Una mpango wa kukata rufaa? - Hapana "Fransis Cheka"

"Binafsi sifikirii kukata rufaa, wewe acha tu niende nikaitumikie adhabu ambayo ilishapangwa na watu wasionipenda eti kwa sababu ya kudai jasho la kazi ya mikono yangu, hawajui ni kiasi gani nilivyoweza kupata ile fedha ya mtaji wa biashara."

"Vipi kuhusu biashara yako ya kuokota chupa za maji?
Nadhani ndiyo hivyo imeshakosa mtu wa kuweza kusimamia kwa sababu mke wangu ni mjamzito, hivyo hataweza pilikapilika za kwenda barabarani kuokota chupa, ni jambo gumu sana kwa kweli, naumia lakini sina jinsi." Source - Global Publishers

Ukweli maneno haya yamenigusa sana, kwa wapenzi wa cheka hamna namna ya kumsaidia huyu mama mja mzito? Mengi/bhakresa huyu mtu alikuwa anafanyakazi ya kuokota machupa yenu ya maji sasa hamna namna ya kumsaidia kweli? binafsi naona kafungwa kwa sababu ya umasikini wake tu. IGP saidi mwema alishawahi kusema Jela sio jehanamu, naamini atarudi tu.
Sheria ni Sheria haichagui mtu wa kumuadhibu na mtu kama yeye ambae ni maarufu, anatakiwa awe kioo cha jamii kuwaonyesha mfano kwa vijana wanaochipukia katika mchezo wa masumbwi kuwa nguvu zake ni za kutumia wakati uko ulingoni.

Hakuna sababu yeyote inampa mtu haki ya kumpiga mtu yeyote kwa kosa lolote, ndio maana tuna vyombo vya sheria kama polisi na mahakama.

Kibaya zaidi alionyesha kujiamini saana maana alipopewa nafasi ya kuleta mashahidi na kujitetea aliamua kutofanya hivyo, hali ilioonyesha hakujutia kitendo alichofanya na kukiona ni sawa.

Hili ni somo zuri kwa wanaojiona kutokana na kujulikana kwao wanaweza kuwa juu ya sheria.
 
umesema mambo ya maana sana
 
You May be blind in the eye, deaf in the ear, kwamba hukuona wala kusikia Kosa alilotenda Cheka! Lakini je are You also blind in the mind kiasi kwamba hutaki kujua kwamba your Cheka alitenda jinai na anastahili kulipa in kind kwa Kosa alilotenda?! Usiwe na upesi Wa kulaumu, tafakari Pia na athari kwa upande Wa pili, poor Cheka Is paying for his deeds! So be it.

Kabla ya kulipuka, ungesoma niliyoyaandika (Kwammba 'ni kweli Cheka katenda jinai''
Sijajua unaponilaumu, au upofu unaodai ninao uko kwenye nini. Mimi sitaku kujadili mtu - ningetaka tusimjadili mtu bali twende mbele zaidi kayaangalia mazingira yanayozisibu mahakama na magereza pamoja na mifumo yetu ya sheria/hukumu.
Ungejitahidi kidogo kusoma post yangu ungeona niliyoandika!
 
suala sio cheka ni ukosefu wa haki ya mtu

Good will basi tutanue wigo tuangalie "Haki za Watu" sio iwe jambo lake kama yeye. . . . . .ili kama ni tatizo basi tulisonte once and for all
 
"Binafsi sifikirii kukata rufaa, wewe acha tu niende nikaitumikie adhabu ambayo ilishapangwa na watu wasionipenda eti kwa sababu ya kudai jasho la kazi ya mikono yangu, hawajui ni kiasi gani nilivyoweza kupata ile fedha ya mtaji wa biashara."

"Vipi kuhusu biashara yako ya kuokota chupa za maji?
Nadhani ndiyo hivyo imeshakosa mtu wa kuweza kusimamia kwa sababu mke wangu ni mjamzito, hivyo hataweza pilikapilika za kwenda barabarani kuokota chupa, ni jambo gumu sana kwa kweli, naumia lakini sina jinsi." Source - Global Publishers

Ukweli maneno haya yamenigusa sana, kwa wapenzi wa cheka hamna namna ya kumsaidia huyu mama mja mzito? Mengi/bhakresa huyu mtu alikuwa anafanyakazi ya kuokota machupa yenu ya maji sasa hamna namna ya kumsaidia kweli? binafsi naona kafungwa kwa sababu ya umasikini wake tu. IGP saidi mwema alishawahi kusema Jela sio jehanamu, naamini atarudi tu.

Sasa unatafuta msaada au unalalamikaa, pesa alizokuwa anapata kwenye masumbwi kapeleka wapi?
 
Back
Top Bottom