Una tambua afya yako ?! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Una tambua afya yako ?!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tumsifu Samwel, Mar 10, 2010.

 1. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #1
  Mar 10, 2010
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  KIJANA NA MALENGO/LENGO LA KWANZA KWA KIJANA NI KUJITAMBUA KIAFYA.

  Nina kila sababu ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa ulinzi wake kwetu sisi kama vijana .kwa maana bila yeye hakuna tuwezalo maana ni neema yake ituongezayo kila siku.

  Nirejee kwenye mada yangu naamini kila kijana ana malengo yake katika maisha na malengo yetu yanatofautiana ila tunalo lengo moja na ambalo ni muhimu kwa kila kijana ,na lengo hilo ndilo lengo la kwanza kwa kila mtu najua msomaji utajiuliza ni lengo gain ,unajiuliza hivyo kwa sababu wengi tume kuwa tukilipuuza tukiliona si muhimu kwetu ila inapofika wakati ndiyo tunalikumbuka kuwa ni muhimu na wakati huo tunakuwa tumechelewa ,nalo si lingine ni lengo la kujitambua afya yetu .

  hili ni lengo muhimu na ni la kwanza kwa kila mwenye malengo na anaye hitaji kutimiza malengo yake ni lazima hilo la afya alipe kipaumbele maana ndilo linalobeba maisha yetu ukijitambua kiafya utakuwa na wakati mzuri wa kujipanga kutimiza malengo yako kuna vijana wengi ambao wameshindwa kutimiza malengo yao kwa sababu tu walipuuza lengo la kwanza la kujitambua kiafya .

  Hebu fikiria vijana wanaochaguliwa kujiunga na vyuo vikuu upewa fomu ambazo hutakiwa wakapime afya zao ili majibu wayapeleke kwa viongozi chuoni lakini vijana wengi kwa kutotambua umuhimu wa jambo hilo lengo la kwanza katika maisha yao uchukua fomu hizo na kuwafwata madaktari na kuwapatia ela kuanzia Tshs 5000/= ili wawajazie bila kupima jambo ambalo mimi naliona ni hatari kubwa sana kwa vijana hao.

  Umuhimu wa kujitambua kiafya nakumbuka mnamo mwaka 2002 nilitambua umuhimu wa kujitambua kiafya ambapo niliamua kupima VVU na majibu kuonyesha nimeambukizwa virusi vya ukimwi (VVU) ila toka hapo nimekuwa nikijipanga vema kutimiza malengo yangu lakini bila kujitambua naamini leo ningekuwa nimeshafariki kwa sababu kujitambua kwangu kumenifanya nijilinde na kujitulinza vema hebu jiulize wewe mwenyewe utajitambua lini? Wengi wamepoteza maisha na mwelekeo kwa sababu tu wamechelewa kujitambua mapema.wapo hawajajitambua ilo ni tatizo kubwa sana kwa vijana .

  Hivi karibuni nilikuwa kwenye mkutano wa vijana wa Afrika waishio na VVU uliofanyika nchini Bostwana ambaopo moja ya mada ilikuwa ni umuhimu wa vijana kujitambua kiafya ila hapa nchini kwetu kuna tatizo lingine ambalo linachangaia sana vijana kutoona kuwa hilo ni lengo umuhimu nalo t unyanyapaa ambao uanzia kwa kijana mwenyewe ,serikali na kwa jamii inayomzunguka kwa mfano kunatetesi kuwa kuna chuo kikuu kimoja nchini kuna vijana waishio na VVU wamejiunga na chuo hicho na vijana hao bado hawajawa wazi juu ya kuishi kwao na VVU ikumbukwe ili mtu awe wazi anahitaji maandalizi ya kutosha maana kuwa wazi kuna faida na hasara zake shariti uzitambue zote hizo si kitu cha kukurupliuka ,sasa tatizo lililopo chuoni hapo baadhi ya wanachuo kwa sababu hawana elimu sahihi ya ukimwi wantaka wenzao hao watangazwe au wafukuzwe chuoni hapo hiyo si haki kabisa na wala huo si ufumbuzi wa tatizo bali ni kuongeza tatizo haya yote yanatokea kwa sababu vijana wengi hatuna elimu sahihi ya ukimwi na staid za maisha .Wito wangu kwa vijana nawaomba watambue lengo lao la kwanza katika maisha yao ambalo ni kuzitambua afya zao na wakikuta wameambukiza VVU usikate tama maisha yanaendelea.
   
 2. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #2
  Mar 10, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,577
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  Ndio natambua!
   
 3. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #3
  Mar 10, 2010
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Vizuri sana kama unatambua afya yako,usisite kuwa elimisha na wenzio nao wacheki afya zao ili wajitambue.
   
Loading...