Unafahamu "Competitive Intelligence" ni nini?

The Consult

JF-Expert Member
Jan 20, 2017
220
252
1115827

Competitive Intelligence ni kitendo cha kampuni kukusanya (gathering) na kuzifanyia kazi (analysis) taarifa za kisoko kwa lengo la kufanya maamuzi ya kimkakati (Strategic Decisions Making). Kitendo hiki pia hujulikana kwa jina la "Business Intelligence". Competitive Intelligence ni nyanja (field) inayochipukia kwa kasi katika masuala ya Mipango Mkakati. Tafiti mbalimbali zinaonyesha kwamba; kuna uhusiano mkubwa kati ya utendaji wa kampuni (corporate governance) na kufanya " Competitive Intelligence"

Kutokana na "survey" iliyofanywa na wataalamu wa "competitive intelligence", inaonyesha kwamba; asilimia 79.2 ya "competitive intelligence" hufanywa kwa ajili ya kutengeneza bidhaa mpya sokoni, asilimia 73.6 ya "competitive intelligence" hufanywa kwa ajili ya kutengeneza mbinu na mikakati ya kimasoko, pia "survey" inaendelea kuonyesha kwamba asilimia 90.6 ya "competitive intelligence" ni kwa ajili ya kujenga ufahamu katika biashara (industry). Mwanzoni mwa miaka ya 1990; asilimia 78 ya makampuni ya Kimarekani na Ulaya yamekuwa yakifanya " competitive intelligence" na kazi hii imekuwa ikifanyika katika idara za masoko (marketing departments), idara za mipango mkakati (strategic planning department) pia katika idara za huduma za mawasiliano (information services department) katika kampuni hizo.

Kutokana na survey iliyofanywa 2007 na McKinsey & Company kwa makampuni makubwa141 ulimwenguni, inaonyesha kwamba; kampuni hizi zimekuwa zikitumia kiasi kikubwa cha fedha kwenye "competitive intelligence" ambapo matumizi yalionyesha kupanda kutoka Dola bilioni moja ya Kimarekani 2007 mpaka Dola bilioni 10 za Kimarekani mwaka 2012.
Kuna baadhi ya kampuni kwa sasa zimekuwa zikiwa-train wafanyakazi wake katika ukusanyaji na ung'amuaji wa taarifa za kiushindani kutoka kwenye vyanzo mbalimbali, kwa mfano kwa sasa, kampuni ya General Mills ya nchini Marekani inafanya kitu hiki.

Upatikanaji wa Taarifa

Kampuni nyingi ulimwenguni, hutumia vyanzo vya nje kwa ajili ya kukusanya taarifa. Kampuni kama A. C. Nielsen Co hutoa taarifa za kimasoko kwa wateja wake mara mbili kwa mwezi, taarifa hizi hutumiwa na wateja wake kwa ajili ya kufanya maamuzi ya kimkakati. Taarifa kuhusu taratibu za kiserikali, ushindani sokoni, bidhaa mpya iliyoingia sokoni huweza kununuliwa kutoka kwa kampuni dalali (information brokers) kama vile Market Research.com (Findex), LexisNexis n.k

Mapinduzi ya teknolojia ya mawasilano kwa kiasi kikubwa yamerahisisha ukusanyaji na upatikanaji wa taarifa za kimasoko. Tatizo kubwa litokanalo na taarifa hizi ni uaminifu wake (authenticity); ni ngumu wakati mwingine kujua ukweli wa taarifa ipatikanayo kwa njia hii, hivyo wakati mwingine huweza kupelekea kufanya maamuzi yasiyo sahihi kutokana na kukosekana kwa usahihi wa taarifa.

Ni muda sasa, kampuni zetu za ndani zikaichukulia COMPETITIVE INTELLIGENCE CAPACITY kama hazina na zana muhimu katika faida ya kiushindani (competitive advantage tool) ambayo kampuni inaweza kuitumia katika kukabiliana na mshindani wake sokoni, kama kampuni nyingi za Ulaya na Marekani zinavyofanya sasa.

Ahasante

The Consult; +255 719 518 367
E-mail; theconsult38@gmail.com
Dar es Salaam
Tanzania

Home of Project Management, Strategic Management & Fundraising Strategies
 
Hakika Mkuu.
Ni muhimu hata kampuni/biashara zinazochipukia zizingatie hii kitu. Ni muhimu sana katika mazingira ya ushindani.
 
Hatuna budi kufikia level hiyo katika marketing, ushindani umekua mkubwa sana
 
I
View attachment 1115827

Iko poa sana kwa nchi yetu tools zipi can be used for competitive intelligence? Wenzetu wanatumia zaidi technology na hasa sababu information zao nyingi na biashara ziko kwenye systems na sites ..tunaweza analyse tools chache au mbinu za kutumia kwa nchi zetu kufanikisha hili..baadhi nilivyowaza Mimi:-

1) kuwa karibu na serikali ili kupata siri za kinaenda kutokea baada ya muda flani na wewe kujiweka tayari kibiashara

2)kuwapeleleza zaidi washindani wako kiundani hata kwa kuwatumia watu wasupport biashara zao kumbe unatafuta siri za ndani

3)kuplay rough games kwa retailers kama wewe ni distributor hata kuwa unawalipa waweke products zako front na ikibidi wakiulizwa product ya msindani wako waiponde na kusifia yako

4)kama mpinzani wako anawafanyakazi ambao ndio kichocheo kikubwa sababu wanajua biashara peleleza wanafanyaje na wako wafanye hivyo kwa kujifunza,ikibidi pandisha dau hata Mara 2 ya wanachopata then wachukue
5)cheki watu gani wanamfanyia ishu zake za mahesabu na wanafanyaje were kafanye zaidi

6)Chunguzavmbinu anazotumia kukopesheka fatilia na wewe IGA au mzidi

TUONGEZEE ZINGINE THOUGH NIMEANDIKA KWA KUANGALIA KAMPUNI KUBWA KIDOGO
 
Back
Top Bottom