Unajionaje?

Unajionaje?

Jolie Jolie

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2017
Posts
7,406
Reaction score
13,824
Huwezi kuwa zaidi ya UNAVYOJIONA.Sehemu ya kwanza ya mafanikio yako ni Ile picha ya KUHUSU WEWE uliyonayo ndani yako.

UNAJIONAJE?
Kuna watu wanajiona HAWAWEZI kwa sababu kuna watu waliwaambia hivyo ama kwa sababu walijaribu kitu na wakafeli.

UNAVYOJIONA ndivyo ambavyo UTASEMA.Ukitaka kujua mtu anajionaje angalia ANAVYOJIAMBIA.Ukiona kila saa unasema maneno "NEGATIVE" ina maana picha yako ya NDANI bado unajiona SIO wa MUHIMU.

Watu huwa wanahusiana na wewe kama vile UNAVYOJIONA.Unapoanza kujiona wewe ni mtu maalumu hata kama hakuna anayekukubali,unapoanza kujiona kuwa UNAWEZA hata kama bado NDOTO yako HAIJATIMIA,ghafla watu wataanza kukuona tofauti na kukuchukulia tofauti.

Leo usijali watu wanakuonaje;Je,wewe unajionaje?Usiseme wanavyokuona na wala USIISHI kama wanavyokuona-SEMA na ISHI kama UNAVYOJIONA.

Unajionaje?
 
Back
Top Bottom