Unajua kwanini ufanye factory reset process Kwenye simu ?

Unajua kwanini ufanye factory reset process Kwenye simu ?

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
1,347
Reaction score
2,755
Kuna mtu au watu Toka wanunue simu hawajawahi kufanya Factory reset hata mara Moja?

Factory reset process, ni kitendo Cha kuweza kufuta Kila kitu Kwenye simu yako kukifanya icho kifaa kiwe kipya Kama umenunua dukani.

Unajua Kuna wakati unakuta simu yako Ina tabia ambazo sio rafiki kwako Kama vile;

• Simu yako Ina tabia ya kugandaganda
• Simu yako inachukua muda mrefu kufungua program au kitu chochote
• Simu yako imekua nzito balaa
• Simu kuingiliwa na virusi
• Simu inachukua muda mrefu kuwaka au kuzima
• Nafasi ya simu yako kuwa ndogo nk

Sasa ukiona simu yako imeanza kuwa na tabia Kama izo basi jitahidi kufanya Factory reset (frp) kwani itakusaidia

• Simu kuwa na Kasi zaidi
• Simu yako kuweza kuongeza nafasi ya kuhifadhi
• Simu yako kuongeza ufanisi wa Kasi na bora kuliko mwanzo
• Simu inakua mpya ivyo utaweza kumpa mtu au kumuuzia mtu bila changamoto yoyote.
• Inakusaidia kuondoa virusi au malware wote walioko Kwenye simu nk.

Ni Muhimu kufanya Factory reset Kila baada ya miezi miwili ili kuifanya simu yako kuwa na nguvu zaidi pia kuondoa matatizo mbalimbali yanayokusumbua kupitia simu yako?

Teknolojia ni Yetu sote [emoji56]

Ebu tuachie maoni yako unatabia ya kufanya Factory reset Kwenye simu yako au lah?
FB_IMG_1648894098799.jpg
 
Kwakweli kama kuna jambo nikiwaza napata kihoro ni kufactory reset simu halafu nianze kuset accounts za apps mbalimbali upya.
 
Point Of Corrention.

Frp stands for Factory Reset Protection.
 
Ahsante kwa kunikumbusha, ila Kwa sasa sina HDD ya kukopia files zangu
 
Mzee hii factory default WAAMBIE watumiajji wa TECNO.

MIMI personal siwezi kufanya factory default coz ya files zilizoko kwa simu.
Unaponiambia nifute hizo files nitazipaataje?
 
Noana hapa kama Simu yako ni kupiga/ kutuma ujumbe ni safi tu kufanya haya ila kuna wengine Simu zao zina Mafaili muhimu kweli kweli labda wayapeleke Drive kwanza kisha ndo wafanye hivyo.
 
Simu za low end nyingi ndio zinaganda ganda mimi natumia ka huawei y9 2019 na huu ni mwaka wa nne lakina hata haigandi
 
Back
Top Bottom