Una swali lolote kuhusu online business, website, mobile apps, technologies zinazotumika, na ushauri kabla hujaamua kuwa na website au app ya biashara

Kuchwizzy

JF-Expert Member
Oct 1, 2019
555
1,000
Habari wakuu,

Kama kichwa cha habari kinachojieleza huu Uzi maalum kwa wale wote wenye maswali kuhusu jinsi ya kumiliki website au app kwa ajiri ya biashara yako

Vitu unavyopaswa kuvifahamu kabla hujaamua kumtafuta IT kwa ajiri ya ku "develop" website/app ya biashara yako

Pia ni vizuri ukafaham technologies zinazotumika Ku develop hizi apps au websites na zipi ni nzuri zaidi kulingana na wazo au biashara yako

Pia kama tayari una miliki online business (website au app) na unahitaji ushauri Wa kitaalam jinsi gani unaweza Ku "scale" app au websites yako iwafikie watu wengi zaidi

Na kama una wazo lolote la online business na Wenda hujui jinsi ya kuliweka sawa sawa hapa ni pahala pake

Mi web & app developer so nitajitahidi kujibu swali lako kadri nitakavyoweza

JINSI YA KUTENGENEZA BIASHARA YAKO MTANDAONI(ONLINE BUSINESS)

1.Kutambua tatizo
Hii ni hatua ya kwanza na ya muhimu katika safari yako ya kuanzisha biashara ya mtandaoni(online business),
Biashara zote za mtandaoni zilizofanikiwa na zitakazo kuja kufanikiwa huwa zina sifa moja kubwa,
Kutatua tatizo....
Fikiria ni kwa kiasi gani upatikanaji wa video ulikua ni changamoto kabla ya YouTube?

Au upatikanaji wa taarifa kwenye internet kabla ya Google?

Au mawasiliano ya haraka na salama yalivyokua changamoto kabla ya WhatsApp, Signal au Telegram?

Jinsi gani ilikua ngumu Ku interact na marafiki kabla ya Facebook?

Kujua watu mashuhuri wamesema nini kabla ya Twitter?

Mitandao yote hii imefanikiwa baada ya kutatua tatizo Fulani

Ni Aidha unatatua tatizo kwa kuja na jawabu jipya,au una boresha jawabu lililopo

Kama alivyosema CEO wa zamani na mwanzilishi wa Alibaba Group,Bilionea Jack Ma kuwa njia rahisi ya kugundua tatizo ni kuangalia sehemu zipi zina malalamiko mengi?

Mfano,Vijana wengi wanalia na ukosefu wa ajira?,una jawabu lipi Ambalo una amini litatatua au kupunguza ili tatizo?

2.Utekelezaji(implementation)
Baada ya kupata jawabu lako,sasa ni mda sahihi wa kulitekeleza....(itaendelea)

Karibuni

0748333586
 
Capital

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
1,365
2,000
Asante sana hii ndo nilikuwa natafuta. Ushauri ni bure au tunalipia?
 
Kuchwizzy

JF-Expert Member
Oct 1, 2019
555
1,000
Mi nataka kufungua online TV nifanyeje
By "Online TV" na assume una maana ya YouTube Channel
Kitu kikubwa cha kuzingatia hapo ni Quality na Quantity za content unazoweza kuzitengeneza

Ni kwa kiasi gani utaweza kuweka content zake,mfano una upload content(video) mpya baada ya mda gani?
(Aidha kila baada ya wiki moja,au kila baada ya siku ngapi,inategemea umejipanga vipi)

Pia content unazoziweka zina quality kiasi gani,kwanzia camera utakayo/utakazo tumia,level ya editing utakazofanya

Mtazamaji ataheshimu Online TV yako baada ya kuona quality ya content utakazo upload pale

Kitu kingine cha kuzingatia ni utayarishaji wa content zako,hakuna tofauti kubwa kati ya traditional TV na Online TV tukija kwenye Utayarishaji wa content

So jitahidi kuwa professional kidogo kwenye uandaaji wa content zako

Pia usisahau kuwa relevant, content utakazo upload ziendane na maudhui/jina LA Online TV yako

Kama online TV yako ni "AfyaHub" kwa mfano
Basi mtazamaji anategemea kukutana na content zinazohusiana na Afya

Cha mwisho,chagua "niche" au aina gani ya content utakazo deal nazo

Kama ni habari za udaku,Afya,Burudani,Biashara etc
Zingatia consistency, kama unaamua Ku upload new content kila wiki Basi iwe hivyo

Note: Jitahidi kuwa original kidogo kwenye content zako,YouTube wanaheshimu sana copyright issues
 
King Rabbit

JF-Expert Member
Mar 29, 2015
503

Noted!!!
 
Nov 14, 2019
6
45
Mkuu mimi naomba msaada jinsi ya kufungua app ya kibiashara kama ilivyo ile ya KIKUU. Ambayo mteja anaweza akafanya malipo ya moja kwa moja na kuweka idadi ya bidhaa anazo hitaji n.k.
 
Kuchwizzy

JF-Expert Member
Oct 1, 2019
555
1,000
Mkuu mimi naomba msaada jinsi ya kufungua app ya kibiashara kama ilivyo ile ya KIKUU. Ambayo mteja anaweza akafanya malipo ya moja kwa moja na kuweka idadi ya bidhaa anazo hitaji n.k.

App kama ya kikuu una maanisha "online shopping application"

Zipo za aina tatu,kuna B2B,B2C na C2C
Na assume hapa una maana ya B2C ikiwa wewe kama mmiliki Wa application ndiyo supplier Wa bidhaa (Business) na watumiaji Wa application yako ndiyo customers (C)

Kama tayari una bidhaa na unauzoefu Wa kuuza bidhaa yako (offline) kuingia kwenye online business ni rahisi. Tofauti ni kwamba duka au store yako inakua ndani ya simu ya mteja wako

Sasa kuna aina mbili za applications
Tuna native application, hizi zinauwezo Wa Kufanya kazi kwenye aina moja tu ya operating system kama Android au IOS

So kama unahitaji native application, unahitaji team mbili za developers watakao design app mbili tofauti moja kwa android na nyingine kwa iOS (iPhone)

Aina ya pili ni cross platform application, hii ni app moja yenye uwezo Wa kufanya kazi kwenye operating systems zote mbili yaani Android na iOS

Hapa utahitaji developer au team moja ya developers kwa ajiri ya Ku develop hii app

Utaona hapo juu,cross platform application ndio changua bora zaidi kwa sababu ina gharama nafuu ukilinganisha na native applications zinazohitaji team mbili tofauti za developers

Note:native app na cross platform app kwa 99% zina utendaji sawa kabisa

Sasa tuje kwenye cost na jinsi gani unaweza kuipata app aina ya kikuu

Hapa unaweza tafuta software developer mwenye angalau uzoefu Wa mwaka mmoja Wa Ku develop cross platform application
Bei inategemea developer na developer ila INA cheza from 500k na zaidi inategemea na vitu gani (features) unataka ziwemo kwenye application

Ukiacha kutafuta developer,kuna soko LA mtandaoni maalum kwa ajiri ya kununua application za namna hio
(Japo hii sio njia nzuri zaidi kwa sababu unaweza pata application ambayo haina feature unazozihitaji au utakazo zihitaji baadae)

I hope nimekujibu,karibu

NB:hakikisha una uzoefu Wa hio biashara offline
 
Isanga family

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
8,538
2,000
Safi sana mtaalamu nimepata kitu hapo hiyo namba yako inapatikana whatsAp ili tuwasiliane zaidi...
 
Kuchwizzy

JF-Expert Member
Oct 1, 2019
555
1,000
Youtube chanel ni lazima kulipia hata kama unafundisha na sio utoaji habari,?
Nadhani hio sheria inalenga sana watoa habari,japo kuwa imekaa kiunyonyaji sana

Kwasababu wewe ndiyo mmiliki wa YouTube Channel,na YouTube ni Mali ya Google,kampuni ya kimarekani

Ni Tanzania tu ambapo YouTube Channel zinalipiwa

Nadhani kama unalengo LA kuanzisha YouTube Channel na channel yako hailengi utoaji wa habari haswa zile sensitive unaweza usihofu kuhusu hilo suala kwa sasa mpaka labda itakapokuwa kubwa kiasi cha kuteka attention ya serikali

Kwa sababu there is no way serikali ikafungia YouTube Channel yako

Wataku face wewe kama wewe
 
  • Thanks
Reactions: Doz

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom