Unachotakiwa kukijua kuhusu ndoa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unachotakiwa kukijua kuhusu ndoa

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Mar 28, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Mar 28, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 28,301
  Likes Received: 3,208
  Trophy Points: 280
  WIKI iliyopita nilikuwa na mizunguko katika mikoa ya Tanga, Morogoro na Dar es Salaam ambako nilikutana na watu mbalimbali kwa lengo la kushauriana kuhusu masuala ya ndoa.

  Utaratibu wa aina hii utaendelea, kutokana na ukweli kuwa kuna idadi kubwa ya watu wameonyesha kuhitaji kufanyiwa ushauri hasa wa ana kwa ana.

  Baadhi ya mambo ambayo niliyazungumza na ambayo baadhi yake nitaendelea kuyasisitiza ni namna ya kuifanya ndoa kuwa sehemu ya amani. Msingi wa kuwa na ndoa nzuri ni kwa wanandoa kukumbushana majukumu yawapasayo.

  Msingi wa kuanguka kwa ndoa nyingi ni pale upande mmoja au pande zote zinaposhindwa kutimiza kile ambacho kinawapasa kufanya. Kwa mfano yawezekana uko kwenye ndoa, ni kweli wewe ni mwanaume mwenye uwezo wa fedha, wengine wanawanunulia magari au kuwafanyia mambo mazuri wake zao.

  Hata kwa wanawake pia, wapo ambao wamekuwa wakiwafanyia yaliyo mazuri wanaume zao hasa kwa kuwapa fedha nk, lakini wanashindwa kufahamu kuwa suala la kula vizuri au fedha sicho hasa muhimu kwa wanandoa.

  La muhimu katika ndoa ni kuangalia pande zote, kwa mfano kama ni kweli uko sawa kwenye suala la fedha, unapaswa kuangalia pia katika suala la mahusiano na mahaba kwa ujumla, je kama mwanaume, una uwezo wa kushughulika kama ambavyo mwanaume anapaswa.

  Tafiti zinaonyesha kuwa katika siku za hivi karibuni kumekuwa na wanaume wengi wenye kusumbuliwa na tatizo la nguvu za kijinsia...wengine ninapozungumzia suala hili, huwa wanaona kama nafanya masihara, lakini ukweli ni kwamba mwanamke anamuhitaji mwanaume lijali, aliyekomaaa, eeeh kiasi kwamba hata akiwa mbali anaseme yaani yule mwanaume we acha bwana, sijawahi ona.

  Kwa kawaida inapaswa ukitoka katika chumba cha mahaba na mwanamke hadi akitema mate yaangukie kifuani�sio chini. Eeeh akitema mate puu!!! Yaangukie kifuani�tiii!!! Hapo ni swa kabisa. Hizo ndizo nguvu zimpasazo mwanaume kuwa nazo.

  Lakini zaidi ya yote haitii raha hata kidogo, kuna watu kama namna ya kula kila siku ni kifo cha mende�.tena wengine hawajishughulishi katika mahaba�wengine wanasema �aaah kama tayari niambie nataka kuwahi�.

  Vitu kama hivi kwa ujumla vinakinaisha mahusiano. Ni jambo la msingi sana katika maisha ya wanandoa kupenda kujifunza vitu vipya, kupenda kuangalia na kufahamu mwenzangu anapenda nini na nimfanyie nini.

  Si vizuri kwa mfanya kujipendelea, kama ilivyo kwa wanaume walio wengi. Juzi nilikuwa nazungumza na kijana wa kabila Fulani, ndio kwanza kaingia mjini kutokea kijijini, akawa ananiambia aaah mimi sitakaa nioe Dar.

  Nikamuuliza kwa nini�akajibu kwamba wasichana wengi wa Dar wana manjonjo�eti mwanamke tikisika�aaah mbaya kabisa, eti �sichana� nyonya huku mimi�aaah mkosi.

  Baada ya kumfuatilia kwa makini, kumbe aliingizwa mjini na baa medi fulani, alimfanyia mikogo na miondoko hadi alikoma mwenyewe�wizi mtupu. Akawa anafikiri anamfurahisha, lakini kumbe kwa staili ya kabisa la yule kijana, hakufurahi hata kidogo, zaidi ni kwamba kuanzia siku hiyo alimchukia.

