Unafiki wa Mwafrika, wa Mtanzania ni wa kiwango cha lami!

Nichumu Nibebike

JF-Expert Member
Aug 28, 2016
8,696
2,000
Watanzania ni watu wenye kasumba ya ajabu sana. Wengi wao ni watu wanaopenda kutendewa kitu wasichopenda kumtendea mwingine! Nitatoa mifano miwili nikijaribu kubainisha unafiki wa watanzania walio wengi!
Aicha Radhia alipoteuliwa kuwa Miss Tanzania, swala hili lilieta mushkeli mkubwa sana na manung'uniko nchini, kisa tu Aicha alikuwa ni mtanzania mwenye asili ya India. Watanzania walihakikishwa wanambagua Aicha na kutompa ushirikiano wa kutosha katika kipindi chake cha umalikia wa taji la miss Tanzania... Hata wakati anashinda kuna watu walimwaga machozi uwanjani wasikubaliane na the fact kuwa 'mhindi' amekuwa miss Tanzania.
Watanzania hao hao waliombagua Aicha Radhia, ndio wanaolia kuwa wanabaguliwa kwenye mataifa ya watu kam Marekani, Ulaya na India, huku wao pia wakiwa wanafanya hayo hayo.
Huu ni unafiki wa hali ya juu sana!

Hivi karibuni limeibuka sakata la makinikia!
Watanzania asilimia kubwa wakililia mgawanyo sawa wa mapato ya madini!
Wananchi hao hao wakitozwa hata elfu moja ya gunia la mkaa, wanakuwa wakali kulipia na hawataki hata kuchangia pato la serikali kwenye gunia lenye thamani ya sh elfu thelasini na tano, lakini eti wao wanataka wale wanaochimba madini wachangie!
Hivi sisi wananachi, kwa nini hatutaki kuwafanyia wenzetu kile tusichopenda kufanyiwa?
Watanzania wangeonesha nia ya dhati kuwa kweli wanataka muwekezaji naye alipishwe zaidi ikiwa wao hawataki kulipia zaidi?
Huu ni unafiki wa kiwango cha lami!
 
Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
12,788
2,000
Watanzania ni watu wenye kasumba ya ajabu sana. Wengi wao ni watu wanaopenda kutendewa kitu wasichopenda kumtendea mwingine! Nitatoa mifano miwili nikijaribu kubainisha unafiki wa watanzania walio wengi!
Aicha Radhia alipoteuliwa kuwa Miss Tanzania, swala hili lilieta mushkeli mkubwa sana na manung'uniko nchini, kisa tu Aicha alikuwa ni mtanzania mwenye asili ya India. Watanzania walihakikishwa wanambagua Aicha na kutompa ushirikiano wa kutosha katika kipindi chake cha umalikia wa taji la miss Tanzania... Hata wakati anashinda kuna watu walimwaga machozi uwanjani wasikubaliane na the fact kuwa 'mhindi' amekuwa miss Tanzania.
Watanzania hao hao waliombagua Aicha Radhia, ndio wanaolia kuwa wanabaguliwa kwenye mataifa ya watu kam Marekani, Ulaya na India, huku wao pia wakiwa wanafanya hayo hayo.
Huu ni unafiki wa hali ya juu sana!
Utakuwa gabachori wewe siyo bure
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom