Una ushauri gani kwa vyama vilivyosusia uchaguzi mdogo kwa uchaguzi mkuu 2020

MLAU

JF-Expert Member
Aug 23, 2007
4,726
3,354
Tumeona uchaguzi uliofanyika jana 13 January 2018 katika Majimbo mawili huko Ruvuma na Singida na baadhi ya kata kadhaa kuna vyama vilisusia uchaguzi huo kwa kusema kuwa ktk uchaguzi wa mdogo kama huo kwa kata 43 havikutendewa haki kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi na hata sheria ya vyama vingi ya mwaka 1992.

Sasa na imani kuna uchaguzi mkuu 2020 kwa mujibu wa sheria je una maoni gani kwa vyama vilivyosusia uchaguzi huu mdogo?

Viendelee kususia hivi hivi mpaka vitakapotendewa haki?

Vishiriki hivyo hivyo hata kama havitatendewa haki?

Vipiganie kutendewa haki kipindi kabla ya maandalizi ya uchaguzi?

Au una maoni mengine? na ni yapi?
 
Uwoga wa watanzania uko palepale katika kila angle
 
kutotendewa haki kwenye uchaguzi maanake kuna taratibu za kisheria zilikiukwana ikiwa hivyo ndivyo ilivyokua basi waathirika walipaswa kuchukua hatua nyingine za kisheria tofauti na kususia uchaguzi. Vinginevyo kitendo chao cha kuchelea kufanya kinaonyesha kua madai yao hayana msingi wowote. Inawezekana kabisa walijua watashimdwa na hivyo wamekwepa aibu hiyo kijanja kwa kususia uchaguzi.
 
Kama kwenye fomu kuna vyama 10 vinaonekana vilishiriki basi inatosha. Vyama vingine ni Sacco's za watu ndio maana havikushiriki.kujadili Sacco's za watu nikutowatendea haki.
 
Ni kosa kubwa limefanywa kwa kususia. Pamoja na kwamba tunajua uchaguzi si wa haki na uhuru na umejaa hila za kila aina ikiwemo kuuawa na wizi wa kura wa kufa mtu. Mazingira ya uchaguzi huu ndiyo hayo hayo yatayokuwepo 2020, Je, 2020 pia watasusia?
 
Na uhakika hadi 2050 mazingira yatakuwa haya haya yaliyowafanya wasusie leo na itakuwa ukichaa kushiriki 2020 halafu waanze tena kulialia kuibiwa.

Mbowe anaogopa vuguvugu la kuambiwa aachie ngazi kutokana na matokeo mabovu tu na siyo kingine ilhali Zitto anataka CDM wamuone ana-interests kama zao arejee kundini.
 
kutotendewa haki kwenye uchaguzi maanake kuna taratibu za kisheria zilikiukwana ikiwa hivyo ndivyo ilivyokua basi waathirika walipaswa kuchukua hatua nyingine za kisheria tofauti na kususia uchaguzi. Vinginevyo kitendo chao cha kuchelea kufanya kinaonyesha kua madai yao hayana msingi wowote. Inawezekana kabisa walijua watashimdwa na hivyo wamekwepa aibu hiyo kijanja kwa kususia uchaguzi.
twaweza oyeee
 
Tumeona uchaguzi uliofanyika jana 13 January 2018 katika Majimbo mawili huko Ruvuma na Singida na baadhi ya kata kadhaa kuna vyama vilisusia uchaguzi huo kwa kusema kuwa ktk uchaguzi wa mdogo kama huo kwa kata 43 havikutendewa haki kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi na hata sheria ya vyama vingi ya mwaka 1992.

Sasa na imani kuna uchaguzi mkuu 2020 kwa mujibu wa sheria je una maoni gani kwa vyama vilivyosusia uchaguzi huu mdogo?

Viendelee kususia hivi hivi mpaka vitakapotendewa haki?

Vishiriki hivyo hivyo hata kama havitatendewa haki?

Vipiganie kutendewa haki kipindi kabla ya maandalizi ya uchaguzi?

Au una maoni mengine? na ni yapi?
Viendelee tu kusisia hlf subiri tuvipe ushauri ifikapo 2021 baada ya uchaguzi mkuu.
 
Ni kosa kubwa limefanywa kwa kususia. Pamoja na kwamba tunajua uchaguzi si wa haki na uhuru na umejaa hila za kila aina ikiwemo kuuawa na wizi wa kura wa kufa mtu. Mazingira ya uchaguzi huu ndiyo hayo hayo yatayokuwepo 2020, Je, 2020 pia watasusia?
Swali kwa waliosusia...ukishiriki unaongeza kuonyesha mapungufu wazi wazi na hata sababu za kuonewa kama kupo kunakuwa wazi kuliko kususia ambako kuna watu wanaficha mapungufu.
 
Ofisi ya msajili wa vyama ivifute, kuna vyama vya siasa havijawahi kushiriki siasa achilia mbali uchaguzi tangu visajiliwe. Vimekuwa vikitumika kuhalalisha matokeo ya uongo ya tume ya uchaguzi. Hivyo vyama havishiriki sikuhizi tumekuwa tukiviona kwenye matokeo ya uchaguzi tu ili kuonyesha eti kuna demokrasia ya vyama vingi Tanzania. Msajili avifute vyote ibaki ccm na polisi itapendeza.
 
Polisi siyo chama au wewe ndo umekisajili?
 
Hahaha nilisahau nilidhani ni chama, mbona huwa wanashiriki kampeni na uchaguzi?! Nilisikia Tanzania kuna amani lakini polisi hushiriki kampeni na uchaguzi lakini hawajawahi kushinda, basi nao msajili awafute tu.
 
Wakifutwa Polisi basi wataletwa JWTZ
 
Wakifutwa Polisi basi wataletwa JWTZ
Hahaha yote sawa tu ilimradi hawagawani kura na ccm waletwe tu.
Nchi hii chama kimoja tu, ccm hao wengine nisawa na polisi tu, wanashiriki kampeni na uchaguzi lakini hawajawahi kushinda.
 
Kama kwenye fomu kuna vyama 10 vinaonekana vilishiriki basi inatosha. Vyama vingine ni Sacco's za watu ndio maana havikushiriki.kujadili Sacco's za watu nikutowatendea haki.

Na kama kwenye vyama kumi vilivyoshiriki uchaguzi vinapata kura 0 basi haviko katika mduara wa vichwa vya watanzania.Hivyo basi CCM ilishindana na kivuli chake mwenyewe
 
Back
Top Bottom