sheiza
JF-Expert Member
- Sep 29, 2010
- 7,634
- 11,696
Ni kweli kabisa wanasiasa akili zao wote zinafanana. Mwanasiasa siku zote yupo kwa ajili ya kutafuta maslahi yake na familia yake kwa kivuli cha kuwapigania wananchi ila muda huwa unawasuta.
Katika mahojiano juu ya kifo cha Membe kwa wanasiasa, kuanzia Nape, Mbowe hadi Zitto. Kila aliyehojiwa alionyeshwa kuhuzunishwa kwa sababu Membe alimgusa moja kwa moja yeye binafsi na sio taifa. Hata Lema ameandika hivyo hivyo
Kwa akili hizi za wanasiasa hawa nimegundua ilikuwa ngumu mno kuendana na falsafa ya Magufuli ya kutaka kuleta ustawi wa hali za wananchi badala ya hali za wanasiasa kama kina Mbowe.
Ndio maana kuna tofauti kubwa ya namna wanavyozungumzia viongozi waliokuwa upande wao na wale ambao hawakuwa upande wao kimaslahi.
Vivyo hivyo hata maoni yao juu ya hao viongozi kwa kiasi kikubwa yanatofautiana na wananchi wa kawaida.