Gagurito
JF-Expert Member
- Feb 11, 2011
- 5,600
- 804
Nchi hii haiwezi kuendelea kama wananchi wa nchi hii hawatafanyakazi na kulipa kodi.
Tupo takribani 44,929,002 ila wanaokadiliwa kulipa kodi (watu pamoja na mashirika) ni 2.7 m.
Cha ajabu wabunge wetu licha ya kupata mishahara minono (takribani 12m kwa mwezi) hawalipi kodi. Mwalimu wa sekondari mwenye degree ambaye mshahara wake ni laki 532,000 anakatwa shilingi 56,400 (kodi kwa mwezi) anachangia shilingi laki 672,000 kama kodi kwa maendeleo ya taifa hili kwa mwaka licha ya mishahara yao kuwa midogo.
Swali la kujiuliza hapa ni juu ya uhalali wa wabunge wetu kuishauri na kuhoji mambo mbali mbali serikali juu ya mapato na matumizi (ya kodi) wakati wao hawalipi kodi.
Je, huu sio unafiki wa Wabunge wetu kwa wananchi na taifa?

Kweli watanzania wengi ni wavivu sana wa kusoma na kufanya utafiti lakini ni wepesi wa kulalamika na kulaumu. Nani alikwambia kuwa wabunge hawalipi kodi? Nani alikwambia kuwa mawaziri au rais halipi kodi? Hawa wote wanalipa kodi kutoka kwenye mishahara yao.
Kwa faida tu kila mtumishi wa umma bila kujali wadhifa hulipa PAYEE kama ifuatavyo:
Kiwango cha Kodi
Mapato ya jumla yasiyozidi Shilingi 2,040,000/=
Asilimia sifuri (0%)
Mapato ya jumla yanayozidi Shilingi 2,040,000 lakini hayazidi shilingi 4,320,000/=
13% ya kiasi kinachozidi Shilingi 2,040,000/=
Mapato ya jumla yanayozidi Shilingi 4,320,000/= lakini hayazidi shilingi 6,480,000/=
Shilingi 296,400/= + 20% ya kiasi kinachozidi Shilingi 4,320,000/=
Mapato ya jumla yanayozidi Shilingi 6,480,000/= lakini hayazidi shilingi 8,640,000/=
Shilingi 728,400/= + 25% ya kiasi kinachozidi Shilingi 6,480,000/=
Mapato ya jumla yanayozidi Shilingi 8,640,000/=
Shilingi 1,268,400/= + 30% ya kiasi kinachozidi Shilingi 8,640,000/=