Unabii wangu umetimia! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unabii wangu umetimia!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyakarungu, May 18, 2011.

 1. N

  Nyakarungu JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2011
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  Nilikwishawaambia "mawe ni mepesi mkononi, ila ni mazito usoni" sasa leo hii imeanza tarime, mfano ni huu kuanzia sasa, na utaendelea kuwatokea viongozi (watawala)wote.

  Mimi ni miongoni mwa vijana tunaoitakia mema jamii yetu ya kitanzania, na kwa sababu hii sina budi kuwapongeza wananchi wa nyamongo kwa yale waliyoyafanya kwa kuwaadhibu hao wawakilishi fake.

  Huu msemo wangu "mawe mepesi mikononi ila mazito usoni", unamaana kuwa, kwa wananchi wenye uchungu, ni rahisi kuyachukua hayo mawe bila kusikia uzito wake, na yatagundulika kuwa ni mazito, pindi yatakapotua usoni mwa mlengwa.

  Natoa onyo kali kwa viongozi( watawala), wanaojitokeza kwenye mikutano ya hadhara na kutamka senteso nyepesi zenye kebehi na zinazoudhi, adhabu yao, itakuwa zaidi ya hii ya nyangw'ine.

  Pia watambue kuwa amani haipo tena tanzania, bali kuna utulivu tu, utulivu huu, ukitibuliwa hata na sisimizi, ni lazima haya ya tarime yatokee, hii ni mara ya pili katika mwezi huu wa tano, kwa tukio la aina hii kutokea, tumeona jinsi lamwai alivyoabishwa kule jimboni kwake kwa kupigwa mawe, je, hii ndio aina ya uwajibishajia wanayoitaka ccm ili wabadilike? basi na sisi wananchi tumegundua kuwa, njia nzuri ya kufikisha ujumbe kwao ni hii, ya kuwachapa mawe mepesi mikononi, na yakitua usoni mwao, yanadhihirisha uzito wake.

  Na sio tu kwa nyambari, ila tukio hili litawafuata wote waliomsaidia kuingia bungeni, akina wasira, mama kabaka wale wote tunaowajua n.k, pia kwa viongozi wengine wenye kejeli, mizaha na dhihaka nao wamo kwenye orodha.

  Nashukuru Bwana mwita waitara aliyekuwa mgombea ubunge Tarime (CHADEMA), hakuwepo kule Tarime, vinginevyo wangemsingizia kuwa yeye kawachochea na kuwatuma watu wakampe kichapo nyang'wine.

  Chacha Wangwe (Rasta) bado anaishi mioyoni mwa wanatarime, aliowafundisha kuukataa unyanyasaji, uonevu na dhuluma. R.I.P Wangwe.


  KILA MWENYE PUMZI NA APUMUE KWA NGUVU BILA MALIPO - Nyakarungu
   
 2. Columbus

  Columbus JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,010
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Tumechoshwa na maneno ya kejeli pamoja na ahadi hewa zisizotekelezeka ili mradi upigiwe kura za ushindi.
   
 3. N

  Nyakarungu JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2011
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  Ndugu distazo,
  sijakuelewa naomba msaada wako maana naona hapo kwenye red kama vile sijakuelewa umemlenga nani, mimi au nani
   
Loading...