Emmanuel Robinson
JF-Expert Member
- May 29, 2013
- 1,503
- 1,139
Mimi nimeshangazwa sana na unafiki wa baadhi ya watanzania wenzetu. Kila siku wanapiga kelele kuhusu corona na kumlaumu mheshimiwa Rais kwamba hachukui hatua ni hatua zipi wanazozitaka? Unafiki wako sasa mtu anakaa baa anakunywa pombe yake hana hata barakoa akimaliza anakuja jamii forum kupiga kelele.
Mwingine kutwa anazurura tu mtaani wala hana barakoa akitosheka anakuja JamiiForums kupiga kelele. Sasa mimi najiuliza kwa nini huyu mtu asikae nyumbani ajikinge na familia yake? Serikali haijawahi kutumia mgambo kuwakusanya watu majumbani kuwaleta mjini au kutumia mgambo kuzuia watu kuvaa barakoa!
Unamfiki mkubwa kabisa ni ule wa kulazimisha mheshimiwa Rais aseme eti ndiyo mtu avae barakoa. Ikiwa unaona hatari kwa nini usivae barakoa kjuikinga badala yake unataka hadi Rais atoe kauli?. Yaani ukiingia humu mtandaoni utadhani kwamba Watanzania sasa wameisha ! Kwanini presha inakuwa kubwa zaidi?
Shida ninayoiona ni watu kutaka kutumia fursa ya corona ili kutimiza ajenda zao za siri. Angalia kina Peter Msigwa wanachoandika angalia waliobomolewa nyumba Kimara kina Kigogo anagalia waliosahauliwa na system kina Kagasheki wanachoandika Twitter. Hii yote inaonyesha hasira waliyonayo dhidi ya serikali ya awamu ya tano.
Angalia wanavyomtukana waziri wa afya tatizo lake ni nini. Teknolojia tuliyonayo njia ilizotumia serikali ndizo sahihi. Mtu anakuja na wazo shule zifungwe je kuna mwanafunzi yoyote amefariki huko mtaani kwako? Mwalimu je? Hiyo siyo sample ya kutosha kukuonyesha hali halisi?
Ni vizuri kama Watanzania tukaacha tofauti zetu na kuangalia maslahi mapana ya taifa letu. Badala ya kupiga kelele anza kuchukua hatua wewe binafsi na familia yako.