ladyfurahia
JF-Expert Member
- May 10, 2011
- 14,753
- 9,568
mpooooooooooooooooooo wadau
Mmmeshindaje jamani, natumai mko vyema, pole kwa wale wanaoumwa au wako hovyo
Ni mara ingine MAMA PAROKO kama kawaaaa naingia tena mjengoni TENA leo nawafunda WANAUME ambao ni WAVIVU KUPITILIZA hao kazi yao kupiga stori vijiweni hawana hata kitu ambacho wanashighulisha ili kuleta maendeleo katika familia zao.
Leo nawafunda wale watu wavivu jamani yaani hana mbele wala nyuma yeye amekaa tu anasubiria kuletewa ale, amekuwa mzembe, mvivu kupitiliza kwanini jamani mnakuwa kero kwenye mahusiano yenu kisa kuendekeza UVIVU ambao huleta umaskini kwako. Wapenzi kwa wale wenye roho ndogo msiboreke hapa ila nawaasa na kuwafunda mjirekebishe achene kuwa na tabia hiyo kwani huleta migogoro ndani ya familia zenu, na hata mtakimbiwa bure kisa mauvivu yaliyokithiri,
Wanaume wengi siku hizi wamekuwa wavivu ukiwasikia wakisema wanasema hali ngumu ndo hicho kimekuwa kigezo chao wao kutafuta wanaona taabu ,wameshindwa kupambanua na kujipa malengo na kusaka wao wanabaki kukaa tu bora siku imekwenda, Hivi kweli hakuna kitu unashindwa kufanya au kubuni kikakuingizia kipato chako? Na wengine maofisi kwao wanabaki kuagiza kma wao ndo vibosile hiyo yote ni uvivu tu, jamani wanaume na hata akina dada mjirekebishe tabia hizo.
UVIVU ULETA UMASKINI
kwani hamjui kuwa mtu mvivu hupata hata magonjwa pia maana yeye ajishughulishi anabaki kukaa na kusubiri magharibi, kaskazini vitokee vitatokeaje wakati usaki ujitumi kutafuta? ndo hapo sasa umaskini unakuingilia na unakufa kwa wakati usiowako kwani umetaka mwenyewe
Kwa leo naishia hapa jitambue na anza kuthubutu kutoka katika hali hiyo ya UVIVU kwani ni kero ndani ya mahusiano yako, na familia yako usijejuta wakikumbia kisa uvivu tu wako uliouendekeza. Wapendwa wangu hapa tunarekebishana kuwekana betri mpya katika gari zetu ili mtu ajitambue na kujirekebisha sio kijitu kije kikejeri tu ndo nshawapa somo mwenye kumeza na ameze na mwenye kuacha aachane na ladyf
Nawatakia siku njema
Wasalaam
Ladyf