Una mpango wa kukata rufaa? - Hapana "Fransis Cheka"

Una mpango wa kukata rufaa? - Hapana "Fransis Cheka"

eddy

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2007
Posts
17,080
Reaction score
12,300
BONDIA mahiri wa ngumi za kulipwa nchini, Francis Cheka amehukumiwa kifungo cha kwenda jela miaka mitatu kutokana na kumshambulia aliyekuwa meneja wa baa yake, Bahati Kibanda ‘Masika' tukio ambalo lilitokea Julai 2, mwaka jana.

CHEKA5.JPG
Polisi (kushoto) akimwamuru Cheka kutoongea na simu.

Hiyo ilikuwa ni ‘breaking news' katika kituo cha redio cha E-FM, Jumatatu ya wiki hii, mara baada ya kusikia hivyo haraka tukakumbuka kuwa Cheka alikuwa na kesi dhidi ya meneja huyo, lakini kwa kuwa tukio lenyewe lilitokea zamani, kumbukumbu ya kesi itasomwa lini ilipotea, haraka tukaamua kupiga simu kwenye namba ya Cheka mwenyewe.

(Simu inaita, baada ya muda mfupi ikapokelewa). "Haloo."

FrancisCheka.jpg

Cheka akiwa na baadhi ya mikanda yake ya ubingwa.

Championi: Mambo vipi, nazungumza na Francis Cheka?
Cheka: Ndiyo, ni mimi kaka, niambie.

Championi:
Pole sana kwa matatizo, tumepata taarifa kuwa umehukumiwa kwenda jela miaka mitatu, ni kweli?
Cheka: Nimeshapoa, ndiyo hivyo kama mlivyosikia ndugu zangu.

Championi: Sasa hapo upo wapi wakati hukumu imeshatoka?
Cheka: Nipo hapahapa katika Mahakama ya Mkoa wa Morogoro, nasubiri kuchukuliwa kupelekwa kwa mkuu wa magereza kwa ajili ya kupangiwa gereza.

Championi: Hakimu gani ambaye ametoa hukumu yako?
Cheka: Kama sijakosea anaitwa Said Msuya ni Hakimu Mkazi Mwandamizi.

Championi: Kwa hiyo tunaweza kuendelea kuzungumza?

Cheka: Yaaa kaka tuendelee tu kuzungumza.


Nini kilichotokea mpaka ukakumbana na hiyo kesi?

Cheka: Kama utakuwa unakumbuka mwaka 2012 nilipigana na bondia kutoka Malawi, Chimwemwe Chiotcha kuwania mkanda wa IBF Afrika kule Arusha, kwenye pambano hilo nilipata shilingi milioni tano, ambapo kazi ya hizo, milioni mbili na nusu nikaamua kufungua baa, nyingine iliyosalia nikaitumia kwenye matumizi yangu binafsi.

Baa hiyo inaitwa Vijana Social ipo maeneo ya Sabasaba, nilimkabidhi dada mmoja anaitwa Bahati Kibanda maarufu kwa jina la Masika ili awe msimamizi.

Wakati mimi nikiwa bize na mambo mengine, mauzo yakawa hayaridhishi, sasa katikati ya mwaka jana nikaamua kwenda kuchukua funguo za ofisi hiyo kwa sababu mambo hayakuwa yakienda vizuri.

Akakataa kutoa funguo, kukatokea ubishi kati yetu na hakunipatia funguo. Nikaamua kuondoka eneo hilo, baada ya pale ndipo nikaja kukamatwa kwa madai ya kumshambulia huyo Bahati.

Nikapelekwa polisi, nikatolewa kwa dhamana na baada ya hapo ndipo mlolongo wa kesi ukawa unaendelea mpaka kufikia hatua hiyo ya kuhukumiwa miaka mitatu.

Unazungumziaje hukumu ya kesi yako?

Kiukweli sina cha kusema kwa sababu kesi imeendeshwa katika msingi ambayo mimi sikuridhika nayo, kwani ukweli ni kwamba sikuwahi kumpiga meneja wangu.

