Hivi jamani hili suala ni nani alikuwa analianzisha ?maana katika miaka yangu yote 7 ya primary school sijawahi kuwashuhudia though story zilikuwa haziishi..siku nyingine tunanusurika na kuumia kisa mmoja kalianzisha kaona wanyonya damu.je ni kweli walikuwepo ama ilikuwa ni imani tu
Mi nadhani chanzo chake kilikuwa ni zile blood drives za asasi kama Red Cross. Sasa labda kutokana na ufinyu wa kampeni za kuwaelimisha watu kuhusu hilo watu wakaamua kuziba hilo ombwe kwa kuja na nadharia zao.
Mi nakumbuka siku moja wakati niko darasa la tano kuna jamaa mmoja aliropoka 'mumiani hao wanakuja' halafu huyo akatoka nduki. Basi darasani si kukanyagana kila mmoja akitaka kunusuru maisha yake kwa kukimbilia anapojua yeye.
Wengine mashapu shapu kaa sisi tulitokea dirishani. Baada ya kama dakika ishirini hivi hali ikatulia tukarudi tena darasani.
Chemwali umenikumbusha mbali.sisi kwetu kuna baba mpaka amekufa tunaamini alikuwa mnyonya damu.
Stori zalongi sana duh! tuliokuwa tunasoma shule za mbali unapita msituni unafika Shule roho uko mikononi, nilikua nakimbia kutoka nyumbani mpaka Shule
Umesoma mlimani nini?maana dah msitu ulikuwa mkubwa..lazima tukimbizwe.
yaani mi nakumbuka kuna siku tupo shule mvua inanyesha mtu akaanzisha nyonya damuuuu,tuliruka madirishani hatukujali hata mvua kama begi hujafunga madaftari yote chini...unakimbia anayekukimbiza humuoni yaani acha tu
Yani ilikuwa tabu kweli..tulikuwa kama tunakatiza kipori lazima tuwe wengi pale sheli..maana dah wale wajinga walikuwa wanatuvizia kweli..unakumbuka mpaka mama mmoja wa kihaya alianzisha daladala konda yeye ndio kama unaogopa kukatisha kipori anatubeba..ukichelewa inakula kwako.Hahahaaaa ukikatiza kipori lazima mkojo ukubane ukihofia kukutana na masalo
Hahahaaaa ukikatiza kipori lazima mkojo ukubane ukihofia kukutana na masalo