Justine Kakoko
Member
- Oct 5, 2018
- 33
- 58
Na Justine P. Kakoko
Pongezi ni kitu chochote ambacho mtu hupewa na mtu mwingine kama sehemu ya kutambua juhudi, jitihada au mafanikio yake katika ufanyaji wa jambo fulani.
Pongezi ni kitu muhimu sana katika malezi ya watoto japo yawezekana kwa kutojua wazazi/walezi wanaona ni kitu kidogo tu. Ukweli ni kwamba kama ilivyo muhimu kuwaadhibu watoto pindi wakoseapo ni muhimu sana pia kuwapongeza watoto pindi wanapotenda mambo mazuri.
Pongezi kwa watoto inaweza kutolewa katika njia nyingi kadiri mzazi/mlezi atakavyoona inampendeza. Yawezekana mzazi/mlezi akampa mtoto wake aina zifuatazo za pongezi: Moja, Maneno matupu, kwa mfano, “Hongera sana mwanangu kwa matokeo mazuri.” Mbili, Vitu kama vile pesa, vifaa vya kuchezea n.k Tatu, Muda wake, kwa mfano kumpeleka sehemu ambayo anaipenda. Nne, Kumpa huduma, kwa mfano kumsaidia kufanya jukumu lake kwa siku hiyo husika kama vile kumsaidia kufua mavazi yake. Hizi ni njia chache tu ambazo mzazi/mlezi unaweza kuzitumia katika kumpongeza mtoto wako.
Ufuatao ni umuhimu wa wazazi/walezi kuwapa pongezi watoto wao kila wafanyapo jambo zuri:-
Kutoa hamasa kwa watoto kufanya mambo mazuri zaidi. Kwa kuzingatia saikolojia ya mtoto; tabia inayopongezwa hukua zaidi na inayoadhibiwa hudumaa zaidi katika maisha ya mtoto. Mzazi/mlezi unayetoa pongezi kwa matendo mbalimbali mazuri ya mtoto wako unamtengenezea mazingira mazuri ya kuyakuza na kuyaendeleza mambo hayo anayoyafanya mtoto wako zaidi. Mtoto atakayepongezwa baada ya kufaulu mitihani yake ana nafasi nzuri zaidi ya kufaulu vizuri katika mitihani ijayo pia tofauti na yule ambaye hatopongezwa kabisa.
Kumfanya mtoto atambue kuwa unafuatilia juhudi zake. Watoto hupenda sana kujua kuwa mzazi/mlezi wake ana muangalia katika kila anachokifanya; endapo mtoto atajua/kuhisi kuwa hakuna anaye muangalia katika mambo anayoyafanya hata juhudi zake hushuka au kuondoshwa kabisa. Kwa kumpongeza mtoto wako utamfanya ajue kuwa unafuatilia juhudi zake hali itakayomfanya azidishe kufanya mambo mazuri anayoyafanya au kuyakamilisha.
Kuuelezea upendo wa mzazi/mlezi kwa mtoto wake. Kwa watoto au watu wazima, kupongezwa kunachukuliwa kama njia ya kuuelezea upendo. Moja kwa moja mtu anayekupongeza ni lazima awe na upendo na wewe, na asiyekupongeza, hata kama ana upendo na wewe ni lazima uhisi kuwa ana chuki au ajali juu yako. Mzazi/mlezi kwa kumpongeza mtoto wako utatengeneza mazingira ya mtoto wako kuhisi unampenda na unamjali sana hali itayofanya ajihisi vizuri na kujipandisha thamani yake zaidi.
Utamjengea mtoto wako kujiamini. Mtoto anayepongezwa kila anapotenda jambo fulani vizuri huwa ni mwenye kujiamini sana pindi afanyapo mambo yake ukilinganisha na yule ambaye hapongezwi kabisa. Mtoto anayepongezwa mara kwa mara hujaribu kufanya hata mambo magumu ambayo hajawahi kuyafanya kabisa ili tu apewe pongezi pindi akiyakamilisha.
Kumuongezea mtoto uwezo wa kujisimamia na kujitegemea. Mzazi/mlezi anayempongeza mtoto wake kila baada ya kufanya jambo fulani zuri anamjenga mtoto ambaye ataweza kujisimamia na kujitegemea yeye mwenyewe katika kufanya mambo yake. Mtoto anayepongezwa huweka juhudi binafsi katika kila analolifanya ili apongezwe hali hii huongeza mtoto kujisimamia yeye mwenyewe pasipo kusimamiwa na wazazi/walezi wake katika kila kitu. Mtoto anayeweza kujisimamia ni mtoto anayeweza kujitegemea katika mambo mengi.
Japo kuwa pongezi kwa watoto ni muhimu sana katika malezi chanya ya mtoto wako ni lazima uhakikishe unayazingatia mambo yafuatayo ili pongezi isishindwe kuwa njia madhubuti ya kumkuza na kumuendeleza mtoto wako:-
Pongeza juhudi na sio matokeo peke yake. Yawezekana mtoto ajafanikiwa kufikia lengo lake katika jambo fulani lakini aliweka na kuonyesha juhudi za kutosha, toa pongezi kwa mtoto huyu ili iwe hamasa zaidi katika kufanya mambo mengine yaliyopo mbele yake.
Ahadi juu ya pongezi lazima itimizwe. Mzazi/mlezi ukitoa ahadi ya kumnunulia mtoto wako baisikeli akifanya vizuri kwenye mitihani yake basi hakikisha unaitimiza, kutotimiza itamfanya mtoto ashindwe kukuamini wakati ujao pindi ukitoa ahadi nyingine, hali itakayofanya njia ya kumsaidia mtoto kwa kumpongeza isifanye kazi.
Pongezi zinazohusisha kumpa mtoto vitu zitolewe kwa umakini. Endapo mzazi/mlezi utampa mtoto wako pongezi za vitu kama vile pesa basi hakikisha unakuwa makini kutomfanya mtoto kuwa tegemezi juu ya vitu ili afanye majukumu yake yaani kwamba asijengeke kusubiri apewe vitu ili afanye jambo lolote lile. Hii itakuwa hatari katika ukuaji wa mtoto wako. Mzazi/mlezi unaweza kuliepuka jambo hili kwa kuzitumia aina nyingine za pongezi zaidi.
Mtoto anapopongezwa ni lazima aelezwe anapongezwa kwa jambo gani. Mzazi/mlezi unapoamua kumpongeza mtoto wako lazima umueleze kwa nini haswa umempongeza. Kwa mfano unapoamua kumpongeza mtoto wako kwa kumnunulia kifaa cha kuchezea kipya, mueleze “Hii ni zawadi yako kwa kusafisha chumba chako mwaka mzima bila kusukumwa, hongera sana!”
Adhabu na pongezi ni lazima viende sambamba; mzani wa mambo hayo mawili lazima uwe na uwiano sawa ili matunda yawe mazuri. Mtoto akikosea muadhibu au mkanye. Mtoto akitenda jambo zuri mpe pongezi. Kwa kufanya hivi wazazi/walezi mtajihakikishia kuwakuza watoto wenye tabia njema na bora kwa mafanikio makubwa.