Naumia sana lakini hakuna anayejua maumivu yangu kwa sababu kuna mambo mengi yamejificha wakati wa uendeshaji wa kesi yenyewe, mfano sikuwahi kuambiwa nipeleke shahidi kama inavyotakiwa, kitu kinachonifanya nihisi kuwa hakimu pengine alikuwa anatafuta umaarufu wa kunihukumu.

Mimi sina kawaida ya kupigana nje ya ulingo kwa sababu naheshimu kazi ya mikono yangu, lakini sina jinsi kwa kuwa kuna kikundi cha watu wachache ambao hawapendi kuona Cheka akipata mafanikio, wamechangia katika hili.

"Ninaamini kuwa pengine kitendo cha kudai bati kwa viongozi wa Serikali ya Morogoro ambazo niliahidiwa na Rais Jakaya Kikwete baada ya kushinda pambano langu dhidi ya Phil Williams wa Marekani, kimechangia maana walikuwa wakinizungusha.

Una mpango wa kukata rufaa?

Binafsi sifikirii kukata rufaa, wewe acha tu niende nikaitumikie adhabu ambayo ilishapangwa na watu wasionipenda eti kwa sababu ya kudai jasho la kazi ya mikono yangu, hawajui ni kiasi gani nilivyoweza kupata ile fedha ya mtaji wa biashara.

Nadhani ndugu zangu pamoja na mashabiki wanaweza kufanya hivyo ila siyo mimi, kwa upande wangu miaka mitatu siyo mingi, najua itaisha tu halafu nitatoka, sina cha kuhofia kwa sababu sikuanza mimi kwenda gerezani.

Una neno gani kwa mashabiki wako?

Waendelee kuniombea huko niendako, kwa sababu nitarejea kwa uwezo wa Mungu, fitina za watu wachache zisiwakatishe tamaa.

Vipi kuhusu biashara yako ya kuokota chupa za maji?

Nadhani ndiyo hivyo imeshakosa mtu wa kuweza kusimamia kwa sababu mke wangu ni mjamzito, hivyo hataweza pilikapilika za kwenda barabarani kuokota chupa, ni jambo gumu sana kwa kweli, naumia lakini sina jinsi.

Mambo yangu mengi yatakufa kwa sasa, kwa sababu mwenyewe sitakuwepo uraiani.

Mwana naona jamaa wamekuja kuninyanyua ndiyo naelekea kupanda gari kuelekea kwenye makazi yangu mapya ambapo nitakuwepo huko kwa miaka mitatu, ila fanya hivi…(akawa azungumzi ila simu ipo hewani)

Championi:
Haloo! Haloo! Cheka bado upo hewani? (upande wa pili kimyaa, ila simu ipo hewani, baada ya muda ikakatwa)

Baadaye kupitia runinga ilionekana kumbe Cheka alikuwa akizungumza na sisi muda huo mpaka alipokaribia kupanda kwenye gari, ndipo askari wakamnyang'anya simu na kumtaka apande. Safari ikaanza kuelekea gerezani.

Baada ya hapo, mkewe, Tosha Azenga aliyekuwa mahakamani aliangua kilio kikubwa, tukaamua kumwacha atulie kwa siki mbili, kisha juzi tukawasiliana naye na mazungumzo yetu yalikuwa hivi:

Ulijisikiaje baada ya hukumu kutolewa?

Binafsi sikuamini kile alichokisema hakimu, niliishiwa nguvu kabisa, kwa sababu ya uchungu, adhabu aliyopewa ni kubwa sana hata kama amekosea.

Umejipangaje baada ya hicho kilichotokea?

Kiukweli maisha yatakuwa magumu sana kwa upande wangu, maana Fransic ndiye alikuwa nguzo ya familia, mimi ni mjamzito na sina uwezo wa kufanya kazi ngumu, pia nina mtoto anaitwa Heshima anayesoma shule ya msingi.

Utaendeleza biashara yake ya baa?

Mimi sijui vizuri kuhusu hiyo biashara yake kwa sababu muda mwingi tulikuwa tunafuatilia kesi.

Vipi kuhusu bati alizoahidiwa?

Alikuwa akifuatilia tangu Joel Bendera alipokuwa mkuu wa mkoa huu (Morogoro) na hata baada ya Bendera kuhamishwa hakupewa hizo bati zenyewe.

