Mkuu mimi naomba msaada jinsi ya kufungua app ya kibiashara kama ilivyo ile ya KIKUU. Ambayo mteja anaweza akafanya malipo ya moja kwa moja na kuweka idadi ya bidhaa anazo hitaji n.k.
App kama ya kikuu una maanisha "online shopping application"
Zipo za aina tatu,kuna B2B,B2C na C2C
Na assume hapa una maana ya B2C ikiwa wewe kama mmiliki Wa application ndiyo supplier Wa bidhaa (Business) na watumiaji Wa application yako ndiyo customers (C)
Kama tayari una bidhaa na unauzoefu Wa kuuza bidhaa yako (offline) kuingia kwenye online business ni rahisi. Tofauti ni kwamba duka au store yako inakua ndani ya simu ya mteja wako
Sasa kuna aina mbili za applications
Tuna native application, hizi zinauwezo Wa Kufanya kazi kwenye aina moja tu ya operating system kama Android au IOS
So kama unahitaji native application, unahitaji team mbili za developers watakao design app mbili tofauti moja kwa android na nyingine kwa iOS (iPhone)
Aina ya pili ni cross platform application, hii ni app moja yenye uwezo Wa kufanya kazi kwenye operating systems zote mbili yaani Android na iOS
Hapa utahitaji developer au team moja ya developers kwa ajiri ya Ku develop hii app
Utaona hapo juu,cross platform application ndio changua bora zaidi kwa sababu ina gharama nafuu ukilinganisha na native applications zinazohitaji team mbili tofauti za developers
Note:native app na cross platform app kwa 99% zina utendaji sawa kabisa
Sasa tuje kwenye cost na jinsi gani unaweza kuipata app aina ya kikuu
Hapa unaweza tafuta software developer mwenye angalau uzoefu Wa mwaka mmoja Wa Ku develop cross platform application
Bei inategemea developer na developer ila INA cheza from 500k na zaidi inategemea na vitu gani (features) unataka ziwemo kwenye application
Ukiacha kutafuta developer,kuna soko LA mtandaoni maalum kwa ajiri ya kununua application za namna hio
(Japo hii sio njia nzuri zaidi kwa sababu unaweza pata application ambayo haina feature unazozihitaji au utakazo zihitaji baadae)
I hope nimekujibu,karibu
NB:hakikisha una uzoefu Wa hio biashara offline