Umuhimu wa kugawanya majukumu serikalini

Umuhimu wa kugawanya majukumu serikalini

Rebeca 83

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2016
Posts
15,626
Reaction score
33,495
hello JF,

leo nina wazo,kwa nini nchi yetu isigawanywe kwa zones mfano kaskazini,kusini etc,

kuwe na viongozi wa juu kwa hizo zones,

kila zone Iwe independently from each other,

Rais ndio awe mkuu wa zones zote,

wakuu,kwa mfano Rais anachofanya kuendeleza huko Chato,ndio mfano wa kuongoza kizone

kwa huo mfano,unaona umuhimu wa kuwa na kiongozi kila zone,kucreate balance .....na kupunguza gap,kwa zile sehemu zisizoendelezwa kabisa na ziilizoendelezwa,

wakuu,mnaonaje?
 
Sasa huyo rais hatatoka katika mojawapo ya hizo zones? Ikiwa hivyo utamzuiaje kupendelea zone anakotoka?
 
Sasa huyo rais hatatoka katika mojawapo ya hizo zones? Ikiwa hivyo utamzuiaje kupendelea zone anakotoka?

mkuu,hilo la zone,nilikua namaanisha,kila zone ifanye kazi bila kutegemea zone nyingine,ijiamulie -kizone,kukusanya kodi hadi kubuni miradi ya maendeleo,.sioni njia hii kama njia hii Rais ana 'mwanya' wa kuipendelea zone.
 
watu watapiga sana hela..

kumbuka miaka ya nyuma halmashauri zilipewa power za kuajiri na kupanga bajeti zao mwisho wa siku kina lakairo wakatajirika kwa kupiga hela za halmashauri via tenda janja janja.... na ajira zikawa kuanzia mama hadi mjukuu wote halmashauri moja..

magumashi ndio yamefanya centralization irudiiiii.. maana watu wanapiga hela bila huruma
 
Mkuu, hii ni kama utawala wa majimbo ambao awali ulipigiwa upatu na Chadema.
wengi walisema unajenga ukabila lakini ndo mfumo wa USA nchi iliyoendelea sana. perhaps wazo lako ni zuri ila lazima liwe kwenye katiba
 
Mawazo ya Lumumba yanachekesha sana. Au hapa ni chit-chat?

Mi ningekuelewa kama ungesema IGP, Utukufu, Public Procurement, Med Docs Recruitment, Kamati ya Maafa na Bajeti vyote vifanywe na mtu mmoja
 
Mawazo ya Lumumba yanachekesha sana. Au hapa ni chit-chat?

Mi ningekuelewa kama ungesema IGP, Utukufu, Public Procurement, Med Docs Recruitment, Kamati ya Maafa na Bajeti vyote vifanywe na mtu mmoja

hutoagi positive comment kwenye topic zangu,naungana na wale wanaosema ukimuignore mtu then asione posts zako...mfyuuuu
 
mkuu haya mawazo ya ovyo sana wakina mama wakati mwingine sio busara kujitokeza adharani kama hivi awepo MTU wakufany monitoring!
 
Mbona hamkunijibu, leo mnajidai kufanya sera.... 🙄 🙄 🙄 🙄 🙄 😡😡😡😡😳😳😳😳😳
 
Mkuu, hii ni kama utawala wa majimbo ambao awali ulipigiwa upatu na Chadema.
wengi walisema unajenga ukabila lakini ndo mfumo wa USA nchi iliyoendelea sana. perhaps wazo lako ni zuri ila lazima liwe kwenye katiba
Usifananishe maendeleo ya majimbo ya huko USA na pengine na sisi tukiwa na majimbo tutakuwa kama wao, kumbuka wao mpaka sasa wana maraisi waliopita zaidi ya 40, na sisi ndio kwanza 5, wao wametoka kwenye safari ndefu sana kufikia pale so usijidanganye.

Na pia ukigawa nchi kwa zone kiuwongozi wa kujitegemea, kuna baadhi ya zone au majimbo yatakuwa masikini sanaaaaa. Kwa mfano kuna zone zitakuwa na bandari na pengine na muradi mikubwa ya kuingiza fedha hivyo zitanufaika sana, wakati kuna zone hazina miladi yeyote ya mapato iliyomikubwa, sasa wataendeleaje!!!?

Kumbuka maendeleo ya sasa unakuta hela nyingi zinatoka kwenye mikoa fulani halafu zinakwenda kutatua shida za mikoa mingine, lkn kama itagawanywa kwa mtindo huo maana yake itakuwa hakuna maendeleo kwa baadhi ya zone na huku zone nyingine zikinufaika sana, na itafika wakati tutazihama zone zetu kwa kukosa mapato na kwenda zone nyingine na tutafukuzana kwa kudai zone hazitakiwi kuingiana kama hivyo
 
Back
Top Bottom