Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,720
- 215,773
Hbari za leo wapendwa,
Kisa hiki kimemtokea jirani yangu nimeona niwaletee mpate la kujifunza hapa, bwana Juma Bakari ana umri wa miaka 75, alikuwa mfanyakazi wa serikalini, amestaafu takribani miaka 15 iliyopita, katika maisha yake ya kazini alifanikiwa kujenga nyumba ambayo anaishi.
Bwana Juma alijaliwa kupata watoto watano, wote wameoa na kuolewa na wanaishi kwenye miji yao. Bwana Juma mke wake alifariki miaka mitano iliyopita. Bwana Juma yeye ndiye muuzaji wa maziwa pale mtaani kwetu, wengi tuna bill kwake na tunamlipa kwa mwezi.
Juzi tu mvulana wa kazi imefika saa nne asubuhi anamsubiri boss wakachukue majani ya ng'ombe boss hajaamka. Kwenda kugonga mlango wa chumbani kwake kimya, mlango ulivunjwa, bwana Juma amekutwa amelala sakafuni hajitambui.
Majirani tunapewa taarifa jioni kuwa alifikishwa Muhimbili bwana Juma na kwasasa hivi yuko katika chumba cha wagonjwa mahtuti, moyo wake unafanya kazi 50% sehemu iliyobaki haifanyi kazi vizuri, ana kisukari na mapafu yake pia hayafanyi kazi vizuri.
Kwa maelezo zaidi, bwana Juma ni mtu mwenye afya njema, mara ya mwisho alimuona daktari miaka 40 iliyopita. Mara nyingi akipata homa anahisi ni malaria hivyo hununua dawa pharmacy na kusahau. Kama angekuwa na utaratibu wa kupima afya, haya yote yangegundulika zamani.