  Ni kwamba kuna baadji ya makabila yanamzuia mwanamke kucheza wala kufanya chochote, wala kutumia mikono yake wala ulimi nk, anapaswa kutulia tu, kama kuku kachinjwa.

  Nisingependa kulitaja hilo kabila, ambalo huenda likawa ndio pekee Tanzania kwa kuendeleza mila na utamaduni. Ninachotaka kusema hapa ni kwamba wakati mwingine kabla ya kuibuka na manjonjo, muulize mwenzi wako ungependa umfanyie nini. Unaweza kufanya kitu ukifikiri unatengeneza, kumbe unaharibu.

  Ambacho nataka kifahamike ni kuwa ni jambo la msingi kwa wanandoa kupenda kuwa na mazungumzo. Eeh hata nyumbani, utakuta mara nyingi wanawake wanapika vitu kwa mazoea, kwamba aaah mume wangu huwa anapenda wali au ugali. Lakini ni vizuri wakati fulani kumuuliza uonaje nikakupikia tambi nk.


  Wiki iliyopita katika kuzungumza na watu mbalimbali walipenda kufahamu siri muhimu ya kumjua mtu kama ni mwaminifu kweli au la.

  Unaweza kutaka kujua hili kama tayari mmeshaoana au hata bado. Ziko njia nyingi, ambazo binafsi naziona si nzuri. Iliyo nzuri na ambayo humkwazi mtu ni kwa wewe mwenyewe kufanya jitihada zako taratibu na kwa siri bila yeyote kufahamu.

  Ziko njia kwa mfano kuangalia simu ya mwenzi wako ambao kwa ujumla si nzuri, kwa sababu tayari akishajua kwamba huwa unaangalia, atamwambia huyo mwenzi wake kwamba asiwe anaitumia au asithubutu kupiga wala kutuma ujumbe, hadi yeye aanze nk.

  Kimsingi kuna njia nyingi za kuujua ukweli, lakini leo naomba nitangaze kwako njia moja nzuri na ya kipelelezi. Naamini tangu umeanza kusoma magazeti, kusikiliza redio wala kuangalia TV, hujawahi kuona hili, nitakaloliongelea.

  Licha ya kutumia njia zote, iwe ni kuwa karibu na rafiki zake nk, ambao kwa bahati mbaya wengine hawawezi kuwa na maelezo sahihi ya mtu husika nk. Ni suala la msingi wewe mwenyewe kufanya kile ambacho unaamini kwamba kitakusaidia.

  Mara kadhaa nimekuwa nikizungumza kwamba wakati mwingine kama unataka kumjua mtu ambaye unataka kuoana nae, ni vizuri kuwa karibu na rafiki zake, ni sawa lakini kuna watu wengine wana siri kubwa.

  Ukitaka kujua mtu kama ana siri kubwa au la, ni wepesi au ugumu wa kukupeleka nyumbani kwake anakoishi.

  Mtu yeyote ambaye ni mgumu kukupeleka kwake, jua huyo ni mwenye siri kubwa na kwa kiasi fulani ni vigumu kumjua, labda kama ataamua kufanya hivyo yeye mwenyewe.

  Kitaalam hata hivyo, kama mtu humuamini, si vizuri kumpeleka nyumbani kwako. Aidha katika nyakati hizi, acha kabisa tabia ya kumuonyesha mtu kwenye nyumba ambayo unaishi. Uwe makini na watu kwa sababu tumezungukwa na watu wengi wabaya.

  Juzi kuna jamaa alinipigia simu kwamba aaah kuna mwanamke nilikuwa nataka kuoana naye, lakini kwa sababu ambazo sasa naamini kweli ni Mungu yupo kwa kuwa hafai ningeteseka kwa kuwa mtumwa baada ya kuoana naye�eti kawasiliana na rafiki yangu, anataka kujua siri zangu na maisha yangu.

  Akaendelea kusema aaah ni rafiki yangu gani wakati hata nyumbani kwangu sikuwahi kumpeleka, wala sina muda naye, ni vile tu kwamba niliwahi kufanya naye kazi.

  Ni suala la msingi katika maisha kuwa makini na watu, hata marafiki wengine ni wapumbavu, ni watu ambao kama hutakuwa makini wanaweza kukuathiri, anaweza kukuchekea, huku anakung�onga.

  Kuna watu wamekuwa wakiniomba urafiki, kimsingi wote ni rafiki zangu, sihitaji kufuatana-fuatana, acha kila mtu awe na maisha yake, kuna jambo nitakusaidia, kama nina jambo nitashukuru ukinisaidia, usiponisaidia pia sawa, kwa sababu tunaambiwa shukuru kwa kila jambo.

  Katika maisha angalia vitu vya maana, wakati mwingine marafiki ni wabaya. Wakati mwingine watu wengine ni wapumbavu, wanaweza kukusababishia hasara, badala ya faida, jitenge na watu, au kama unaamua kuwa nao, uwe nao kwa umakini. Usijibweteke sana.

  Ile njia ambayo niliyoizungumzia kuhusu namna ya kumjua mtu kama ni mwenye kuiheshimu ndoa au la, wakati mwingine ni pamoja na kutumia vifaa maalum vya kurekodi sauti.

  Niia hii ni ya msingi sana kama una hofu kubwa sana na mchumba wako au mke/mumeo. Katika maisha ni muhimu kuwa na uhakika, acha kupenda kuhisi. Pia ni makosa makubwa kuhisi...kitaalam ni mojawapo ya njia ya kumfanya mtu kutenda mabaya.

  Kwa mfano ikiwa mwanamke au mwanaume alikuwa anakuogopa, sasa unapomwambia kwamba aaah wewe una mtu mwingine...ndio kusema atakuwa anaona aaah kumbe mtu mwenyewe hata kama sijafanya jambo ananisema...inaonyesha hata nikifanya hatajua.

  Tafakari kwa makini suala hili, chukua hatua. Unapaswa kusema jambo baada ya kuwa na uhakika, usiongee tu kama mpuuzi. Jua kuwa unamtuma akafanye hicho kibaya unachomuhisi nacho, ndivyo tafiti mbalimbali duniani zinaonyesha.

  Njia iliyo nzuri kama humuamini ni kuchukua vifaa maalum vya kurekodi, halafu unavichomeka aidha kazini kwake chini ya meza au kiti, au kama huko hauwezi kwenda, unaweza kukichomoka nyumbani hasa chini ya kitanda.

  Kuna vifaa vinaweza kurekodi sauti hata kama ni wiki nzima bila kuzimika. Baadhi yake vinauzwa ghali, lakini msingi hasa wa kuwa na maisha yenye amani ya kweli ni kujua ukweli, kwa hiyo hilo haliwezi kuwa ni ghali kwako.

  Vifaa vya aina hiyo viko vya aina nyingi, vingine ni vidogo sana, kiasi kwamba ni kama peni, baadhi yake ni kama saa, inaweza pia kurekodi hata picha na kamwe si rahisi kukiona kama utakihifadhi vizuri. Pia hata kama atakiona ni vigumu kufahamu kina kazi gani, labda kama naye atakuwa mjanja.

  NJIA RAHISI YA KUJUA UKWELI HARAKA:

  Kuna vifaa vya kurekodi vyenye uwezo mkubwa na nyingine tofauti, kama ni kifaa chenye uwezo mdogo, unachotakiwa kufanya ni kukihifadhi kwenye sehemu unayotaka kikae, kisha anzisha mada kwa mfano, unaweza kutoka hapo ulipokitegesha hicho kifaa kisha unakwenda mbali na kumpigia simu huyo mtu ukiamini kuwa atakuwa pale kisha unamsema 'mke wangu kuna mwanaume alinigia simu nashangaa anaongea vitu vya ajabu, kwani wewe kuna mtu anakufuatilia".

  Kauli hii inatosha kabisa kumfanya huyo mwanamke kumpigia simu mwanaume wa nje mwenye uhusiano naye na kumuuliza kama alipiga simu au la kwa mumewe. Ni muda mfupi tayari utapata ushahidi, labda kuwe na sababu ya kushindwa kuwasiliana naye.
   
Loading...