Una bidhaa na wateja haba? Ukifuata mtindo huu hapa utapata matunda ya haraka zaidi

miamiatz

JF-Expert Member
Dec 4, 2017
504
927
1. Tengeneza network pana kwa kutafuta contacts za watu wengi kupitia mitandao ya kijamii, directories, kutoka kwa marafiki. Wewe chukua details za watu kila unapoona jina la mtu na details zake beba. Hifadhi namba hizo kwenye simu yako kwa kuunda group of contacts na uliite Leads.

2. Andaa ujumbe mzuri wa kujitambulisha na kuitambulisha bidhaa yako ambao utakuwa ukituma kwa kila mtu iwe ni kupitia Whatsapp, sms, Messenger, Telegram, ama app yoyote ya mawasiliano. Mathalani kamna unatoa huduma ya kuwasajilia watu biashara ama makampuni basi tuma ujumbe wenye kueleweka kuwa unafanya usajili kwa gharama gani na mtu atarajie kupata cheti cha usajili baada ya muda gani.

3. Kuna watakaokutafuta. Inakadiriwa kati ya watu 100 utakaowasiliana nao angalau watu 7 (7%) watakutafuta na kufanya nao biashara. Hii ina maana ili ufanye biashara zaidi lazima uhakikishe kila siku unasaka namba za watu. Inaweza kukulazimu kuajiri kijana awe kazi yake kusaka namba za simu na details za watu tu mitandaoni na mitaani. Hata kama unasikiliza kipindi cha mahojiano kwenye TV na mhojiwa akataja namba yake we inakili hata kama ni mwanasiasa, ama hata kama ni Dokta Mwaka. Hifadhi kila namba ikupitiayo machoni pako.

4. Jenga mahusiano na wale wanaokutafuta. Social issues kama birthday, sikukuu, etc hakikisha unawatumia ujumbe mzuri. Kujenga nao mahusiano ni muhimu sana ili wakusaidie kutangaza huduma ama bidhaa yako kupitia word of mouth.

5. Jiunge katika magroup ya kila aina iwe ni Whatsapp, Facebook, etc na katika hayo magroup chukua contacts za kila member aliyepo humo. Siku hizi kujua majina ni rahisi sana mana ukiingiza kwenye app kama ya Tigopesa majina huja.

6. Hakikisha siku ifikapo jioni unakusanya contacts za watu angalau 10.

Njia hii hufanya kazi zaidi kuliko kujitangaza mitandaoni. Pia mtu akipokea ujumbe yeye kama yeye huupa kipaumbele kuliko ujumbe aliouona kwenye group la Whatsapp, Facebook, Telegram, etc.
 
Yes uzi mzuri. Na hii ina apply hata kwa mwenye biashara established. Mteja anapokuja dukani kwa amra ya kwanza hakikisha unahukua details zake na pengine alichonunua. ext time ukiwa na discounts au offers uaanza na hao wateja wako, unawatumia jumbe kuwajulisha.
 
Upo sahihi kabisa... Unafahamu application yoyote inayoweza ku automate data collection kwa ajili kukusanya contact details?

Uzi mzuri bro...thanks...
 
Back
Top Bottom