Buchanan
JF-Expert Member
- May 19, 2009
- 13,192
- 1,976
- Thread starter
- #41
Hivi kuna serikali ya Tanganyika? Ardhi ya watanganyika inasimamiwa na serikali gani?
Kuhusu Warioba, kama ana matatizo yote hayo uliyosema basi hata huyo aliyempa uenyekiti wa tume atakuwa boya kabisa. Unataka kusema mwenyekiti wa chama chenu ni mbumbumbu kabisa kiasi hicho? Au ndio kama vile aliitwa dhaifu? maana inaelekea hajui hata wafujaji wa uchumi kama Warioba kwa mtazamo wako.
Na nikirejea 'signature' yako, hivi hicho chama chenu na Nyerere wake, kama alikuwa na malengo ya muungano halisi, alishindwaje kuweka serikali moja? Upuuzi kabisa.
Mkuu,
Mungu alimuumba Shetani lakini baadaye akawa na kiburi akalewa sifa, akawa adui mkubwa sana wa Mungu! Mungu ataitwa Mungu na sifa zake zilizo njema zitaendelea kutukuka! Warioba naye aliaminiwa sana kwamba atatupa Katiba bora lakini akalewa sifa, akawa sio tu anafanya yale ayatakayo bali akawa hata analazimisha yale anayoyaamini yakubalike, sasa hii nchi imekuwa ya kwake au vipi? Kikwete ataendelea kuenziwa wakati Warioba Historia itaendelea kumhukumu!
Kuhusu "signature" sishangai wewe kumkejeli mwasisi wa taifa hili maana tuliona UKAWA wakiporomosha matusi dhidi yake! Endelezeni basi matusi yenu na chuki mlizo nazo mioyoni mwenu, uzuri wananchi wamefunguka macho wanawaelewa! Kama huamini basi subirini kwenye kura za maoni muone jinsi wananchi wakavyowaumbua!