Unamkumbuka Crush wako wa utotoni? That was real and only unconditional love you will ever experience

Asikwambie mtu, yule crush wa utotoni hasa mara nyingi inakua shule ya msingi ni mapenzi ambayo yanavuruga sana hasa ukizingatia mara nyingi mtu mabae unampenda anakua hana ata habari au aanajua unampenda ila hana habari na wewe yuko busy na yeye na crush wake.
Nakumbuka nilipokua darasa wa tano ndo nilikua na crush huyo then kwao alikua kuna duka, bas kama siku sijaenda shule na sijamuina ni lazima nitoke nikamuone hata kama sikua na nia ya kununua kitu, bahati mabaya ilikua ni kijijini kwao hadi ufike unapita kwenye mapoli ila ilikua niko radhi, nakumbuka kuna siku nyingine nakwenda dukani usiku ili nimuone lakini nikitifika unakuta hayuko dukani unakuta mama yake au ndugu zake wengine, ila hata nikisia sauti yake tu huko ndani basi nakua na furaha.
sikuwahi kumueleza kua nampenda mana nilikosa lakusema nilipokua karibu yake, now ameolewa na hatuna mawasiliano ila mpaka sasa sijawai kuona ile hali tena . hakika yale yalikua true unconditional love.
Itakuwa ni INFATUATION kwasababu true unconditional love never dies or vanishes!
 
Naamini waliokuwa wakipata tabu juu yangu Ni wengi mno, manake nilikuwaga karembo bhanaaaa kapole Sana na kenye aibu nyingiiii, Kuna baadhi tukikutana wanataka watake advantage,

Mi nilimpenda mkaka flani tukiwa form 3 nae alinipenda nadhani manake alikuwa anaona sifa kweli kuwa karibu na mrembo wa shule, alikuwa anafanya poa class kunizidi nami nikaamza kukaza ili nimfikie nikampita na kumpita akaanza kunikunjia akawa anabana hata kunifundisha akaacha,, na kwa miluzi ilivyokuwa mingi nikampotezeaga, tulikutana 2015 ndipo kunitongoza nami nikamwambia nilimpendaga miaka hiyo,,, ila sio kwa utu uzimani tena, mi nikamuona km bado mdogo sana akili yangu iko mbele kuliko yake na vile nimeolewa na mwanaume mkubwa karibu nusu ya umri wangu Basi wakaka niliosoma nao nawaonaga bado wavulana
aisee sorry to ask lakini i know its personal
Ukiolewa na mtu aliyekuzidi nusu ya umri unaenjoy kweli?? hata stori/utani unakuwepo kweli?? mbona kama wadada mnaishi na baba zenu indirect way

Au tension ipo kwenye good life?
 
Nikimpenda mtu ni ngumu sana kumtoa moyoni Sofía ilikua rahisi Kwakua Nilikua bado mdogo. Sipendagi hovyo hovyo na nikipenda looh kila kitu chako na kinachokuzunguka nakipenda. Hata emoj unazokua unatumia nazipenda...nakua nikiziona nakumbuka, nyimbo, Stori, vyote vinakua vinanikumbusha

Ni swala la muda tu!

Fanya basi leo nicheki pirates
 
Sara, Bunge Primary 1998... Nakumbuka jina tu. Sara popote ulipo nakuombea maisha mema.
 
Kelvin alikuja na begi jipya na saa ya mkononi. Crush wangu akahama dawati, akaenda kukaa na Kelvin. Ilikua darasa la pili.

That was my first experience with a heart break and a gold-digger!

hadi jina la mdau unakumbuka?
 
Kashoelewa Zambia, nisingeweza kumpenda tena hata iweje. Nikisema Nakupenda basi hua imetoka ndani kabisa ya roho yangu na nikishakutoa basi siwezi kukurudisha tena. I don't love someone for the sake of Sex. Alivyonitafuta lengo lake lilikua hilo, Siwezi make love na mtu nisiyempenda hata iweje. Labda unibake..
Duh,we mwanaume mwenzetu kweli?? Hongera mkuuu,i'la hizo hisia wnaume hatukuumbwa nazo,

Sent from my CPH1909 using JamiiForums mobile app
 
Siku ya kwanza kuanza darasa la kwanza macho yangu na moyo vinaangukia kwa bint mrembo alieitwa Mimash, nilimpenda sana na yeye alinipenda sana ila tuliogopana hadi kufikia darasa la 5 alihama yeye na familia yake na kuhamia Mombassa Kenya.

Tuliendeleza mawasiliano kwa njia ya Facebook messenger na yeye ndie alienitamkia kuwa ananipenda sana na hakuna kama mimi, ila baada ya miaka miwili yeye na familia yake wakahama tena na kurud kwao India, baada ya hapo hakukuwa na mawasiliano tena hadi leo hii.
Niliumia sana na ulinifanya nipitie maumivu yenye utamu wa kila nikikufikiria, na siachi kuzirudia zile sms tulizochat 12 years back.
Dogo unacrush unachat naye messenger?? Inaonesha we bado hujamalizana na crushes wako,bado una wengine kwa foleni,subiri ifike walau 20 years ndo uje uhadithie majukumu yakishakupiga

Sent from my CPH1909 using JamiiForums mobile app
 
Matilda jamani Matilda,dah,sijawah kuwa na strong feelings Kama zile,amenitesa kuanzia form two Hadi form 4!ilikuwa hata nikimuona mapigo ya Moyo yanazima kwa muda,nashindwa kuongea chochote,tulikuwa tunishia kutazamana tu,alikuwa anakaa kiti Cha mbele darasani kila dakika anageuka nyuma tunagongana macho,tunashindwa kutamkiana,deep moyoni naumia,Sasa hivi ameolewa na mm nimeoa,Sina mawasiliano naye,ila bado nampenda, namuombea mema always!!

Sent from my CPH1909 using JamiiForums mobile app
 
Okay kwanza nianze Primary 1999-2005 nilikua napendwa na mdada mmoja wa kuitwa Lucy,na mm pia nlikua nampenda ila sijui ilikua inakuaje nikimuambia nampenda yeye anakataa,ikafka mda yeye akaanza kunambia ananipenda na mm nakataa,

Kufika la Saba mwanzoni akatokea crush mwingine alikua dada wa mshkaji wangu alikua anasoma St.Anthony Mbagala alikua form two mm la saba,Damn nlimpenda yule mdada alikua msafi ananukia mda wote,nikirudi nyumbani najisemea kesho namuambia kuwa nampenda,nikimuona kesho mdomo unakua mzito,Huyu binti ilikua nikimuona moyo wangu unakua na amani sana!yani nilimpenda kweli.

O level nilimpenda binti mmoja white hivi, nilianza kumuona stand,Nilikua nakaa Mbagala nikipita na gari Mtongani namuona ilikua form one 2006 na tulikua tunasoma shule moja,ila ile shule walikua wanatutenganisha kijinsia,(wanaume na wanawake wanasoma madarasa tofauti)
Kufika form three Mungu sio Athumani wala Mzee Mbonde tukapangwa darasa moja Damn!hisia zikazidi kuongezeka na ubaya zaidi nilikua ndo kichwa wa darasa.Yule binti ilikua ikifka jumamosi nalaani kwa nn wikiendi haiishi ili nmuone!
Hatimaye nlimfungukia kuwa nampenda ila alinikataa kata kata kata mpaka tunamaliza o levo.
 
Back
Top Bottom