Unafiki: Black Lives Matter everywhere, not only in US

The Genius

JF-Expert Member
May 29, 2018
574
1,000
#PichaYaKwanza; Polisi huko Nakuru, Kenya akimburuza kwa pikipiki mwanamke mmoja aliyekamatwa kwa tuhuma za wizi. Polisi walimfunga mikono na miguu kisha wakamburuza kwa pikipiki kuelekea kituoni.

Lakini kabla ya kufika kituoni alikua ameshapata majeraha mengi na nguo zake zote kuchanika na kubaki uchi wa mnyama. Just imagine ukatili na udhalilishaji mkubwa kiasi hiki? Na ni mama mtu mzima ambaye hao askari wanaweza kuwa na umri sawa na wanae

Nimeiona video alipokua akiburuzwa akilia kwa uchungu na kuomba wamfungue. Askari mmoja anajibu kwa dharau kwamba "ng'ata hiyo kamba uikate". A high level of brutality

Lakini hutasikia mtu yeyote akisema BlackLivesMatter wala hutaona watu wakiandamana. Simply kwa sababu mtu mweusi kamfanyia ukatili mweusi mwenzie. Lakini ingekua imetokea Marekani ungeshangaa vijana wa Bukene hadi Sanya juu wameandamana na mabango BalackLivesMatter. UNAFIKI

Wasanii wetu Bongo nao eti walienda ubalozi wa Marekani kulaani tukio la kuawa George Floyd lakini hawajasema lolote kuhusu tukio hili la Kenya. Bila shaka hawajui ubalozi wa Kenya ulipo.

#PichaYaPili; Dereva bodaboda aliyeuawa mwezi April na polisi mjini Nairobi baada ya kudaiwa kukiuka agizo la Lock down. Huyu kijana mkewe alikua mjamzito. Na siku ya kujifungua alimbeba kwenye pikipiki yake hadi hospitali.

Wakati anarudi ndipo akakutana na polisi ambao walimdhalilisha na kumpiga sana. Alifariki dunia siku chache baadae kutokana na majeraha kichwani. Mkewe aliporudi kujifungua badala ya baba kumuona mtoto, mtoto anaoneshwa kaburi la baba. Just imagine.

Lakini hakuna aliyesema BlackLivesMatter kwa ukatili huu. Tunasubiri yatokee Marekani ndipo tupanue midomo. UNAFIKI. Black lives matter everywhere not only in US.

Mtu mweusi ni mnafiki sana, hasa anayeishi Afrika. Vyama vya siasa na NGOs zilishindana kutoa matamko ya kukemea tukio la George Floyd. Nasubiri kuona matamko yao kuhusu huyu mama wa Kenya maana ni tukio la siku mbili tu zilizopita. Chadema, CCM, ACT, CHAUMA etc we are waiting 4u.

Tusijifanye tunathamini sana maisha ya mtu mweusi aliyepo Marekani kuliko ya mweusi aliyepo Afrika. Unawezaje kuona kibanzi kwenye jicho la mwenzio while jichoni kwako una boriti? UNAFIKI.!!

Malisa GJ
FB_IMG_1591963424461.jpg
 

Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
17,794
2,000
Muda huyo mama na huyo kijana wanapitia hayo bwana Floyd alikua bize kuigiza porn.

Ifike hatua tujue yanayotuhusu.
 

Consultant

JF-Expert Member
Jun 15, 2008
9,187
2,000
Waafrika wengi ni Wanafiki kupita maelezo. Sasa huyu Polisi aliyemkanyaga huyo kijana ana tofauti gani na yule jamaa aliyemuua Gorge Floyd mchana kweupe?
 

Bhanunu

JF-Expert Member
Jan 1, 2014
768
250
Muda huyo mama na huyo kijana wanapitia hayo bwana Floyd alikua bize kuigiza porn.

Ifike hatua tujue yanayotuhusu.
Sasa Kwani alikuwa anafanya kosa gani? Alikiwa anaingiza kipato kihalali, kwa hiyo sio kosa , kwa sheria za nchi zake sio kosa
 

Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
17,794
2,000
Sasa Kwani alikuwa anafanya kosa gani? Alikiwa anaingiza kipato kihalali, kwa hiyo sio kosa , kwa sheria za nchi zake sio kosa
Hata mimi sijasema ni kosa. Point yangu ni kwamba 'Alikua anaendelea na mambo yake'
 

Agenda1

JF-Expert Member
Aug 11, 2017
1,420
2,000
Serikali ya kenya, wanaharakati nchini Kenya wameyakalia kimya matukio haya?
 

Bana likasi

JF-Expert Member
Jan 7, 2020
6,968
2,000
Lockdown Polisi Kenya imeuwa jumla ya wakenya 15.Uganda polisi aliuwa mtu na mkewe wakiwa kwenye bodaboda kwa kuwapiga risasi.
 

Bana likasi

JF-Expert Member
Jan 7, 2020
6,968
2,000
Eti USA mwafrika mmoja anauwawa wote wanaandamana,waje Africa waone, dikteta mmoja anauwa hata watu elf 20 na maisha yanaendelea kila mtu na hamsini zake Hakuna cha maandamano Wala nn.
 

adriz

JF-Expert Member
Sep 2, 2017
1,123
2,000
Inasikitisha sana ,halafu kama hakuna kitu kilichotokea sioni mashirika ya utetezi tunayoyafagilia ila nawaza ingekuwa Tz sijui ingekuwaje ...
 

sawima

JF-Expert Member
Jul 9, 2019
2,798
2,000
Mleta mada umenena watu wanajifanya hawajui yanayoendelea huku Afrika.

Juzi nimemsikia rais wa Afrika kusini akikiri nchi yake ni sehemu hatari zaidi duniani kwa maisha ya mwanamke

Ripoti inaonesha kila baada ya saa tatu huko south mwanamke mmoja anauwawa lakini watu hawasemi kitu ila wanaona tu ya US.
 

Bana likasi

JF-Expert Member
Jan 7, 2020
6,968
2,000
Polisi brutally ukatili wa polisi africa ni zaidi ya wenzetu, polisi kuuwa watu Africa ni sawa na kunywa Pepsi. Waafrika twatendeana ukatili Mkubwa sana ili kumfurahisha mtawala kuliko hata alivofanya mkoloni.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom