Unakula au unaliwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unakula au unaliwa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bikra, Jun 2, 2009.

 1. Bikra

  Bikra Senior Member

  #1
  Jun 2, 2009
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 103
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  MARA nyingi watu hupenda kupata ua kufanya mambo fulani fulani kwa kukusudia kupata kitu fulani inaweza kukugharimu pesa na muda mwingi. Bila kujua, unafika mwisho hakupata alichotarajia. Wengi wetu tunaweza kugundua kuwa hatukupata lakini kwa upeo finyu watu wengi hushindwa kujua wamepata au wamekosa. Haya yaweza kutokea kwenye biashara, masomo n.k. Hapo ndipo yanapokuja maswali unakula au unaliwa ndugu wewe?!

  Kwa upande wa lishe haya yanaweza kutokea kabisa. Hasa haya yanapatikana katika mtindo wa kununua na kula.Unatafuta fedha kwa nguvu zote, kisha unapanga matumizi yako kwa bajeti finyu. Je unachonunua kwa ajili ya kula kinakunufaisha vile ulivyokusudia au unatupa pesa zako bure?

  Kuna baadhi ya vyakula ambavyo havina virutubisho vya kutosha kulingana na bei yake. Vinywaji baridi ni mfano wa karibu kabisa. Haiyumkini kila mmoja wetu anapata soda katika mwezi mzima.Soda inauzwa sh.400 lakini kilichomo humo ni maji, sukari, rangi na kemikali zisizounufaisha mwili. Ni bora ukanywa maziwa kikombe kidogo kimoja cha shs.200 na kipande cha keki cha sh.200. Tofauti ya thamani mwilini kati ya soda na maziwa na keki, hata mtoto mdogo anaweza kukwambia. Hivyo basi badala ya kuliwa na soda wewe kula maziwa na keki inayokupatia nguvu vitamini, madini, na protini ndani yake. Kamani suala la kinywaji baridi hata maziwa pia yapo ya baridi.

  Mbali ya soda vinywaji vinavyowekwa kwenye chupa kama black currant na squshi, juice mbali mbali za kwenye mifuko pia ni hatari kwa afya na ni upotevu wa fedha bila kujua. Unaweza kukuta mgonjwa ananunuliwa juisi ya rangi nyekundu eti ili aongeze damu! Masikini kumbe humo ni rangi tu na wala si damu inayofikiriwa. Au hata maji ya zabibu kwenye chupa au ya matunda, vyote hivi ni kiini macho tu. Hakuna cha matunda ndani yake wala uhalisia wowote bali ni wizi wa kutumia akili. Unatoa wewe mwenyewe pesa mkononi na kununua hujaitwa wala kulazimishwa.

  Kama hili huliamini soma kwenye paketi au chupa za vinywaji mbalimbali kilichomo kimetengenezwa na nini. Utaambulia "Artificial flavour" ladha ya kutengeneza, rangi,sukari na dawaza kuzuia isiharibike. Hivyo wajijaza dawa mwilini mwako bila kujua ambazo zaweza kukuzuru hata wewe.Tunakushauri ujizoeshe na kuamini kuwa vyakaula halisi ndio bora zaidi kuliko vyakula vya viwandani. Chungwa moja la sh.100/- linathamani kuliko juisi au soda ya 400/=. Sasa hapo ni kula au kuliwa?

  Vinywaji hivi pia huwa na sukari nyingi ambazo ni hatari kwa afya, hasa kwa meno na wenye matatizo ya kisukari. Usiozeshe meno ya mwanao au kumjaza madawa mwanao au wewe mwenyewe bila sababu ya msingi. Tengeneza maji ya matunda wewe mwenyewe kwa njia nyepesi tu za kukamua au kupondaponda na kuchuja katika hali ya usafi. Usimpe mtoto pesa aende nazo shule akanunulie soda bali mtayarishie mwanao kinywaji toka kwenye matunda halisi.

