Unalikumbuka igizo la Tausi?

Unalikumbuka igizo la Tausi?

h120

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2012
Posts
2,545
Reaction score
3,368
Kuna nyuzi nimesoma ya mbunge huko kenya, aliyewahi igiza kama rukia, basi nikakumbuka mchezo huu uliopendwa sana kipindi hicho.
Uhaba wa Television uliwalazimu wengi kuangalia kwa majirani, kwa sharti la kukaa chini😀.

Haya majina si ngeni kwa masikio ya waliopata nafasi ya kutizama mchezo huu.
-Mzee kasri
-Rukia
-Siti
-Baraza
-Karumanzira
-Lindi

Hichi kipande cha filamu hiyo huko youtube.
 
kuna mhusika aliitwa
kilonzo sijui kalonzo nikumbusheni vizuri

old z gold jaman nimekumbuka mbaaaliii shule ya msingi... huko duh
 
Hiv kwanin hii michezo ya kuigiza,..au hata ile ya enzi zile kina bishanga,au ile ya kina kibakuli ilikuaga mitamu sana kuliko hiz bongo muv za skuhiz,hiz bongo muv ni uchaf mtup,hakuna kitu,sjawai ona acting za ajab kama bongo muv
nyama yao. hapo unamgusa gwiji Mhogo mchungu....

ukienda mbali zaidi jangala, jongo, majuto(t.v) uledi(maigizo kwa njia ya redio) n.k
 
Dah!! Huu mchezo ulisaidia kupaka mke 2000-2001. Tulizugia tu kwenda kuangalia igizo bas mzee unatumia fursa kuweka mambo sawa. Siku maisha tit wala hakumbuki tena.
 
Huu nakumbuka wakat nipo diploma IFM kuna kadada kalikuwa kanaitwa rukia basi kalitudanganya Yule rukia kweny tausi ni pacha wake tukaamini. Dah umenikumbusha mbali sana
 
yaan siku ya mchezo unaoga mapemaa....maana hukawii kuambiwa ukaoge katikati ya mchezo
 
Yani huu mchezo ulikuwa mtamu balaaa.

Yani kile kipindi hata kwenda chooni kuoga peke Yangu nilikuwa naogopa kutokewa na zimwi la mama Lindi.

Kwa nikalazimika kuoga huku mlango nimeuwacha wazi ili likinitokea tuu nachomoka kama kombora la Kim jong un
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom