joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,613
Nimejaribu kutafakari kwa kina sana kuhusu safari za Uhuru Kenyatta katika visiwa vya Jamaica na Barbado huku nikilinganisha na matatizo makubwa ya kiuchumi yanayolikumba Taifa la Kenya kwa sasa.
Katika safari hizi, Uhuru ameambatana na mawaziri watatu, 1) Mambo ya nje, 2)Elimu na 3)Utalii. Katika safari hii, rais hakutumia ndege yake, badala yake imekodishwa ndege ya kisasa na kifahari sana "Gulf stream" kwa gharama kubwa sana.
Nimekua nikijiuliza maswali kadhaa, Waziri wa Elimu katika nchi hizi anakwenda kufanya nini?, kweli Kenya, Jamaica na Barbados kuna uhusiano gani katika Elimu?.
Kuhusu Utalii, kweli Jamaica na Barbados ni miongoni mwa nchi zenye kupeleka watalii duniani au kupokea watalii kama sisi waafrica?, hivi kweli ni sahihi kwa Kenya kupoteza gharama kubwa kwa sasa kulenga watalii wa Jamaica na Barbados?. Je safari hizi katika kipindi hiki ambacho serikali ya Kenya inashindwa hata kulipa Madeni yanayoikabili KQ zinatija kwa Kenya?
Naomba kuwakilisha.