Unakumbuka breakup yako ya kwanza?

Nimejisikia kusema yalionikuta, nakumbuka katika hizo harakati ad mawazo ya kujiua yalikuja, kaka alinifata akanishauri sana ,

Naweza sema mimi nilimuacha kuogopa auibu ya kuachwa mimi ila niliumia kimya kimya
 
Nilipogundua anataka kuniacha nikamuwahi akajifanya bado ananipenda kumbe ananilia timing anifanyie suprise ya kuniacha, siku anataka kukamilisha mpango wake nilimtandika makofi hatosahau maishani

Yaani nikipiga upande huu narudia upande wa pili ndo nahesabu kofi moja.
 
Mimi alinitajia mapungufu yangu kama leo, then kesho akaniambia tuachane.

Nikakumbuka maneno ya Padri mmoja wakati anapewa upadrisho, kwamba Mungu amempigania pamoja na mapungufu yake. Nikajifanyia reflection na kuhesabu baraka zangu , nikashukuru na kumove on.
 
Hahahahahahahahaaa
 
Inauma sana,
Aliniambia ana maongezi muhimu na familia yangu akaniomba niwape taarifa na kuwasisitiza mama na ndugu zangu wawepo siku ya kikao. Nilijitahidi sana kuandaa mazingira mazuri ya kufanyia kikao bila kujua naandaa panga la kunichinjia! Niliachwa mbele ya ndugu zangu.
Sitaisahau siku ile,
Mama watoto popote ulipo Mungu akubariki na akupe umri mrefu na mafanikio wewe na mwanetu, najua ipo siku ukweli utaujua na Mungu atakurudisha mikononi mwangu hata kama itapita miaka 20.
#Evln
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mkuu umenifanya nicheke Sana usiku huu.
 
Okay naitwa Ngareroo natoka pande za hapa Ngarenaro..Aah kwa upande wangu mimi kuna manzi anaitwa Angel nilimfatilia zaidi ya miezi6 hadi ndala zangu zikaisha pia nilitengeneza kibarabara kabisa maana daily nilikua napita pale karibu na kwao,manzi alinikubalia leo alafu kesho akanibamiza et tuachane daah!!ata sijamla yaani,kipindi ananipigia simu akinambia tuachane nilikua nakula nyama lakini ile nyama niliiona kama likiazi tu haina ladha yoyote akati ilikua tamu kinyama.
 
We nae uliendekeza mapenzi ya kishamba/ ya kizungu wakati wewe ni mbongo tu! Kwanini usingepiga chini tokea tu ulipojua kuwa ndugu zake hawakupendi!
 
We jamaa umenifanya kwa sauti usiku huu, eti nyama ikawa kama likiazi.
BTW pole sana jombaa hawa viumbe ndo maana wengine wanatinduliwa na kuachwa.
 
Ulimkosea nini akakupiga chini?,mtoe na sababu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…