Wasanii wa kwetu hapa ni wa ajabu sana yaani waliwekwa ndani wakina TID na wenginao ila hapakuwa na hata mmoja aliekuwa akipost picha zao na kuwapa maneno ya faraja ila sasa kawekwa Vanessa Mdee sasa kila kona kwenye social media wanapost picha zake na kumpa maneno ya faraja.
Hapo ndio unajua kuwa watu wana makundi yao na hakuna umoja ni unafki tu na uzandiki wa hali ya juu.
Huwezi kuwa rafiki wa kila mtu. Hata waliopo kazini, sio kila mfanyakazi ni rafiki yako wa karibu. Hivyo, kutokufanya chochote kwa mtu asiyekaribu nawe sioni kwanini uwe unafiki
Hao wasanii ni kama jirani zako tu hapo mtaani ukiishi nao poa lazima watakua nawe kwenye kila jambo ila kama picha haziendi basi siku nyumba yako ikiwaka moto watakuja na petroli wakisema maji.