Unadhani una Matatizo ya kifamilia....soma kisa hiki

Mama

JF-Expert Member
Mar 24, 2008
2,848
58
Jamaa wawili walikutana kwenye kituo cha basi wakafanya mazungumzo. Mmoja aling'ang'nia kuzungumzia kero za familia yake hatimaye mwenzake akasema " Unadhani familia yako ina matatizo?"

Basi sikiliza kisa hiki.

"Miaka michache iliyopita nilikutana na mwanamke mjane aliyekua na binti mkubwa tu na tukaamua kuoana. Baadaye baba yangu akamuoa binti yangu wa kambo hivyo huyo binti yangu wa kambo akawa mama yangu wa kambo na Baba yangu akawa mtoto wangu wa kambo wa kiume ambapo mke wangu akawa mama mkwe wa mkwe wake.

Baadaye binti ya mke wangu yaani binti yangu wa kambo alipata mtoto wa kiume. Mtoto huyo wa kiume akawa ndugu yangu kwa sababu tulichangia baba mmoja. lakini kwa vile alikuwa ni mtoto wa binti wa mke wangu papo hapo akawa mjukuu wa mke wangu na mimi nikawa babu yake mdogo wangu.

Lakini hayo yote yalikua si kitu mpaka mimi na mke wangu tulipopata mtoto wa kiume. Sasa msichana ambaye ni ndugu wa mtoto wangu huyo wa kiume kwa kuchangia mama yao mmoja, akawa pia bibi yake. Hali hiyo ilimfanya pia baba yangu kuwa shemeji wa mtoto wangu ambaye ndugu yake wa kike kwa upande wa mama yao ndie mke wake baba yangu. Kwa hiyo mimi ni shemeji yake mama yangu wa kambo ambapo mke wangu ni mama mdogo (anti) wa binti yake mwenyewe . Kwa hiyo mtoto wangu wa kiume ni mpwa wa baba yangu ambapo mimi ni babu yangu mwenyewe.

SWALI.

Je, unadhani mpaka hapo wewe una matatizo ya kifamilia? Acha kulalamika!
 
Binaadamu wote wanamipaka .. hata mila na diini zetu zinatuelekeza na kutupa mipaka

hao watakuwa jamii ya wanyama flani
 
Back
Top Bottom