Francis12
JF-Expert Member
- Sep 30, 2016
- 7,533
- 22,278
Nanakili kutoka kwa Comrade Dotto Bulendu.
_______________________________________________
Gazeti jipya la "Mwelekeo" limendika hii leo kuwa aliyekuwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu alifukuzwa baada ya kudaiwa kuzima jenereta wakati wa mkutano wa kampeni wa Rais Magufuli huko Iringa na kusababisha Rais Magufuli wakati huo akiwa mgombea asisikike vizuri.
Ramadhani Madabida yeye anatuhumiwa kumfananisha Lowasa na Mtume, jambo ambalo wajumbe walisema hilo ni kosa kubwa!.
Huku Sophia Simba yeye anadaiwa kuwa hata baada ya uchaguzi,aliendelea kwenda nyumbani kwa Edward Lowasa kwa kificho akiwa kavaa hijabu,na hivyo kudaiwa kuwa amekuwa akipeleka siri za chama kwa Lowasa!.
Erasto Kwilasa wa Shinyanga,yeye ametuhumiwa kupeleka siri za chama mkoa wa Shinyanga kwa mtangulizi wake Hamis Mgeja,huku Christopher Sanya yeye alisusa kushiriki kampeni za Ubunge baada ya jina lake kukatwa.
___________
Nini maoni yako? Unadhani tuhuma hizi zina uzito wa kutosha kuwafukuza uanachama viongozi hawa? Je hizi ni tuhuma kweli au ni majungu na umbea? Kamati kuu ya CCM kukaa na kujadili kwamba kuna mtu alikua akienda nyumbani kwa Lowassa akiwa amevaa baibui, haya si majungu? Nani alimuona? Kama baibui huficha sura alijuaje ni Sophia Simba? Je unadhani haya ni majungu? Na je ni sahihi vyombo vikubwa vya maamuzi vya CCM kukaa na kujadili taarifa zinazoonekana ni majungu na umbea??