Nimeshawahi kutibu couple ya aina hii (discordant couple), kwa kweli zipo nyingi...na mara nyingi ni mwanamke anakuwa HIV +ve na mwanaume ni -ve. Na mara nyingi pia wanaume huwa wanabaki na wanawake zao japo wengine huwa hawataki kushiriki nao tendo la ndoa.
Kuna couple moja niliwahi kuitibu nao walikuwa wachumba mwanamke akawa +ve na mwanaume -ve, wakaoana, lakini yule mwanaume hakuwa anasikiliza ushauri wetu wa jinsi ya kujikinga wakati wa kupata mtoto, baada ya miezi 6 ya ndoa mwanaume naye akawa +ve, alilia sana, lakini wakaendelea. Na sasa wana mtoto mmoja hasiye na maambukizi.