Unafahamu vipi kuhusu miaka 6000 ya ukomo wa Dunia?

Unafahamu vipi kuhusu miaka 6000 ya ukomo wa Dunia?

Hii hoja nimekuwa naisikia kitambo sasa
 
Wanasayansi wanasema ulimwengu una miaka bilion 13 toka utokee lakini lakini watu wa dini wanasema ulimwengu una miaka 6000 toka umeumbwa.
Kwahiyo nani tumuamini.
Lakini hapo wakumuani ziadi ni wanasayansi kwasababu hii dunia inaendeshwa kisayansi.

Na huyo wanae sema atauleta mwisho wa dunia ataanzia wapi hii dunia ni kubwa sana.
Kila mtu achague anaye muamini,mimi siwezi kuamumini mwanadamu mwenzangu ambaye anakufa bali ntamwamini Mungu asiyekufa
 
ACHANENI NA MAMBO YASIYOWAPATIA WOKOVU,HATA KAMA UKIJUA DUNIA INA MIAKA MINGAPI UNADHANI KWA AKILI YA KAWAIDA ITAKUSAIDIA NINI?

TUBUNI MLEJEE MPATE KUSAMEHEWA
 
ACHANENI NA MAMBO YASIYOWAPATIA WOKOVU,HATA KAMA UKIJUA DUNIA INA MIAKA MINGAPI UNADHANI KWA AKILI YA KAWAIDA ITAKUSAIDIA NINI?

TUBUNI MLEJEE MPATE KUSAMEHEWA
Mkuu unatufokea 😀 😀 😀
Ila kiukweli badala ya ku focus, na kusaidia wajane, kuhudumia yatima, kupenda jirani zetu,n.k.

Everyday is Saturday...........................😎
 
M/MUNGU ameficha baadhi ya mambo ambayo ni beyond na human brain.1.ameficha siku yako ya KUFA 2.ameficha matendo yako siku ya kiama 3.ameficha kiumbe tumboni kuwa ni jike au dume.(kabla ya kupuliziwa roho tumboni).4.ameificha siku ya kiama .
Japo ktk hii siku ya kiama Allah amemuelezea mtume Muhammad s.a.w dalili ambazo amezisimulia ktk hadithi zake na ktk Quran pia.dalili za kiama ni nyingi sana lkn zifuatazo ni baadhi.
1.Mauaji ya kutisha yasiyo sababu Bali ni propaganda tu za wauaji tunaona mifano.mashariki ya Kati,n.k
2.maasi na maradhi zasiyokuwa na dawa mfano Aids.etc
3.amana itakapokuwa haipo au kupoteza kwa amana .mfano ukimpa MTU kitu km pesa akupelekee sehemu.au kutunza.je utazipata tena?
4.dunia kuwa km kijiji.tunaona zama hizi
5.wanawake kutembea uchi na kuvaa Nguo lkn hawajavaa.
6.smoke to the entire world.wengine wanatabiri ni nuclear bombs zitaripuka na kuathiri duniani
7.Masiihu dajjal (a person with one eye who will distribute bad morals and killings and fisaad (uharibifu)duniani.
8.a giant animal will appear from down the earth who will cause devastation
Zipo dalili nyingi lkn NIMEANZA na hizo kwanza.nitrudi inshallah
hoja za watoto hizi

1.ameficha siku yako ya KUFA 2.
si kwa wote
kuna watu wanajua wanakufa lini tena anaacha na barua na anaamua afe kwa njia gani
 
[QUOTE="fungi, post: 16618012, member: 215472"
Umri wa dunia mpaka sasa ni zaid ya miaka bilion 4
na bado ipo ipo sana provided hakutotokea any changes kweny mother nature
[/QUOTE]..... Sema dunia inamiaka bill 4 na jua. Lina nimiaka bill 7 lkn binadam ameanzs. Kuishi. Duniani miaka 6000+ iliopita
 
Hatutatoboa 2100. Hatutaishi mfumo huu wa sasa Yesu atakuwa karudi. Bado kuna miaka 1007, 7 dhiki kuu. 1000 utawala wa Kristo duniani. Jumla dunia inatakiwa ifikishe miaka 7000, namba 7 ya ukamilifu. Baada ya hapo hakutakuwa na kitu kinaitwa Earth ulimwenguni.
 
Wakuu, heshima kwenu. Naleta kwenu mjadala huu unaohusu mpango wa Mungu kwa ukomo wa sayari dunia ambao kuna watu wamekuwa wakisema kuwa, Mungu kaipangia Dunia miaka 6000. Wanaodai hivyo wamekuwa na hoja wanazozitoa kuhalalisha madai yao. Nitaleta kwenu baadhi ya hoja hizo, na kwa kadri ya kila mtu anavyofahamu, ataongezea ili hatimaye nami pamoja na wengine tupate kitu.
Hoja namba 1
Kwamba, Mungu aliumba mbingu, nchi na bahari kwa muda wa siku sita na ya saba akastarehe.
Hoja namba 2
Yanatumika mafungu kadhaa ya biblia ambayo japo yana maana halisi (literal meaning), lakini yanatumika pia kama yalikuwa yanalenga kutoa ujumbe wa kinabii (prophetic meaning). Baadhi ya mafungu hayo ni haya yafuatayo.
Kutoka 21:2 Ukimnunua mtumwa wa Kiebrania, atakutumikia muda wa miaka sita; mwaka wa saba atatoka kwako huru bure.
Kutoka 23:10-11
Utapanda mbegu katika nchi yako muda wa miaka sita na kuyavuna maongeo yake; lakini mwaka wa saba utaiacha nchi itulie na kupumzika..

Joshua 2:2-5 ...fanya hivi siku sita. Na makuhani saba watachukua tarumbeta saba
za kondoo waume, mbele ya hilo sanduku; na siku ya saba
mtauzunguka mji mara saba.

Hata ukisoma habari za naamani, safari ya saba kujichovya katika maji, ndipo akatakasika ukoma wake.

Hoja hizo zote zinatumiwa kufikio hitimisho kuwa, Mungu hukamilisha mambo yake katika mfuatano wa vipindi 6, inaweza kuwa siku sita, majuma au miaka. Na kwenye ufunuo inaeleza watakaokwenda mbinguni, ama pasipo kuonja mauti au kwa kufufuliwa, watatawala na kristo miaka 1000 (Ufunuo 20:1-5). hivyo wanahitimisha kwa kusema kuwa. Muda ambao Mungu kaipa dunia (baada ya dhambi) ni miaka 6000, na miaka 1000 ni ya kupumzika mbinguni. Jumla miaka 7000, ndipo mbingu mpya na nchi mpya zinatengenezwa. Umeshawahi kusikia nadharia jii? kama ndiyo, hebu ongezea kuhusu ulivyosikia wewe.
cc: Ntuzu mshana jr TODAYS Eiyer na wadau wote, karibuni.
Hata ukihesabu kwa miaka 6000 inamaana sio hii miaka tunayohesabu sisi ya 2020, hii ilianza baada ya Yesu. Sasa kama ndivyo, kwake yeye anahesabu tangu alipoiumba na hapo ni baada ya miaka kadhaa ndipo akaumbwa Adam akaletwa. Mitume wa Mungu wapo 25 ambapo ltk hao Yesu alikuwa wa 24 na Mwisho ndio akaja Muhammad (Saw). Sasa kutoka Adam, Luth, Isaac, Ismail, Yusuph, Ibrahim, Nuh, Suleiman na wote wa Kabla watakuwa wametumia miaka mingapi tayari? So kama dhana hii ni kweli, basi dunia itakuwa imebaki miaka michache mno. Na inapaswa kuwa ni 6999 , ikitimia tu 7000 balaa linaingia
 
Hata ukihesabu kwa miaka 6000 inamaana sio hii miaka tunayohesabu sisi ya 2020, hii ilianza baada ya Yesu. Sasa kama ndivyo, kwake yeye anahesabu tangu alipoiumba na hapo ni baada ya miaka kadhaa ndipo akaumbwa Adam akaletwa. Mitume wa Mungu wapo 25 ambapo ltk hao Yesu alikuwa wa 24 na Mwisho ndio akaja Muhammad (Saw). Sasa kutoka Adam, Luth, Isaac, Ismail, Yusuph, Ibrahim, Nuh, Suleiman na wote wa Kabla watakuwa wametumia miaka mingapi tayari? So kama dhana hii ni kweli, basi dunia itakuwa imebaki miaka michache mno. Na inapaswa kuwa ni 6999 , ikitimia tu 7000 balaa linaingia
Umechanganya mafaili hapo kwenye mitume.
 
Kila kitu kiliumbwa ndani ya siku sita

MWANZO 1 : 1
" Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi"
Kuna uumbaji ulishafanyika hapo awali, kabla huo uliotajwa Mwanzo 1:1. Mfano, when were angels created?
 
Back
Top Bottom