Utafute hela kiasi gani sasa?
Asilimia 26 ya watanzania wanaishi chini ya mstari wa umaskini yaani mtu 1 kati ya wanne hawezi kutimiza mahitaji muhimu ya kula kuvaa,.nk hata hao waliobaki ndio hawa wabangaizaji tu wanaishi kwa mshahara usiokutana.
Haya niambie mbona hao watu wameoa na wanaishi na wana watoto wamekua hadi kuwaoza? tena huko vijijini kwenye umaskini mkubwa? .
Mbona hawakataliwi? Mbona hawaachwi?
Au Unazungumzia Madanga?
Tafuta hela ufanye maendeleo yako na Jamii yako, mwanamke hashikiliwi kwa hela peke yake, mbona matajiri wanaachwa kila kukicha?
Kasome Maslows Hierachy of needs uone behaviour ya binadamu, binadamu akitimiza hitaji moja atahitaji lingine na hilo lingine halihusiani na pesa kabisa na ina endelea hivyo mpaka akatapokufa.
Sasa wewe tafuta hela ili upate mwanamke ukimpata anakuja kugundua una hela kweli ila ni la Saba anataka mwenye elimu kama yeye utakufa na stress utamwacha.