Una experience gani mbaya au nzuri kuhusu kukaa kwa ndugu?

tatizo wengi wetu tumejijengea imani kwamba kukaa kwa ndug lazima utaonewa au kunyanyaswa...
Yaaan unataka ukae kwa ndug usiguswe kwa lolote kama malaika..?
Ukiambiwa osha vyombo piga deki chota maji kalishe mifugo kapike kutumwa sehém, haya yote unaona manyanyaso wakat kwenu kwa baba na mamako shida tupu au unafanyishwa kazi ngumu na wadogo zako au Kaka/dada zako wapo sebuleni wanaangalia TV na hulalamiki... Ila kwa ndug unasema unaonewa. Sikilizeni vijana huwez kukaa kwa mtu burebure umjazie choo ule ulale kama malkia, no way out utavitolea jasho tu... Alafu mambo ya kukaa kwa ndug yalikua ya kizamani sikuhiz pambana na hali yako
Njooni mumuone ndugu mwingine huyu
 
Nina uzoefu mbaya na mzuri, mzuri ndio umenona sana ingawa kauchafu kadogo kakiingia kwenye mchuzi, mchuzi unaharibika.

Nimelelewa, nimesomeshwa hadi walipoutua mzigo kwa Serikali kwenye elimu ya Juu(Chuo).

Nimekuwa mwanafamilia wa moja kwa moja nilipolelewa ingawa wazazi wangu wapo pia ila mzee ndio miyeyusho sasa(sina mapenzi naye hata kidogo, huu ni ukweli mchungu maana ndio kasababisha nikalelewe kwingine kuanzia udogoni hadi nikawa mkubwa)..

NB: Unaweza ukamlea mtoto ukidhani unamtesa na kumkomoa kumbe unamjenga/unamfunza uvumilivu, umahiri wa kupambana na shida na raha.

Walezi tusibague watoto( wako na wasio wako) katika malezi, tulee watoto kwa usawa.
Mzee alikuwa hana uwezo nn, au ujana ulikuwa mwingi akakwepa majukumu
 
Mzee alikuwa hana uwezo nn, au ujana ulikuwa mwingi akakwepa majukumu
Ujuaji tu ila.
Sio mtu wa kuelimika hata elimu ya mtaani ya namna ya kupambana hata kama hajapata elimu ya darasani(hajasoma hata darasa la kwanza). Hakutaka kabisa kutupeleka shule, alipeleka shule watoto 2 tu wa mwanzo. Wengine alikataa ila tumeipata kupitia kwa watu wengine.
 
dah...umenikumbusha, kaka yangu alinisingizia kuwa ninamkimbizia mkewe ili anifukuze tu nyumbani. Niliumia sana. Baada ya wiki mbili nikapata kazi nikahama kwake. Jeraha aliloniwekea ilinichukua muda sana kuliondoa. Na wakati huo ninatafuta kazi, natembea kama mbuzi tangatanga wa mjini, hata hormones zote zimezirai kabisa.
Hisia zimezirai polee ndugu wengine mtihani kweli
 
Kuna zile family hasa zinapatikana Dar es salaam. Yaani kila mtu anajinunulia chakula kivyake. Mfano asubuhi atakaejisikia kupika chai atajinunulia sukari yake robo na vitafunwa vyake mwenyewe. Mchana utaona huyu kaja na chips, yule kaja na mihogo , mwingine kaja na firigisi. Mpaka unafikiria hii ni familia au ni watu wanaishi ghetto tu!
Malezi ya ajabu sana mno sitaki hata kuyakumbuka asante BABU kwa ile caring yako unahakikisha nimekula nimeshiba ndio nirudi nyumbani nikalale tuu na hapo na maji ya kunywa unanipa mimi inakuwa ni kitanda tuu na mahali pa kuoga na kubadili the rest are history.
Asante dunia niliiona na kuijua na kila mara nashukuru kwa kunipokea ila daaah Mungu anajua huna mia hutakula wala kunywa
 
Back
Top Bottom