Umuhimu wa Sensa ya Watu na Makazi

Rashda Zunde

Senior Member
May 28, 2022
199
231
Ukweli ni kwamba watu wenye ulemavu wana mahitaji mbalimbali, hivyo kupitia sensa itakuwa sehemu sahihi ya kushughulikiwa changamoto zao, baada ya kukamilika kwa utaratibu huo.

Kitendo cha kuwaficha wenye ulemavu hao kutawakosesha haki yao ya msingi katika shughuli za maendeleo zitakazokuwa zinaletwa na serikali katika maeneo yao.

Pia, kila mmoja ndani ya familia na jamii kwa ujumla ana wajibu wa kuendelea kuwakumbusha wazazi, walezi au familia zinazoishi na watu wenye ulemavu kuhusu umuhimu wa sensa.

Naiomba Jamii kutozingatia vitendo vya upotoshaji unaokuwa unatolewa na baadhi ya watu katika mambo muhimu kwa maisha yao, badala yake wajiandae kuhesabiwa.
 
Back
Top Bottom