Unafiki wa wanaChadema kwa Chadema

Unafiki wa wanaChadema kwa Chadema

Kitu nilichojifunza ni inabidi Mbowe ajifunze kubadilika kwa njia ngumu kidogo ndio atasaidia hata hawa washabiki kuelewa siasa zinapaswa kwenda vipi. Huwezi kupinga kila kitu ukaonekana mzima. Inafikia hatua watu wanashabikia serikali ikishtakiwa na mabeberu! Hawajadili constructively bali kejeli na kila dalili hata za kushirikiana na hao wanaotushtaki! Huu uzandiki haukubaliki!!
Wamepinga nini embu toa mfano maana shida yenu mkikosolewa tu mnasema wamepinga!! Wamepinga nni so far
 
Ninachoona ni baadhi ya watu kuyaunga mkono hayo maandamano indirectly. Kuunga mkono na kuandamana ni vitu viwili tofauti.

Ninachoshangaa ni kutegemea watu waandamane ambao hata kukiri kijasiri kuwa wataandamana wanaogopa.

Ila msijekuwaingiza chaka watu hasa wanachama wasiojielewa wakafanywa mfano nyie mkiwa makwenu mkifatilia kwenye tv.

Siasa za kijasiriamali zimetuchosha. Watanzania watapofikia wakichoshwa na serikali wala hawataambiwa cha kufanya na yeyote. Watachukua hatua ngumu wenyewe.
Maandamano ni haki ya kila raia muhim mkitoa kibali basi polisi wawepo kulinda usalama basiii alafu watu wasipokuja ndio mlalamike sio mnakejeli kwamba hakuna atakayeandamana ilihali muda huo huo mnasema OLE WAKE !!!

Iko wazi kabisa mkiruhusu maandamano watu watajaa hasa miji mikubwa ila mkiyazuia mkajaza mapolisi watajitokeza wachache hivyo amueni moja mkejeli ili wawaprove wrong au mzuie tujue hayapo sio mnakejeli ilihali mmekataza maandamano ya amani!! Inashangaza sana
 
Eti unasema Chadema wana matusi,chuki na kebehi kwa serikali?Kwani hiyo serikali unayoizungumzia lin iliwapenda Chadema zaidi ya kuwabeza na kuwaita wanafiki tu,kuwabambikia kesi!!!!hulion hilo?By the way unasema Chadema ingeunga mkono serikali kwenye juhudi za kutetea rasilimali ?Ivi ulishawahi kujiuliza agenda ya ufisadi waliianzisha Chadema,Serikali au JPM alishawahi kuipongeza Chadema kuibua ufisad na kuipigia kelele na vivo hivyo kwenye madini Chadema walipiga kelele juu ya sheria mbovu!baada ya kupongezwa leo wanaitwa wakala wa mabepari!???Alafu ndo umuunge mkono JPM kwa lip?wakati vibaraka kama nyiny mlkua mnawaita Chadema ni wazushi awamu ya 4 eti leo mnajifanya watetez!!!Bro tafuta kazi nyingine kutetea unafiki na wanafiki sio kazi ndogo!

Agenda ya ufisadi waliianzisha chadema, walikuwa original nayo!! what happened?/ be genuine?? who is lowassa in chadema?? halafu unaniita mnafiki??
 
Yale matusi, chuki za wazi, vijembe , hasira na kebehi za wanachadema kwa serikali hii, au hata mwenzao ambaye ana mawazo ya tofauti umezidi kuiacha uchi chadema

Wengine tumejaribu kila njia kuiongozea damu chadema kuipa uhai na hata kuwasha mashine za kupumulia, tena kwa upendo tu ila tumeambulia matusi na kebehi

Matusi ya wanachadema kwenye social media hauwezi kuamini kabisa kuwa hawa watu ndio wanakula pasaka ya leo ili hali Mbowe, mbowe huyu huyu yuko ndani!!

Haikuwa rahisi kudhania sugu atawekwa ndani(bado yumo ndani)

Mbowe ukitoka, badilisheni style ya siasa zenu. watanzania wanachuki mdomoni na wana upendo moyoni!! pale wanapokuwa wana upendo mdomoni na wanachuki moyoni..ni WANAFIKI..kweli mbowe wewe wa kulala ndani huku salary slip, nguruvi, mag 3, na wote chadema kindakindaki wanakula pasaka kwa raha zote!!..bila hata drama za kisiasa kuonyesha mko ndani?

