Unafiki wa baadhi ya Watanzania wenzetu

Emmanuel Robinson

JF-Expert Member
May 29, 2013
1,503
1,139
Mimi nimeshangazwa sana na unafiki wa baadhi ya watanzania wenzetu. Kila siku wanapiga kelele kuhusu corona na kumlaumu mheshimiwa Rais kwamba hachukui hatua ni hatua zipi wanazozitaka? Unafiki wako sasa mtu anakaa baa anakunywa pombe yake hana hata barakoa akimaliza anakuja jamii forum kupiga kelele.

Mwingine kutwa anazurura tu mtaani wala hana barakoa akitosheka anakuja JamiiForums kupiga kelele. Sasa mimi najiuliza kwa nini huyu mtu asikae nyumbani ajikinge na familia yake? Serikali haijawahi kutumia mgambo kuwakusanya watu majumbani kuwaleta mjini au kutumia mgambo kuzuia watu kuvaa barakoa!

Unamfiki mkubwa kabisa ni ule wa kulazimisha mheshimiwa Rais aseme eti ndiyo mtu avae barakoa. Ikiwa unaona hatari kwa nini usivae barakoa kjuikinga badala yake unataka hadi Rais atoe kauli?. Yaani ukiingia humu mtandaoni utadhani kwamba Watanzania sasa wameisha ! Kwanini presha inakuwa kubwa zaidi?

Shida ninayoiona ni watu kutaka kutumia fursa ya corona ili kutimiza ajenda zao za siri. Angalia kina Peter Msigwa wanachoandika angalia waliobomolewa nyumba Kimara kina Kigogo anagalia waliosahauliwa na system kina Kagasheki wanachoandika Twitter. Hii yote inaonyesha hasira waliyonayo dhidi ya serikali ya awamu ya tano.

Angalia wanavyomtukana waziri wa afya tatizo lake ni nini. Teknolojia tuliyonayo njia ilizotumia serikali ndizo sahihi. Mtu anakuja na wazo shule zifungwe je kuna mwanafunzi yoyote amefariki huko mtaani kwako? Mwalimu je? Hiyo siyo sample ya kutosha kukuonyesha hali halisi?

Ni vizuri kama Watanzania tukaacha tofauti zetu na kuangalia maslahi mapana ya taifa letu. Badala ya kupiga kelele anza kuchukua hatua wewe binafsi na familia yako.
 
Jitu lipo kila siku lina zurura kariakoo kutafuta ugali wa wanawe kiasi kwamba siku lisipoenda linakufa njaa yeye na mitoto yake, lakini utakuta lipo hapa JF linalaumu eti rais hachukui hatua.

Ningekuwa mimi Magufuli ningesambaza jeshi mtaani hasa nijini na kupiga marufuku ya watu kutoka nje kwa wiki 2 tu, yani wiki 2 tu wala siyo tatu wala nne, nakwambia hata haya machadema mbona akili zitarudi tu!

Hata hawa maaskofu wanaopiga kelele za corona huku wakiendelea kuruhusu misa, ningekuwa Magufuli piga ban ibada zote kwa miezi miwili tu uone kama akili hazijawakaa sawa. Sasa hivi wanaoiga kelele si makapu ya sadaka bado kila jumapili yana jaa!
 
Mtoa mada ni sampuli ya wale wanafiki anaowasema. Kama Rais anahamashisha watu wasivae barakoa wewe unaona ni sawa? eti watu wavae tu kwani kazi na majukumu ya Rais dhidi ya raia wake uvijui?

Yaani Rais kusema kua barakoa zina Corona na still maduka yanaendelea kuyauza unadhani anatimiza majukumu yake.

Acha unafiki mtoa mada.
 
Ungepoteza huu muda kufanya kazi za shamba kuliko kuandika upuuzi huu ambao hata Polepole akiuona anakufukuza kazi.
 
Jitu lipo kila siku lina zurura kariakoo kutafuta ugali wa wanawe kiasi kwamba siku lisipoenda linakufa njaa yeye na mitoto yake, lakini utakuta lipo hapa JF linalaumu eti rais hachukui hatua.

Ningekuwa mimi Magufuli ningesambaza jeshi mtaani hasa nijini na kupiga marufuku ya watu kutoka nje kwa wiki 2 tu, yani wiki 2 tu wala siyo tatu wala nne, nakwambia hata haya machadema mbona akili zitarudi tu!

Hata hawa maaskofu wanaopiga kelele za corona huku wakiendelea kuruhusu misa, ningekuwa Magufuli piga ban ibada zote kwa miezi miwili tu uone kama akili hazijawakaa sawa. Sasa hivi wanaoiga kelele si makapu ya sadaka bado kila jumapili yana jaa!
Unawaita wenzio jitu,basi wewe ni LIJITU.
 
Asiseme Ugonjwa haupo,serikali Ikili Ugonjwa upo,na kuvaa barakoa,kunawa na maji tiririka,na kuepuka mikusanyiko,ni hatua zilizothibitishwa na wataalamu wa afya kuzuia maambukizi ya corona,
Watanzania ni Kama binadamu wengine,hatuna upekee wa kuzuia maambukizi.
Raisi asiseme watu wapige dua tu kuishinda corona,na hizi porojo kwamba mwaka jana tuliishinda korona aziache,mwaka jana serikali iliacha kutoa takwimu,pili,shule zilifungwa kwa muda,watu walivaa mask,na baada ya kuacha,kukawa na incubation period ya kurudi,na sasa hv,kimestawi,na kinaua
 
Jitu lipo kila siku lina zurura kariakoo kutafuta ugali wa wanawe kiasi kwamba siku lisipoenda linakufa njaa yeye na mitoto yake, lakini utakuta lipo hapa JF linalaumu eti rais hachukui hatua.

Ningekuwa mimi Magufuli ningesambaza jeshi mtaani hasa nijini na kupiga marufuku ya watu kutoka nje kwa wiki 2 tu, yani wiki 2 tu wala siyo tatu wala nne, nakwambia hata haya machadema mbona akili zitarudi tu!

Hata hawa maaskofu wanaopiga kelele za corona huku wakiendelea kuruhusu misa, ningekuwa Magufuli piga ban ibada zote kwa miezi miwili tu uone kama akili hazijawakaa sawa. Sasa hivi wanaoiga kelele si makapu ya sadaka bado kila jumapili yana jaa!
Yani kama wewe unavyowaza,na yeye huku anawaza akithubutu tu kufanya unachomshauri hapati kodi,miradi yake yote itasimama.
 
Jitu lipo kila siku lina zurura kariakoo kutafuta ugali wa wanawe kiasi kwamba siku lisipoenda linakufa njaa yeye na mitoto yake, lakini utakuta lipo hapa JF linalaumu eti rais hachukui hatua.

Ningekuwa mimi Magufuli ningesambaza jeshi mtaani hasa nijini na kupiga marufuku ya watu kutoka nje kwa wiki 2 tu, yani wiki 2 tu wala siyo tatu wala nne, nakwambia hata haya machadema mbona akili zitarudi tu!

Hata hawa maaskofu wanaopiga kelele za corona huku wakiendelea kuruhusu misa, ningekuwa Magufuli piga ban ibada zote kwa miezi miwili tu uone kama akili hazijawakaa sawa. Sasa hivi wanaoiga kelele si makapu ya sadaka bado kila jumapili yana jaa!
Elimu, Elimu, Elimu...
 
Huu ujinga ulioandika inaonekana umepoteza muda bure, muda huu ungeutumia kwenye maombi na kufuata miongozo ya WHO ingekusaidia sn wewe na jamii nzima.
 
Back
Top Bottom