IKARAHANSI
JF-Expert Member
- Jul 30, 2019
- 398
- 479
Kwa mara ya kwanza nakusoma mama D ukiandika kwa hisia sana! Dah! Ulivyotumia hilo neno hapo sasa: ^kihuni sana^ 🙂 🙂 🙂Kitu kinachoitwa Mfumo dume kimeingizwa kwenye jamii kihuni sana.
Neno mfumodume limeshindwa kutenganisha majukumu ya mwanaume na mwanamke na kwa kutozingatia majukumu yao kwa asili ya uumbaji wa Mungu.
Neno mfumodume limefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuweka gap kubwa sana na kuharibika kwa maana halisi ya ndoa kadri ya uumbaji na imani zetu.
Leo wanawake vichwa ngumu na wanaume vichwa ngumu.... hata lile andiko la Efeso 5:23 "Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili." linapoteza maana kila siku. Bila kujua maana ya haki sawa na zipi haki sawa Siku hizi mwanaume anadai haki sawa na mwanamke anadai haki sawa
Jameni haki sawa zipogi tuu kama kupata elimu sawa, matibabu, kazi za jamii ila mengine tukiingiza hii kitu tutakufa tukiwa tumechoka sanaa
Kwa hiyo generation hii haina dawa tena, mama D ? Au ndiyo yale ya samaki akikauka hakunjiki tena?Tufanye bidii kubadilisha watoto wetu labda tutanusuru generation ijayo
Kwa hiyo generation hii haina dawa tena, mama D ? Au ndiyo yale ya samaki akikauka hakunjiki tena?
Sasa familia ni yao, mume ni wa mke, na mke ni wa mume. Shida iko wapi? What's the difference? Au mimi ndiye sijaelewa ^key-two^ hapa? I mean, ukitoa pesa kwenye mfuko mmoja, zinaingia mfuko wa pili.Hii generation ya ajabu sana. Nilikutana na ugomvi wa mume na mke siku moja hii familia ina watoto 3, mke anasema amechoka na kutumikishwa... pesa yake ndio inatunza familia(kula,kulala, kuvaa, ada), na bado ameto mtaji ambao mume ndio anasimamia biashara lakini huyo mume hataki kulipa hata school fees za watoto.
Nikasema wanawake sie mabingwa wa kujieleza hebu nimsikilize mume wake!
Weeeee! Mwanaume kacharauka povu kama loteeee anasema mke ana biashara nyingine pia hiyo ndio inatakiwa kulisha familia, halafu suala schoolfess kwa watoto wao lazima wagawane sawa kwa watoto wawili; na kama huyo mmoja hatamlipia atajua mwenyewe😥😥😥
nasikia anaupiga mwingi mpaka unatoka uwanjani mpira!
Ubarikiwe sanaAhsante mleta Uzi..naendelea kusoma comments na kujifunza
So tukae tukitazama jamii ikiangamia.Men wametawala muda mrefu sana; duniani sasa ni zamu ya females. Just relax guys, power is stealthily & steadily sleeping from your flimsy hands!