Una neno gani kwa jamii?

Naomba serikali itusaidie, angalau wangemfunga hata kifungo cha nje, kwani sisi wote akiwemo baba yake mzazi ambaye ana matatizo ya macho tunamtegemea yeye.

Source: Global Publishers

========



"Binafsi sifikirii kukata rufaa, wewe acha tu niende nikaitumikie adhabu ambayo ilishapangwa na watu wasionipenda eti kwa sababu ya kudai jasho la kazi ya mikono yangu, hawajui ni kiasi gani nilivyoweza kupata ile fedha ya mtaji wa biashara."

"Vipi kuhusu biashara yako ya kuokota chupa za maji?

''Nadhani ndiyo hivyo imeshakosa mtu wa kuweza kusimamia kwa sababu mke wangu ni mjamzito, hivyo hataweza pilikapilika za kwenda barabarani kuokota chupa, ni jambo gumu sana kwa kweli, naumia lakini sina jinsi."

Ukweli maneno haya yamenigusa sana, kwa wapenzi wa Cheka hamna namna ya kumsaidia huyu mama mja mzito? Mengi/Bhakresa huyu mtu alikuwa anafanya kazi ya kuokota machupa yenu ya maji sasa hamna namna ya kumsaidia kweli?

Binafsi naona kafungwa kwa sababu ya umasikini wake tu. IGP saidi mwema alishawahi kusema Jela sio jehanamu, naamini atarudi tu.
 
Francis Cheka ana athari za ngumi ambazo alipigwa na mabondia aliocheza nao. Kama ambavyo Mohamed Ally alivyopata Parkinson Syndrome au Rashid Matumla anapoongea kama mtu àliyetumia dawa za kulevya basi Cheka imemuathiri uwezo wa kufikiri sahihi.

Hilo soo angeweza kulimaliza kwa kuongea na mdai wake nje ya mahakama lakini ubongo wake hauoni hayo.
 
Mfumo wetu wa sheria unahitaji kujengwa na kupanuliwa ili uweze kutilia maanani hali ya bondia huyu na familia yake pamoja na wanafamilia watakaoathirika na hukumu.
1. Ni kweli katenda jinai
2. Ni kweli anastahili adhabu
3. Lakini ni kweli anamdai mhanga wake! Tatizo la mifumo yetu ya sheria imezingatia kutoa adhabu na wakati mwingine kukomoa na ni vigumu kuweza kupima mfungwa anasaidikaje anapofungwa gerezani. Kuna baadhi ya kesi ambazo kifungo cha gerezani hakisaidii upande wowote katika shauri.
Cheka ni mmoja tu wa waathirika wa mifumo ya sheria ambayo ni One dimension!
 
Francis Cheka ana athari za ngumi ambazo alipigwa na mabondia aliocheza nao. Kama ambavyo Mohamed Ally alivyopata Parkinson Syndrome au Rashid Matumla anapoongea kama mtu àliyetumia dawa za kulevya basi Cheka imemuathiri uwezo wa kufikiri sahihi. Hilo soo angeweza kulimaliza kwa kuongea na mdai wake nje ya mahakama lakini ubongo wake hauoni hayo.

Mkuu nakubaliana nawe kuna siku niliwah kumuona akicheza mziki kwenye club moja ya usiku,alikuwa amekunywa lakin kikichonistua ni behaviour zake ukizingatia ni celebrity.alikuwa anacheza kwa fujo na ilikuwa ukikatiza mbele yake anakubambia be it mme au mke.
 
Mfumo wetu wa sheria unahitaji kujengwa na kupanuliwa ili uweze kutilia maanani hali ya bondia huyu na familia yake pamoja na wanafamilia watakaoathirika na hukumu.

1. Ni kweli katenda jinai

2. Ni kweli anastahili adhabu

3. Lakini ni kweli anamdai mhanga wake! Tatizo la mifumo yetu ya sheria imezingatia kutoa adhabu na wakati mwingine kukomoa na ni vigumu kuweza kupima mfungwa anasaidikaje anapofungwa gerezani. Kuna baadhi ya kesi ambazo kifungo cha gerezani hakisaidii upande wowote katika shauri.
Cheka ni mmoja tu wa waathirika wa mifumo ya sheria ambayo ni One dimension!

