Forgo
Member
- Apr 7, 2016
- 27
- 60
Vyama pinzani kazi yake kuu ni kuikosoa serikali pale inapokosea iweze kujisahihisha na kutimiza wajibu wake kwa wananchi.
Hapa kwetu kuna ujinga wa watawala kuwaaminisha wananchi kwamba kuikosoa serikali ni kosa, ni ugaidi na ni uasi.... Rais Magufuli ametumia hisia nyingi za uchungu na kuonyesha kuumia ili kuikamilisha imani hii kwa wananchi, na walio wengi waliamini vyama vya upinzani vinamkwamisha Rais Magufuli kutimiza wajibu wake.
Baada ya kufanikisha hilo Magufuli alianza kuikanyaga KATIBA YA NCHI wazi wazi na kupuuza kabisa utawala wa sheria. Hili lilionekana mapema na hata viongozi mbalimbali wa kisiasa walipokemea walipuuzwa na kupingwa sababu tu ni mahasimu wa Rais kisiasa, walichukua uzito wa Mtu mmoja aliyepewa dhamana kutuongoza aliyeapa kuilinda na kuitetea KATIBA anapogeuka kiapo chake mwenyewe na asitake kukemewa ni dalili za UDIKTETA.
Mtakumbuka CHADEMA walianzisha vuguvugu la kupinga udikteta, operation waliyoiita "Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (UKUTA)", Yote ilikuwa ni jitihada za wapinzani kuurejesha utawala wa sheria lakini walipingwa vikali na mtawala aliyejivika huruma za wananchi, na akaagiza vifaa vyakivita!! Bunduki, Mabomu ya Milipuko, Mabomu ya machozi, Virungu, Gadi, Groves, Washawasha zikafunguliwa na Askari polisi wakaanza mazoezi ya vitisho mitaani na kupiga risasi ovyo ovyo kweye makazi ya watu.
Hadi hapo wasioelewa maana hawakupaswa kuambiwa maana, nini tafsiri ya neno Dikteta?.
Leo kumekucha nikaenda ofisini na baada ya kupunguza majukumu ya kiofisi nikatembela mitandao ya kijamii nakutana na simanzi, mishangao, taharuki na hasira za watanzania wakimzonga Rais Magufuli kwa kauli moja wanasema "Tusubiri Bunge lije lituokoe".... "Hivi kumbe Magufuli Dikteta?".... "Sikutegemea huyu baba!"....
Hahahaha watanzania bwana!!!, hakuna watu wanafiki kama sisi watanzania.... Labda sababu tulio wengi wajinga na kwa ujinga wetu tutajiona wenye laana ya milele....
#Hapa_Hamkuwepo? Mbona hii ilipita kimya kimya?
"Kwenye kampeni zangu ni wapi mlinisikia ninataja neno katiba? Sijawai taja hata maramoja!!, watanzania tuachane na haya mambo ya KATIBA MPYA, Mniache ninyooshe nchi". - JPM
[HASHTAG]#Leo[/HASHTAG] mnalalama na kushangaa hapa?
"Mimi ndiye Rais wa nchi hii, mtake msitake, hata mgaregare, hakuna wakunipangia mimi" - John Joseph Pombe Magufuli
Tulia tuicheze ngoma ya kwetu wenyewe, ukikanyagwa kaa kimya!
Forgo #JF