Umuhimu wa kutembelea makaburi upo?

Umuhimu wa kutembelea makaburi upo?

Ni muhimu sana. Hata RC tuna utaratibu wa kuwaombea misa. Ni vema ukawakumbuka bado wangali hai kiroho.
HAKUNA UMUHIMU, UAIFATE WASEMACHO MAPADRI, WALE HAWAFATI BIBLIA,

Zaburi 6:5 inasema, “Maana mautini hapana kumbukumbu lako: Katika kuzimu ni nani atakayekushukuru?”

Mtu anapokufa hawezi kukumbuka wala kushukuru au kufanya kitu chochote.
Sasa niwaulize wale mnaowaombea wafu rehema na misamaha je nani anawashukuru?

Zaburi 88:10-12 “Wafu je! Utawanyia miujiza? Au waliofariki watasimama na kukuhimidi? Fadhili zako zitasimuliwa kaburini? Au uaminifu wako katika uharibifu? Miujiza yako itajulikana gizani? Au haki yako katika nchi ya usahaulifu?”

Hivyo katika kaburi ni sehemu ya “usahaulifu”, “uharibifu” na “gizani”. Mtu aliyekufa hawezi hata kumsifu Bwana.

Zaburi 115:17 “Sio wafu wamsifuo BWANA, Wala wo wote washukao kwenye kimya;”
 
Mpe Yesu maisha no misukosuko anymore.Hachana na habari za ibada za wafu huo ni.ushetani maana unataka kujilisha upepo kwamba ukitembelea makaburi ndio misukosuko itaisha hiyo ni ibada ya wafu.
Ukiokoka tu kila kitu kitakaa sawa kwenye tatizo Yesu atakutetea na zaidi ya yote utaupata uzima wa milele.
Baada ya kifo ni hukumu ova,,hakika mungu anaweza kwa wale waaminio.
 
Niaminivyo Mimi baada ya kifo ni hukumu,kama hukutengeneza ukiwa hai basi utahukumiwa kwa matendo yako.
 
Ndugu zangu, fahamuni kuwa Mtu aliumbwa kwa vitu viwili. ( mwili ambao ni mavumbi, na pumzi iliyopuliziwa na Mungu). Hivyo, pumzi ya Mungu+mwili, kikatokea kitu kingine cha tatu ambacho ni Nafsi. Mtu anapokufa mwili hujitenga na roho. Roho hurudi kwa muumba. Nafsi huenda kuzimu au paradiso kufuatana na maisha Mtu aliyoyaishi kama ni mema au mabaya.. Katika zaburi6:5, na zaburi88:10--12, anapozungumzia kumbukumbu, anamaanisha mwili. Mwili ukitengana na roho pamoja na Nafsi, hauwezi kufanya chochote. Mwili ni sawa na gari. Ili gari litembee, lipige honi, liongeze mwendo, lipinde kulia au kushoto, au lisimame, lazima dreva awemo ndani. Dreva anaposhuka gari halita Fanya chochote.. Mtu anapokufa, mwili huharibika, Lakini roho pamoja na Nafsi haviharibiki ni vya milele. Nafsi iliyotoka kwenye mwili, iendapo kuzimu, au paradiso, huenda na vitu hivi.:--1. Kumbukumbu hazipotei, 2.Elimu aliyokuwa nayo haipotei, 3. Daraja alilokuwa nalo duniani, kama vile utajiri ,cheo,.4. Huruma, au chuki, na kupenda....Kuyahakikisha hata angalia hadithi ya kweli aliyoihadithia Bw. Yesu mwenyewe katika Luka16:19--31. (Utajiri aliyeitwa Dives, na Maskini aliyeitwa Lazaro.. Unapofanya ibada ya wafu inaamsha Nafsi za wafu yaani unatengeneza mnyororo wa mawasiliano pamoja na wafu. Na wafu ili wapate kuwasiliana nawe lazima wapate mwili ili kufanya mawasiliano na walio hai, ndiyo maana huwa wanawapagaa watoto au hata watu wazima ili kukamilisha mawasiliano kwa kuwafanya mediums,au chombo cha mawasiliano.. Angalia katabu cha Samueli 28:8---14, jinsi Mfalme sauli alivyoenda kupiga ramli kwa njia ya wafu, alipomuuliza Nabii samweli ambaye tayari alikuwa amekufa . Kupitia medium yule mwanamke wa Endori , aliongea na Samweli mwenyewe , na akambiwa Yale yayatakayomtokea baadaye. Na yalitimia....Angalizo..-- MUNGU amekataza watu kuwaomba, kuwauliza msaada wowote ule wafu , ni machukizo. Sauli mfalme aliishia kufa kama ailivyoambiwa na Samuel I kupitia medium wa Endori. . Take care.
 
Back
Top Bottom