Kwa maoni yangu sheria haina mapungufu na ukifuatilia majibu ya Francis Cheka kwa hakimu yanaonyesha kuwa alikuwa anadhani "kuwa star" kutamuokoa ndiyo maana hakuwa anatilia maanani.

Kumbuka hata Mkuu wa Mkoa wa Morogoro aliyehama Bendera ansema hakujua kuwa Francis Cheka ana kesi. Hata wale viongozi wa ngumi kama akina Mlundwa, Alhaj Yasin wanashangaa.

Ina maana kama kichwa cha Cheka kingekuwa kizuri angewafuata kwa ushauri na wangemuambia amalizane na mlalamikaji nje ya mahakama.

Na pengine wangemsaidia na fedha ya fidia. Ila kwa kuwa mangumi aliyopigwa wakati anawatandika wenzie yameathiri medulla oblangata ya kichwa chake.
 
Kwa maoni yangu sheria haina mapungufu na ukifuatilia majibu ya Francis Cheka kwa hakimu yanaonyesha kuwa alikuwa anadhani "kuwa star" kutamuokoa ndiyo maana hakuwa anatilia maanani. Kumbuka hata Mkuu wa Mkoa wa Morogoro aliyehama Bendera ansema hakujua kuwa Francis Cheka ana kesi.

Hata wale viongozi wa ngumi kama akina Mlundwa, Alhaj Yasin wanashangaa. Ina maana kama kichwa cha Cheka kingekuwa kizuri angewafuata kwa ushauri na wangemuambia amalizane na mlalamikaji nje ya mahakama.

Na pengine wangemsaidia na fedha ya fidia. Ila kwa kuwa mangumi aliyopigwa wakati anawatandika wenzie yameathiri medulla oblangata ya kichwa chake.

Kumbuka cheka amekuwa akifatilia ahadi ya mabati kutoka kwa mkuu wa kaya kwa hiyo sidhani kama walikuwa hawajui kuwa jamaa ana kesi, ila yeye cheka karidhika, concern yangu ni huyu mama mja mzito ambaye maisha yake yalitegemea mumewe aokote makopo na chupa za maji ya kilimanjaro ndo aishi sasa itakuwaje?

kama mtu aliua watu kwa kuwakanyaga na gari akapewa faini tu, huyu aliyekuwa anadai chake ndo afungwe kweli?
 
Kwa maoni yangu sheria haina mapungufu na ukifuatilia majibu ya Francis Cheka kwa hakimu yanaonyesha kuwa alikuwa anadhani "kuwa star" kutamuokoa ndiyo maana hakuwa anatilia maanani. Kumbuka hata Mkuu wa Mkoa wa Morogoro aliyehama Bendera ansema hakujua kuwa Francis Cheka ana kesi. Hata wale viongozi wa ngumi kama akina Mlundwa, Alhaj Yasin wanashangaa.

Ina maana kama kichwa cha Cheka kingekuwa kizuri angewafuata kwa ushauri na wangemuambia amalizane na mlalamikaji nje ya mahakama. Na pengine wangemsaidia na fedha ya fidia. Ila kwa kuwa mangumi aliyopigwa wakati anawatandika wenzie yameathiri medulla oblangata ya kichwa chake.

cku ilipotoka hukumu fikra zangu za mwanzo kwa mm niijua kaichukulia kesi rahis sana kama mdau mmoja kasema awali alitakiwa amtafute mlalamikaji wayamalize pembeni pili kushirikisha wadau mbalimbali hakuna kesi ndogo kamwe.
 
Kwa maoni yangu sheria haina mapungufu na ukifuatilia majibu ya Francis Cheka kwa hakimu yanaonyesha kuwa alikuwa anadhani "kuwa star" kutamuokoa ndiyo maana hakuwa anatilia maanani. Kumbuka hata Mkuu wa Mkoa wa Morogoro aliyehama Bendera ansema hakujua kuwa Francis Cheka ana kesi.

