Unaishi Kigamboni?

Chimama

Member
Jan 4, 2012
43
13
Members mnaoishi Kigamboni naomba tusaidiane/ tushauriane jinsi ya kuboresha huduma za vivuko vyetu hasa upande wa taarifa. Leo asubuhi, kivuko kidogo cha Mv Kigamboni kilikuwa kimepark na Mv Magogoni ndio ilikuwa inafanya kazi hivyo kusababisha foleni kubwa sana ya magari na msongamano wa watu. Average waiting time kwa magari ilikuwa 2hrs (labda kama ulipita kwa wajeshi then 1hr)..muda mwingi sana kupoteza kwenye foleni hasa asubuhi.

Nilikuwa naona kungekuwa na bando la matangazo where wangekuwa wanatuwekea hizo updates...kama leo vyote havifanyi kazi au vinafanya etc ili watu waamue kuzunguka au kusubiri. Pia wanaweka kutangaza kwenye radio kama traffic wafanyavyo kuhusu road congestions. Well hayo ni yangu, nawasilisha.
 
Mi ninaishi Kigamboni maeneo ya Tuamoyo...nilisikitishwa sana na watu kumuunga mkono Magufuli kwa ufidhuli aliotutendea...wanajaribu kulinganisha kivuko chetu na cha kwao Chato!!...Hata JK alisema kazi ya utabibu ni touti na
kazi nyingine...vivyo hivyo imuhimu wa kivuko cha Kigamboni ni tofauti na vingine...kama hawaamini tukubaliane kesho
tuandamane mpaka ikulu siyo mbali ni jirani yetu sana mita chache mara baada ya kuvuka... FFU watatupiga mabomu tukiwa tayari tupo ndani ya Ikulu kwa hiyo yatawawasha na akina Riz-1.
 
Wamaoishi Kigamboni ni waathirika wakubwa wa huduma mbovu za kivuko. Pia wanalipia gharama kubwa kwa huduma duni kabisa. Nadhani umefika muda sasa kuwa na umoja wa wanakigamboni ili watetee maslahi yao. Kwanza ni muhimu wawe na mwakilishi katika bodi ya undeshaji wa vivuko. Pili ni muhimu wapatiwe nafuu ya gharama kutofautisha na wengine wanaovuka kwenda kustarehe au kufanya biashara. Hapa ninamaanisha wale wanaotumia magari kwasabau ndio wanaoathirika vibaya na foleni na gharama kubwa. Lazima ijulikane kuwa hii ni huduma na sio biashara. Nadhani ilikuwa kosa sana Waziri alipopandisha bei ya kuvuka akidai kuwa wanatafuta pesa za kununua vivuko vingine sijui vya kwenda Tegeta! Siyo kazi yetu kuichangia serikali inayaotoza kodi kwa ajili ya investment katika miundombinu.
 
Waliingiza siasa kwenye huduma za jamii...kazi kweli kweli. Wanaotumia barabara wanachangia kwa kulipa kodi...kivuko - unalipa kodi na gharama za kuvuka...yaani wanaona wanatupa priviledge kweli kutuvusha na siyo haki yetu kwani K'mboni ni sehemu ya makazi ya watu...Lol..
 
Poleni sana wakazi wa K'mboni.

By the way nina kijiploti huko lakini nikifikilia usumbufu na gharama za pale pantoni najikuta kwenye dilemma ya kuhamia huko au la.
 
Njia pekee ya kuboresha kivuko ni daraja, na Kikwete kisha anza hilo, maana kawaletea kivuko kikubwa katika Afrika mashariki lakini bado tu, kukitunza hamjui.
 
Back
Top Bottom