Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 361,078
- 831,704
POLISI MBEZI KWA YUSUFU MNASTAHILI PONGEZI!
Mtu huyu (pichani) aliyejitambulisha kwa jina la Juma kutokea maeneo ya Bulula - Kimara Suka alikuwa amekamatwa akituhumiwa kufanya vitendo vya wizi leo mchana eneo la Rift Valley, Kimara Suka. Watu wenye hasira walikuwa wakimshambulia kwa mawe, mapanga, nk! Ilikuwa ni neema ya Mungu nilikuwa natoka kumsindikiza Mchungaji aliyenitembelea ndipo nikasikia mayowe na kelele. Nilipofika eneo la tukio nilikuta hali ya mtuhumiwa siyo nzuri! Nilichofanya ni kwenda kusimama kando yake na kutoa ishara ya kuwataka watu waache kumpiga.
Ninamshukuru Mungu watu wale walitii sauti yangu ingawa wapo waliokuwa wakisubiri niondoke ili waendelee .......
Niliamua kupiga simu katika kituo cha Polisi Mbezi Kwa Yusufu. Wakati Polisi wakijipanga kuja na nilipogundua kuwa mazingira yale yalikuwa hatarishi kwa mtuhumiwa, nilifanya utaratibu na nikafanikiwa kumsogeza mbele kidogo ili kuokoa maisha yake. Ninaushukuru sana Uongozi wa Kituo cha Polisi cha Mbezi kwa Yusufu kwa kuitikia wito wangu wa ghafla.
Kipekee ninamshukuru sana Afande Zena aliyeongoza Kikosi cha Polisi waliokuja kumchukua mtuhumiwa kwa kutumia gari la Polisi. Ninawashukuru pia watu waliokuwa wanampiga mtuhumiwa kwa kutii sauti yangu kama mtumishi wa Mungu ya kuwataka kuacha kumpiga na hivyo kuepusha umwagaji wa damu ya mtu katika eneo lao. Ninamshukuru sana Mungu kwa kuwa sasa mtuhumiwa yupo salama katika mikono ya Polisi ambako taratibu za kisheria zitaendelea. Mtuhumiwa aliumia sana maeneo ya kichwani ila sikutaka kamera yangu ionyeshe majeraha. Tumuombee mtu huyu ili Mungu ampe neema ya kuokoka na kumwamini Yesu.
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki 12 Oktoba 2007.