Unaijua Ottoman Empire? Soma Hapa.

FM facts

Member
Mar 16, 2019
45
88
Himaya ya Ottoman ni Moja Kati ya Himaya Iliyokuwa Kubwa Zaidi Duniani Wakati wa Utawala Wake Huko Ulaya na Maeneo Mengine Mengi ya Afrika na Asia.
Utawala huu Uliitikisa sana Dunia Kwa Zaidi ya Miaka 600 Kati ya Mwaka 1299–1923 na Inaelezwa Utawala huu Bado Upo Katika Baadhi ya Maeneo Mpaka Leo.

Utawala huu pia Ulikuwepo Nchini Armenia na Ulikua ni Utawala wa Kinyama/Mateso/Shida Kwani Akinamama na Watoto wa Jinsia Zote Walikua Wanabakwa na Kuteswa Vikali na Kuna Mabinti Wengi Waliokua Wanafunzi, Walibakwa, Walisulubiwa Msalabani na Kuteswa Hadi Kufa Mwaka 1915.

Inaelezwa Zaidi ya Watu 1.5M Waliuwawa kwa Kubakwa na Kuchinjwa Nchini Armenia Pekee Kati ya Miaka ya 1914–1923 Wakati wa Mapinduzi ya Kuutoa Utawala Huo Dhidi ya 'Young Turk' Ambao Walishinda Vita.

Wasichana Wengi Wadogo Wa Kuanzia Miaka 8 Walikuwa Wakiuzwa Kingono, Wakiuzwa kama Watumwa, Wakibakwa Mbele ya Mama zao na Akinamama Walibakwa Mbele ya Watoto Wao, Walilazimishwa Kuolewa Huku Wengi Wakiuliwa kama Kuku na Hii yote Ilikua Chini ya Utawala wa Himaya ya Ottoman Huko Armenia.

Mwaka 1918 Kilitoka Kitabu Kikichoitwa 'Ravished Armenia' Kilichokua Kikieleza Kila Kitu Kikichotokea Nchini humo na Kitabu Hiki Kiliandikwa na Binti Mdogo 'Arshaluys Mardiganian' Aliyepona Katika Janga hilo na Kukimbilia Nchini Marekani.

Mwaka Mmoja Baadae Mwaka 1919, Ilitoka Film Nchini Marekani Iliyoitwa 'Ravished Armenia' na Story Yoote Katika Film hii Ilitoka Katika Kitabu Hiki cha Ravished Armenia.

Ottoman Empire ndio Himaya Kubwa Zaidi Katika Historia ya Dunia na Ilizitawala Nchi Nyingi sana!! Zaidi ya 20 Zikiwemo Albania, Algeria, Armenia, Bulgaria, Misri, Eritrea na Ugiriki.

Himaya Nyingine Kubwa Zaidi Katika Historia ya Dunia Zilikua ni British Empire, Mongol Empire, Roma Empire na Mughal Empire.






IMG_20190409_100328_815.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ahsante kwa maelezo yako,kipindi nipo advance nilikuwa nikisikia wale Wa History takers wakilitaja hilo jina Ottoman Empire ....kumbe ndo hiyo history yake
 
Back
Top Bottom