  Vyakula vinapokuwa vimeharibika hutoa dalili mbalimbali za kuonesha kuwa havifai tena.Vyaweza kutoa harufu tofauti na ile ya awali (mbaya) kubadilika rangi n.k. Pamoja na hayo, watu hupuuza na kula vivyo hivyo vilivyo. Matokeo yake hupelekea kuumwa tumbo na kuharisha na kupoteza maji na virutubisho vingine. Gharama inarudi kwenye dawa na malipo ya kumwona daktari. Umekula au umeliwa?

  Waweza kuona chakula kina uvundo hafifu 'mouldy' , hasa kwa vilivyolala na kuwekwa kwenye joto. Vinyoa hivyo huwa na sumu ambayo hudhuru bila kuonesha haraka madhara yake. Kuwa mwangalifu kuchagua mikate au af-keki (half cake)inayokaa muda mrefu, kwani vijidudu 'fungus' wanaweza kujificha ndani yake.

  Epuka kula vyakula vilivyoachwa vya moto kwa muda mrefu kwani joto ni hali inayopendwa na vijimelea aina ya bakteria kuzaliana.

  Usinywe maji ovyo au juisi za mitaani zisizochemshwa ili mradi tu ni rahisi kwa bei lakini ni ghali kiafya. Barafu na aina zake vyote havina thamani sana mwilini kulingana na bei yake.

  Unapotoa pesa zako, jiulize unakula au unaliwa pesa zako?
   
  Last edited: Jun 3, 2009
 2. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Hii taarifa ni y amwaka gani soda ikiwa inauzwa sh. 200??????

  Bottom line, "Kula uliwe"
   
 3. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2009
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Mmmmh;

  Mkuu mbona hiyo title ya thread ina utata kwa kiswahili chetu cha kisasa? Au ndo ya kutokea.
   
 4. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  B.
  thread yako ni murua sana.
  Asante
   
 5. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #5
  Jun 2, 2009
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145

  [​IMG]
  Bikra
  Member
  Join Date: Wed May 2009
  Location: Mwilini - Kote Kote !
  Posts: 40
  Thanks: 0
  Thanked 5 Times in 4 Posts


  Yani mbele na nyuma..?
   
 6. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2009
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  [​IMG]WomenofSubstanc [​IMG]
  WomenofSubstanc has no status.
  JF Premium Member


  WOS huyo demu wa kwenye Avatar yako yuko poa ile mbaya, naweza pata contact zake?..lol

  MJ
   
 7. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #7
  Jun 2, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  halafu ukishazipata?
   
 8. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #8
  Jun 2, 2009
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Amani amani WOs, vipi unatafuta punching bag nini?., samahani kama nimekukwaza.


  MJ
   
 9. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #9
  Jun 2, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  LOL
  Usihofu ndugu yangu.WoS siyo mgomvi kiivo.Nitakutumia contacts zake ila vuta subira.
   
 10. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #10
  Jun 2, 2009
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Ulinishtua nikajua labda unamuonea donge, unatamani ningeomba zako..lol
   
 11. OsamaBinLaden

  OsamaBinLaden JF-Expert Member

  #11
  Jun 2, 2009
  Joined: May 2, 2009
  Messages: 706
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  duh...

   
 12. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #12
  Jun 2, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  unajuaje kwamba nimeng'aka kwa sababu huyo ndio WoS mwenyewe?
   
 13. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #13
  Jun 2, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,808
  Likes Received: 319
  Trophy Points: 180
  Wos:

  Title ya thread hii ilinikimbiza mpaka nilipoona umejikita humu ndani. Now, let me nisome kinachoendelea kabla ya kuanza kula.
   
 14. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #14
  Jun 2, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  za10,
  ukiniona basi ujue ni salama tu.
   
 15. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #15
  Jun 2, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,808
  Likes Received: 319
  Trophy Points: 180
  Kwi Kwi Kwi.

  Tukiona watu wenye hekima mmetangulia tunajua mambo ni salama. Maana title ya thread ilivyokaa inanikumbusha ZeUtamu.
   
Loading...