Member

  #3
  Aug 26, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 733
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu toa ushauri wako acha kuponda
   
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  Aug 26, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Aamue kuwa mtu wa haki
  amalizie nyumba ili mkewe aishi na watoto
  ahame na kuanza life upya...
   
 5. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #5
  Aug 26, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  huyo mwanamke ni mzinzi by nature......alishajaribu kumshushia kichapo?
   
 6. BIF

  BIF Member

  #6
  Aug 26, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uyo ni wa kumuacha tu hakuna cha kusubiri apo mana baadae atakuja kupata kubwa zaidi ya hayo aliyopata,tena uyo jamaa ana moyo sana na ni mvumilivu sana,mimi nampa hongera sana mana amevumilia sana.
   
 7. Mtalingolo

  Mtalingolo JF-Expert Member

  #7
  Aug 26, 2012
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 2,188
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  It can work sometime eeh??
   
 8. Mtalingolo

  Mtalingolo JF-Expert Member

  #8
  Aug 26, 2012
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 2,188
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mmh ila hii taasisi yandoa inamambo mengi sana.
   
 9. c

  christmas JF-Expert Member

  #9
  Aug 26, 2012
  Joined: Jul 21, 2011
  Messages: 2,605
  Likes Received: 275
  Trophy Points: 180
  ni wakati huu ndio msimu wa vioja kwenye ndoa na hasa vinavyoletwa na wanawake au vilikua toka zamani coz to me wanawake sasa wamezid duuh
   
 10. F

  Fidelis big Senior Member

  #10
  Aug 26, 2012
  Joined: Aug 31, 2011
  Messages: 114
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mie ndo maana nachukia ndoa za kikiristo,talaka kwetu mwiko! USHAURI wangu apige chini huyo malaya atamletea maradhi
   
 11. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #11
  Aug 26, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Maelezo yako Asulo yanaonyesha wazi wazi kuwa mkewe ameanza tabia mbaya za uhuni. Kwenye ndoa kuna mambo ya kuvumilia lakini kama umeshamuonya mtu kwa tabia za uhuni zaidi ya mara moja na still anaendelea, kuvumilia zaidi ya hapo ni kusubiri magonjwa au kuja kupigwa na hivyo vibwana vya mumewe. Kama mwanamke amefikia hatua ya kuondoka nyumbani anavyopenda na kurudi anavyotaka na sasa anadiriki kusafiri na kuzima simu then ni uvumilivu gani hapo unaohitajika? Anavumilia kusubiri kifo? Akapime HIV kama yuko safi ni heri ya lawama kuliko fedheha, ni bora kumpiga chini haraka!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. Asulo

  Asulo JF-Expert Member

  #12
  Aug 26, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 733
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwa hiyo unamaanisha amuache kimya kimya?
   
 13. Asulo

  Asulo JF-Expert Member

  #13
  Aug 26, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 733
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwa kweli Bony ni mpole sana..hajawahi kuunyanyua mkono wake kumpiga mkewe.
   
 14. Asulo

  Asulo JF-Expert Member

  #14
  Aug 26, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 733
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu kiukweli jamaa ni mpole hadi kapitiliza. Mi mwenyewe nilishangaa alivyonisimulia mkasa wake wote wa ndani.
   
 15. Asulo

  Asulo JF-Expert Member

  #15
  Aug 26, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 733
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu jamaa ameshawaza sana kumpiga chini,ila anahofu juu ya watoto wao..Na akifikiria ni vile ndoa ni ya kanisani.
   
 16. j

  jeneneke JF-Expert Member

  #16
  Aug 26, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 760
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Sana jamani tena ambayo mtu huwezi kuamini inaogopesha!hajampeleka hata kwa wazazi?amkali kimya mwezi na chumba ahame aone respond ya mke ndo amue cha kufanya
   
 17. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #17
  Aug 26, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  BIF, Banded Iron Formation????
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. k

  kabye JF-Expert Member

  #18
  Aug 26, 2012
  Joined: Nov 4, 2011
  Messages: 355
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  danger
   
 19. Asulo

  Asulo JF-Expert Member

  #19
  Aug 26, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 733
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu ni very danger..
   
 20. ELFU-ONEIR

  ELFU-ONEIR Senior Member

  #20
  Aug 26, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 183
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyo mdada ni wakutupa kule kabla giza halija ingia
   
Loading...