Unakikumbuka kivuko cha utete? Mrithi Daraja Mkapa aliyeacha vilio

James Hadley Chase

JF-Expert Member
Mar 25, 2020
1,565
2,642
YOYOTE aliyekuwa nje ya nchi kwa miaka mingi na alikuwa hafuatilii chochote kilichopo nchini, akarejea, ukimwambia kuwa unakwenda mkoani Lindi na Mtwara na utafika leo hii hii, anaweza kukushangaa na kuishia kucheka.

[https://res]

Ndiyo, kwa sababu atakumbuka kuwa ili kutoka mikoa hiyo ya Kusini kufika Dar, au kutoka Dar kwenda huko, ilikuwa safari ambayo kama ukiwahi sana inaweza kuwa ni siku tatu au nne.



Kama si hivyo inaweza ikawa ya wiki, wakati mwingine mwezi mzima. Unaweza kumuuliza sababu, akakwambia ukifika Rufiji ni lazima usubiri kivuko, au utumie usafiri wa hatari zaidi wa kuvuka na ngalawa au mtumbwi.

Utamshangaza zaidi ukimwambia kuwa kwa sasa kuna daraja. Nadhani atakuuliza maswali kadhaa ili kuthibitisha hicho unachokisema.

Daraja la Mkapa lilifunguliwa rasmi Agosti 2, 2003 na Rais wa awamu ya tatu wakati huo, Benjamin Mkapa ambaye ndiye aliyekuwa chachu ya kujengwa, na awali ilionekana ni kama ndoto hivi.

Daraja hilo lenye urefu wa mita 970 ambalo limeunganisha mikoa ya Dar es Salaam, Lindi na Mtwara, lililopo Ikwiriri mkoani Pwani, limekuwa ndiyo mkombozi siyo tu kwenye usafiri, lakini kumaliza mateso, visa, mikasa na vifo vya wananchi wengi waliokuwa wakipoteza maisha kwa sababu mbalimbali, lakini kikubwa ikiwa ni uhaba wa kivuko.

Rais Mkapa na viongozi wenzake wanaona hakukuwa na haja ya kununua vivuko vingi kama Feri la Kigamboni, bali kujengwa daraja.

Ndiyo daraja refu zaidi kuliko yote Tanzania mpaka sasa na daraja la tisa kwa urefu Afrika.

Kivuko kikuukuu kilichokuwepo hapo kilitesa sana watu, hususan abiria, kwani mbali na ubovu wake, lakini pia kilishindwa kumudu wingi wa abiria wanaotoka Dar kwenda Kusini na wanaotoka Kusini na kwenda Dar



Inabidi abiria wasubiri wanaovuka upande mmoja na mabasi yao, na upande mwingine na mabasi yao, kwa utaratibu maalum ili kukifanya kisizidishe abiria na mizigo.

Hii ilifanya watu waishi sehemu hiyo kwa siku moja, mbili tatu na kuendelea kutegemea abiria waliopo.

Mbaya zaidi usiombe pantoni ya MV Utete iharibike. Ni hatari zaidi ya hatari yenyewe, kwani baadhi walikuwa wakivuka na mitumbwi midogo, ambayo wakati mwingine ilikuwa inashindwa kumudu kubeba abiria na kupinduka.

Hapo ndipo vifo vingi vilikuwa vinatokea kwa abiria kuwa chakula cha mamba na kuuawa na viboko wanaotapakaa kwenye mto huo.

Nakumbuka mwishoni mwa miaka ya 1970, nikiwa mdogo, mpangaji wenzetu mmoja alipata safari ya kwenda kwao Lindi akiwa na mke na watoto wanne.

Tulishangaa aliporejea akiwa na mtoto mmoja tu. Tulipouliza kama wamebaki walikokwenda, tukaambiwa japo kwa lugha ya kuambiwa sisi watoto kuwa wamezama kwenye mto Rufiji baada ya mtumbwi waliokuwa wakivuka kupinduka.

Waliobaki ni mwenyewe baba, mke na mtoto mmoja wa kwanza. Watatu wote waliishia mto Rufiji. Kisa ni kwamba walipofika walikuta kivuko ni kibovu na haikujulikana lini. Baadhi ya abiria wenye pesa au haraka waliamua kukodi mitumbwi kwa malipo ili kuwahi, na wasiokuwa nazo walipata adha ya kukaa wakati mwingine kwa muda mrefu, njaa, mbu, na mateso kibao vikiwakabili.

Mmoja wa Wahandisi waliosimamia ujezi wa daraja la Mkapa, Mhandisi Kaitanda Michael aliwahi kubainisha na kuainisha mateso waliopitia si abiria tu, bali hata wananchi wa maeneo hayo kabla ya daraja hilo kujengwa ni pamoja na kushindwa kuvuka Mto Rufiji kwenda ng’ambo ya pili kufuata huduma kutokana na mto huo kujaa maji pamoja na mamba wengi hususan wakati wa masika.

"Mara kadhaa kivuko kilikwama kwenye matope kwa siku zisizotabirika na kusababisha msongamano mkubwa wa magari, wanafunzi walitaabika kwa kukosa chakula kwa siku kadhaa na hawakujua lini watanasuliwa na kuweza kuendelea na safari. Changamoto haikuwa hiyo pekee, akina mama wajawazito waliteseka kwa kusoka huduma za uzazi, wapo waliojifungua njiani, wengine walipoteza maisha yao na ya watoto, hata vitendo vya ukatili wa kijinsia vilikuwa vinafanyika." Alisema Mhandishi huyo na kuongeza.

"Kutokana na kukosekana kwa miundombinu imara hususan daraja na barabara, suala la usafiri na usafirishaji wa bidhaa katika mikoa hiyo ya kusini lilighubikwa na changamoto lukuki na hivyo kusababisha gharama za maisha kuwa juu ambapo bidhaa kama sukari ilipanda mara tano ya bei iliyokuwepo wakati huo. Hapakuwa na watu wenye maono ya shughuli za kiuchumi kwa sababu ya kukosa mawasiliano, hakuna masoko, Mfanyakazi wa serikali akipata uhamisho kwenda mikoa ya kusini utasikia watu wakiuliza amekosa nini, ilikiwa ni kama adhabu." Alisema.

Rufiji ni mto mkubwa wa Tanzania, chanzo chake kikiwa ni Kusini Magharibi ya nchi, kwenye maungano ya matawi la mto Kilombero na Luwegu. Matawi ya mito hiyo, huungana na kuunda mto Rufiji ambao unaanza safari yake ya unatiririsha maji na kuishia kwenye Bahari ya Hindi


ippmedia
 
umejitaidi kuelezea lakini iko kivuko kilikuwa akiitwi utete utete ni kingine kilikuwa kinavusha wilayani kama ulikiona kilikuja mara moja kusaidia tu hapo kilikuwa kinaitwa mv ndundu
 
kweli kimeondoa hadha lakini daraja limekuja kuudidimiza mji wa ikwiriri watu walitajirika sana hapo ikiwemo michezo ya kuharibu kivuko ili watu wauze biashara
 
umejitaidi kuelezea lakini iko kivuko kilikuwa akiitwi utete utete ni kingine kilikuwa kinavusha wilayani kama ulikiona kilikuja mara moja kusaidia tu hapo kilikuwa kinaitwa mv ndundu
Mndengereko kaandika.. ahsante
 
Back
Top Bottom