Unamuamini Mungu! Je, Yeye anakuamini?

Unamuamini Mungu! Je, Yeye anakuamini?

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,741
Reaction score
25,681
Kila binadamu ukimuuliza katika dunia hii kama anamwamini Mungu, atakwambia kwamba kweli anamuamini. Ni sawa, inawezekana hata kwa muovu wa kwanza duniani anamwamini Mungu, lakini swali linakuja, je, Yeye Mungu anakuamini kama unavyomuamini?

Kuna kitu ningependa kukwambia jioni ya leo kwamba unapomuomba Mungu kitu, cha kwanza kabisa ni kukutazama kama anakuamini au la. Unamuomba Mungu utajiri, uwe mfanyabiashara mkubwa mno, lakini je, Mungu akikupa bilioni moja leo, utaendelea kuwa karibu naye?

Kuna wengine wanamuomba Mungu milioni kumi huku wakiahidi kwamba watamshukuru Mungu, anachokifanya ni kukupa lakini moja aone utafanya nini. Cha ajabu, unakwenda kufanya starehe, hukumbuki watu wenye matatizo, hata mama nyumbani humkumbuki.

Mungu hawezi akakupa bilioni moja uliyoomba na wakati umeshindwa hata kumfanya akuamini katika ile laki moja aliyokupa. Ndugu yangu, tuyatengenezeni maisha yetu, Mungu atuamini kama tunavyomuamini, tukifanikiwa, tutakuwa mabilionea siku moja, tutapata kila kitu tunachokitaka, lakini tusipomfanya Mungu atuamini, kila siku tutakuwa tunamuomba pesa nyingi lakini atakachotuma ni kidogo mno na kile tunachohitaji.

Kuna wengine wanapata utajiri, hakai na familia, kila siku kulala nje kiasi kwamba mpaka mke anamuomba Mungu auchukue utajiri wa mumewe ili mapenzi yarudi, watoto wanamlilia Mungu auchukue utajiri wa baba yao ili arudi nyumbani kwani hali inatisha sana.

Mungu hataki kukupoteza, wakati mwingine anajua kabisa kwamba kama nikimpa Nyemo hii milioni 100, mtaani watakoma, atafanya fujo na mwisho wa siku kutupwa gerezani. Huyu Nyemo nikimpa gari, aisee ataendesha kwa fujo kutaka sifa kwa wanawake, kuna siku atapata ajali na kufa, ili nimuokoe, nisimpe gari, nisimpe pesa kwani atanisahau.

So wakati mwingine Mungu hatupi vitu fulani kwa sababu bado hajatuamini kwani ni mara nyingi amekuwa akitupa vitu vidogo lakini hivyohivyo tunamkufuru kwa kufanya mambo ambayo yanampelekea kujuta kutugawia vitu hivyo.

Hebu tubadilike, tumfanye Mungu atuamini kwa vile vidogo anavyotupa ili baadaye atupe vikubwa na tustaajabu. Kama kweli tunahitaji bilioni moja katika maisha yetu, haina budi kumfanya Mungu atuamini hata kwa shilingi laki moja anayotupa.

Wangapi wameelewa ninachokizungumza? Share na wenzako, watag marafiki zako ambao unatamani sana kuona Mungu akiwaamini siku moja ili wafanikiwe.
 
Umenena vyema...

Ila sisi binadamu hua na imani sana juu ya Mungu pale tunapokua kwenye matatizo au kuhitaji msaada...

Tukishapata 'm.atako hulia mbwata'


Cc: mahondaw
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom