Mkuu tunajichukulia tunastahili sana vitu ambavyo sio haki yetu kabisa.
Unaweza ata enda lunch na jamaa ako ukamlipia chakula au kinywaji kwa kua mmezoeana hasemi ata asante. Mpenzio/rafiki anakupigia simu wakati mnaagana hata mtu hasemi asante kwa kupiga... unampisha mzee kiti kwa daladala anakaa tu kama bubu.. nk nk.
Neno asante ni neno dogo lakini nikuhakikishie halizoeleki... nikimaanisha mtu hachoki kushukuriwa kamwe. na shukrani inayogusa zaidi ni yale mambo madogo dogo ambayo hata mtu hategemei kama amekufanyia kitu cha kimaana kiivo, ila anashtukia unampa shukrani tena kwa unyenyekevu mkubwa. inagusa sana na inachagiza mtu kufanya zaidi na zaidi.
Asante ni ufunguo wa mengi mazuri ya ulichoshukuru.