Mbowe, Magufuli hachukiwi!!..Magufuli anatakiwa kuwa supported kwa nguvu zote ili CDM ipate support ya wananchi....unatakiwa kujipambanua na kwenda hatua ya mbali ambayo utawaambia wananchi kile ambacho unajua magufuli hataweza

kwa mfano "kusema CDM inaunga mkono jitihada zote za rais kwenye kudhibiti madini" ILA sisi chadema tukipata fursa tutahakikisha wale waliolifikisha taifa hapa tunawatafuta na kuwafilisi" unaposema hivi CDM inakuwa connected na jamii directly unapoweka condition ambayo unajua CCM hawataweza unakuwa MPINZANI!!

Hii kanuni rahisi ya busara na kanuni ya dhahabu mmeshindwa kabisa kui capture..mmesahau kucheza SIASA mnaeneza chuki, hasira, vijiba vya roho


Faida gani mnapata sasa? hao wazungu hawawezi kuwasaidia

Nilijua mbowe ukikamatwa Tanzania itatikisika!!'.haitakalika...haitatawalika....nilijua mbowe ukikamatwa mjini kutakuwa hakupitiki!..wanachadema wameonekana mashoga si mashoga, wanawake si wanawake, wamekuwa hayawani, hawaoni soni wala aibu....wanachadema wamekuwa kama kikundi cha taarabu, no siasa ni KUSEMA tu, kuandika tu...kutukana tu

Haya mbowe yuko ndani wako kimya tu..HIVI MBOWE UKITOKA NDANI unakuwa kiongozi wa nani?? kwa nini hamtaki kuamini kuwa siasa bora ni kuitambua jamii husika inataka nini, ina tabia gani? ..mtanzania anaweza kukutukana na kukudharau hata unapodai haki yake!!.ebo!..hallow ..wake up!!..Tanzania siyo nchi ya vurugu, get this fact

wanachadema wanatukana hata unapowapa ushauri mwema!..wako frustrated mpaka hata wakiwa wanakojoa hawajiamini!

Chuki inaleta kansa, mnajiumiza, mnateseka bure!! get life..

ebu anzeni siasa, kwa sasa HAMFANYI SIASA, mnaua chama

wale wa kutukana ambao hamjaenda kumwona mbowe ndani, na hamjaweza kufanya lolote....njooni mtukane na hapa
Ebwana hii inaitwa uppercut chembe kidevu...lazima ukae
 
Waberoya brother ndio reasoning imeshuka kiasi hiki??

Kwani wewe ulitaka mbowe akiwekwa ndani CHADEMA wafanye maandamano ili mseme wanaingilia uhuru wa mahakama???

Kama CHADEMA as u claim haina mass support unatumia vigezo gani?? Kwanini hamruhusu maandamano ya amani na mikutano ya kisiasa ili tujue mbivu na mbichi sio mnakuja na kejeli kuwa CHADEMA haikubaliki kwa wananchi ilihali hamruhusu wafanye mikutano

Walivyopokwa haki ya mawakala wao kwenye uchaguzi waliandamana kwa uwingi tu mkaishia kuwapiga risasi na mkatupa lawama nyingi kwa mbowe hadi mkawafungulia kesi alafu leo hii unakejeli kwamba hakuna anayeandamana ilihali unajua wakiitisha maandamano mtayazuia na zaidi mtawaua watu

Kuhusu kuunga mkono umetoa hoja mfu kabisa hayo unayosema yameshaongelewa sana kwenye bajeti kivuli na ripoti za wizara kivuli zinazosomwa bungeni wakati wa bunge la bajeti yaani wanachukua hoja za serikali kuu na kuzitengenezea hoja mbadala sasa kivipi unajifanya ndio unashauri CHADEMA wawe na sera mbadala ilihali zipo zinasomwa kwenye hotuba za kambi rasmi ya upinzani kwa wizara mbalimbali???

Shida ya wana JF wengi tunapenda kuandika kabla ya utafiti nashangaa waberoya wa enzi zile ulikuwa na nondo kweli zimeshiba siku hizi umekuwa wale wale kama polepole unaongea kwa kukariri sio kitafiti

Nikuulize nipe kitu kimoja tu ambacho upinzani wamepinga.... Nitajie kimoja tu hapa
Mkuu, bila shaka kuna watu inabidi mjibizane kwa vile mnafahamiana muda mrefu hapa. Lakini watu wengine ukisoma maandishi yao unajua kuwa wanafahamu ukweli LAKINI kwa MAKUSUDI kabisa, wameamua kuweka pembeni fahamu na utimilifu (integrity) wote kwa maslahi binafsi (sijui ya aina gani?). Kuna niliodhani ni watu objective wenye mawazo ya maana lakini sasa hivi wanaandika kama watu wa vijiweni. Mantiki yote imewekwa pembeni umebakia ushabiki wa "kiswahili" tu. Eti, CHADEMA inapinga kila kitu; Magufuli anatakiwa kuwa supported kwa nguvu zote kwa juhudi zake za kudhibiti madini. Seriously?

Halafu, mtu anajua kabisa kuwa utawala huu unaendeshwa kiimla kwa kauli za rais (decrees): katiba, sheria, taratibu rasmi vimewekwa pembeni. Vyombo rasmi vya dola (polisi) kazi yake kuu ni kudhibiti upinzani wa kisiasa na hapo vinatumia risasi hadharani kukabiliana na waandamanaji huku visivyo rasmi (wasiojulikana) vikiendeleza utekaji na mauaji ya wapinzani (na waandishi wa habari jasiri). Halafu mtu mwenye akili zake timamu anachekelea sarcastically kuwa "upinzani wa sasa ni dhaifu sana"; Mbowe yuko ndani hawajafanya chochote?

You have to have some lingering empathy to such guys to even respond to such trash. My apologies.
 
aisee!! Mbowe yuko ndani kweli? mungu wa chadema!!
 
ni kweli mbowe yuko ndani

ni kweli chadema iko kimya

ni kweli hamna la kufanya

hata ubunifu tu wa mitandaoni kumkumbuka mbowe siku ya pasaka hakuna!!

no drama, kuko kimyaaaaa..........

sio fair nyie wanachadema, sio
Sikiliza nikwambie mkuu..ni sacrifice kubwa sana kuwa opposition bongo hasa kwa kipindi hiki

Kwa sababu ya nature ya watu wetu

Mimi ningewashauri kina mbowe waachane tu na siasa...wanaweza kuishi maisha mazuri tu na familia zao.....watanzania wakichoka wataamuwa wenyewe wafanyeje.
 
Halafu watu wanaweza kusema wataandamana tarehe 26.. hivi kama kuna kuandamana si ingekuwa wakati viongozi wakuu wa upinzani wako ndani? watu walitaka kula Pasaka kwanza.. Upinzani sasa hivi ni dhaifu sana...
Ndio ni dhaifu sana..as if ni jukumu binafsi la mbowe kuwa opposition..baadhi ya watanzania ni wapumbavu sana.

Mbowe anaweza kuishi maisha yake akaachana kabisa na chadema...sasa wewe utanufaika nini?
 
Waberoya kwa kweli chama kikuu cha upinzani tz kinaitaji maombi sijui ni nini kimewakuta na cha kushangaza ni kwamba wamesahau kuwa walikuwa wanapata support kubwa kutoka kwa wa tz wenye hali ya chini na sasa wanapata support kutoka kwa baadhi ya watu wenye hali ya kati na sana hali ya juu hii inatokana na kuwa magufuri now ansuppot kutoka kwa watu wa hali ya chini kutokana na siasa zake hapo ndio napokubaliana na wewe kuwa chama kikuu cha upinzani kinaitaji kulijui hili na kubadili aina ya siasa zake maana watu wa hali ya chini ndio wapiga kula kuendelea kumchafua na kumchukia magufuri ni kuendelea kupoteza uungwaji mkono kutoka katika kada ambayo ndio tegemeo kipindi cha uchaguzi
Kwa hio unashauri ili upinzani wapate support ya wapiga kura wamuunge mkono magufuli?
 
Ndio yupo ndani.Hata wewe unaweza kuwa ndani vilevile..Mandela alikaa ndani 30 years..sembuse mbowe.....cha ajabu ni nini hapo??

cha ajabu ni wewe ambaye haujampelekea hata ukoko wa pilau..kisha unajiita kamanda
 
Waberoya kwa kweli chama kikuu cha upinzani tz kinaitaji maombi sijui ni nini kimewakuta na cha kushangaza ni kwamba wamesahau kuwa walikuwa wanapata support kubwa kutoka kwa wa tz wenye hali ya chini na sasa wanapata support kutoka kwa baadhi ya watu wenye hali ya kati na sana hali ya juu hii inatokana na kuwa magufuri now ansuppot kutoka kwa watu wa hali ya chini kutokana na siasa zake hapo ndio napokubaliana na wewe kuwa chama kikuu cha upinzani kinaitaji kulijui hili na kubadili aina ya siasa zake maana watu wa hali ya chini ndio wapiga kula kuendelea kumchafua na kumchukia magufuri ni kuendelea kupoteza uungwaji mkono kutoka katika kada ambayo ndio tegemeo kipindi cha uchaguzi

hii ndio siasa

uko sahihi sana

siasa ni kutaka kura pia
 
Mkuu wakisema wanaitwa wachochezi, wanapotezwa, kutiwa ndani hata kopoteza uhai, kaa chini tafakari wakiti kupuka siasa imepigwa marufuku mpaka 2020 ila kwa ccm sasaa ulitaka ukawa wafanye nini? Kuandamana au kufungwa jela?
 