Hata wale viongozi wa ngumi kama akina Mlundwa, Alhaj Yasin wanashangaa. Ina maana kama kichwa cha Cheka kingekuwa kizuri angewafuata kwa ushauri na wangemuambia amalizane na mlalamikaji nje ya mahakama. Na pengine wangemsaidia na fedha ya fidia. Ila kwa kuwa mangumi aliyopigwa wakati anawatandika wenzie yameathiri medulla oblangata ya kichwa chake.

Na hilo ndilo kusudio la post yangu ya hapo nyuma. Yaani mahakama isingeangalia kosa na hukumu peke yake, mahakama ingezingatia pia the state of the mind the the accused - Huyu bwana inawezekana ameathirika na mingumi

- lakini kuna wengi wameathirika na magonjwa ya akili, madawa ya kulevya, umaskini na ukosefu wa elimu ambapo mara nyingi mahakimu na sheria zetu zinawatwanga miaka kadhaa bila kuangalia mazingira na hali zao!
 
Mkuu nakubaliana nawe kuna siku niliwah kumuona akicheza mziki kwenye club moja ya usiku,alikuwa amekunywa lakin kikichonistua ni behaviour zake ukizingatia ni celebrity.alikuwa anacheza kwa fujo na ilikuwa ukikatiza mbele yake anakubambia be it mme au mke.

Ha haaa Bwana Mapesa!!! Na wew alitaka kukubambia wakati we ni Me,(dume)
 
Na hilo ndilo kusudio la post yangu ya hapo nyuma. Yaani mahakama isingeangalia kosa na hukumu peke yake, mahakama ingezingatia pia the state of the mind the the accused - Huyu bwana inawezekana ameathirika na mingumi - lakini kuna wengi wameathirika na magonjwa ya akili, madawa ya kulevya, umaskini na ukosefu wa elimu ambapo mara nyingi mahakimu na sheria zetu zinawatwanga miaka kadhaa bila kuangalia mazingira na hali zao!

Defence against Criminal Liability- Insanity
 
Kwa hiyo kama kuna watu wanaotaka kumsaidia kukata rufaa inabidi waanze na issue ya insanity! Waombe akapimwe akili pengine anastahili kukaa Milembe kuliko pale gereza la mkoa wa Morogoro.
 
Kwa hiyo kama kuna watu wanaotaka kumsaidia kukata rufaa inabidi waanze na issue ya insanity! Waombe akapimwe akili pengine anastahili kukaa Milembe kuliko pale gereza la mkoa wa Morogoro.

pia tunaweza peleka ombi kwa rais ampe msamaha katika sherehe za muungano.
 
kumbe alikuwa ana mradi wa kuokota makopo ?. alafu ni mtu maarufu.

huyu jamaa atakuwa na kasoro za akili.

hapana kuokota makopo sio wehu ndo ajira zilizobaki mjini.
 
Acha ku dharau biashara za watu wengine, Kuna mtu namjua kwa siku anatengeneza 10000 kwa kuokota chupa, haya tuambie wewe kwa siku una make bei gani.. wa hapahapa
 
Last edited by a moderator:
Mfumo wetu wa sheria unahitaji kujengwa na kupanuliwa ili uweze kutilia maanani hali ya bondia huyu na familia yake pamoja na wanafamilia watakaoathirika na hukumu.
1. Ni kweli katenda jinai
2. Ni kweli anastahili adhabu
3. Lakini ni kweli anamdai mhanga wake! Tatizo la mifumo yetu ya sheria imezingatia kutoa adhabu na wakati mwingine kukomoa na ni vigumu kuweza kupima mfungwa anasaidikaje anapofungwa gerezani. Kuna baadhi ya kesi ambazo kifungo cha gerezani hakisaidii upande wowote katika shauri.
Cheka ni mmoja tu wa waathirika wa mifumo ya sheria ambayo ni One dimension!

You May be blind in the eye, deaf in the ear, kwamba hukuona wala kusikia Kosa alilotenda Cheka! Lakini je are You also blind in the mind kiasi kwamba hutaki kujua kwamba your Cheka alitenda jinai na anastahili kulipa in kind kwa Kosa alilotenda?! Usiwe na upesi Wa kulaumu, tafakari Pia na athari kwa upande Wa pili, poor Cheka Is paying for his deeds! So be it.
 
Back
Top Bottom