mkaamweusi
JF-Expert Member
- Feb 19, 2013
- 618
- 828
Mtakwimu ni mtu ambaye amesheheni na anajua jinsi ya kuzitumia statistical tools (powerful weapons), kuanzia kuamua ni data gani zikusanywe, aina gani ya data zikusanywe ili kuweza kutatua tatizo fulani katika nyanja kama biashara, uchumi, madawa ya binadamu na wanyama, utawala, uzalishaji, na nyingine nyingi, ni mtu muhimu sana kwaajili ya kuonyesha kimahesabu ni kwanini taasisi, kampuni ama mtu binafsi afanye maamuzi gani.
Mtakwimu ni mtu ambaye anaingia katika kila nyanja (multidisciplinary) anaweza kuhitajika kuzichambua data katika viwanda, mahospitalini, taasisi za kiutafiti, wizarani, bungeni na Taasisi za elimu.
Nimebahatika kukutana na watakwimu wengi mtaani,wengi wao wapo underused ama misused, mfano, utamkuta mtakwimu(statistician) ni mwalimu wa hisabati kwenye sekondari fulani ya private, ama ameingia kwenye biashara ndogo ndogo ama yupo tu nyumbani anawaza zikitoka nafasi za JKT aombe akafikiliwe mbele ya safari, ama amewekwa kuwa mdodosaji wa taarifa za kitakwimu wakati hii kazi inafanywa na wahitimu wa kidato cha nne,
Najiuliza je? Serikali kupitia nbs haioni umuhimu wa kuunda angalau mfumo wa kuwasajili wataalamu hawa ili watambulike kisheria maana ninaona miaka ya mbeleni hawa wataalamu watakuwa very needful ukilinganisha na sasa.
Pia wataalamu wa takwimu ni kwa namna gani unaweza kuwa independet na kuisaidia jamii inayo kuzunguka moja kwa moja kama walivo waalimu, wasanifu majengo, mafundi umeme na wengineo.