Acha uongo wewe!!! nani aliyekudanganya Tanzania ni non violent country!? Unaishi chini ya jiwe!? Lissu alipigwa risasi 38 akiwa Rwanda? Ben Saanane alipotea akiwa Burundi? Roma na wenziw waliotekwa na kuteswa walikuwa Uganda? Miili inayookotwa ufukweni mwa bahari iliokotwa Somalia na kuja kutupwa Coco beach? Azori Gwanda mwandishi wa Mwananchi aliyepotea kwa zaidi ya miezi minne sasa alipotea akiwa Congo!?

Tatizo lako unafiki unakusumbua sana ndiyo maana unaandika uongo. Ungeacha unafiki ungeona hali halisi ya nchi yetu kuhusu chuki za kutisha, udhalimu, dhuluma na hata mauaji ambayo chanzo chake kikuu ni huyo dhalimu.

Huu uongo wako beba upelele Lumumba kule utawapata wengi watakao kuona wewe ni genius kwa huu uongo wako lakini si humu. Huwezi kudai huyo dhalimu ni kiongozi mzuri huku akidharau katiba ya nchi, akidharau sheria mbali mbali za nchi, akidharau Bunge na mahakama. Akidharau haki za raia na vyombo vya habari nchini.

Sasa hivi imefikia hadi kujichotea trillions za pesa za walipa kodi bila idhini ya Bunge. Hii inasababisha wizi na ufisadi mkubwa sana wa pesa za walipa kodi. Bunge liliidhinisha bilioni 2 tu katika mwaka wa fedha wa 2017/2018 lakini ambazo zimeshatumika ni zaidi ya bilioni 350 HUU NI WIZI!!!

Nchi haiendeshwi hivi nchi ina taratibu zake za miaka nenda miaka rudi ambazo ni lazima zifuatwe badala ya mtu mmoja kutaka kutuaminisha kwamba kwa sababu yeye ni "mzalendo" basi aachiwe afanye vile atakavyo hata kuambiwa chochote kile, kukosolewa au kushauriwa hataki.

Tia akili kichwani acha kuidumaza ili kuganga njaa na kutafuta teuzi.




Sasa chadema yenyewe haitii sheria!! Kama mngekuwa mnatii sheria mngeliaandamana bila kibari!!???RIP akwilina
 
Acha
Mkuu wakisema wanaitwa wachochezi, wanapotezwa, kutiwa ndani hata kopoteza uhai, kaa chini tafakari wakiti kupuka siasa imepigwa marufuku mpaka 2020 ila kwa ccm sasaa ulitaka ukawa wafanye nini? Kuandamana au kufungwa jela?[/QUOTE

Acha kuwadanganya wananchi!! Mikutano ya ndani mbona inaruhusiwa? Lakini Fanya mkutano kwa kuxhunga mdomo wako usichafue Mkuu Wa nchi!!
 
ni kweli mbowe yuko ndani

ni kweli chadema iko kimya

ni kweli hamna la kufanya

hata ubunifu tu wa mitandaoni kumkumbuka mbowe siku ya pasaka hakuna!!

no drama, kuko kimyaaaaa..........

sio fair nyie wanachadema, sio
Walikuwa wanamsumbiri yule kahaba Wa marekani awamrishe maana wanatumia akili yake kufikiri!!hahahahahaha
 
cha ajabu ni wewe ambaye haujampelekea hata ukoko wa pilau..kisha unajiita kamanda
Aliyekwambia mimi ni mwanachama wa chadema ni nani?? Mbona mna akili mbinuko hivi...

Kwa hio unataka kuniambia hata mandela watu walikuwa wanajazana jela kumpelekea ukoko wa pilau?

Siku hizi watu sijui akili mmepeleka wapi
 
Uzi wa kuokoa chama na ni tested facts ila utamaduni wa chama Kama kawaida walishaanza mitusi .utamaduni mbovu chini ya jua
Chadema iko mbiyoni kufa inapiga mateke kama mfu akatikaye roho huku mapepo hakimsubiri!! Ukiwashari matusi mengi!! Yani !!! Lakini tabia ya muongo inajulina daima!!ukinyonga utawamaliza tu pole pole!! Ukiona mpaka katibu ya mbunge Lema anakimbia maana yake ameona kuna siafu
 
Back
Top Bottom